Takukuru Arusha yaokoa Milioni 43 zilizoyeyuka kishirikina

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 43 za wanakikundi cha imani group kilichopo Sombetini jijini Arusha baada ya fedha hizo kupotea katika mazingira ya utata.

Akiongea na vyombo vya habari Mkuu was Takukuru mkoani Arusha,Frida Wikes amesema kuwa fedha tasilimu zilizokabidhiwa kwa wanakikundi hao ni sh,Milioni 23 huku kiasi kingine kilichobaki baadhi ya wanakikundi hawajakabidhi fedha hizo.

Fedha hizo zimelipwa kutoka kwa mhasibu wa kikundi hicho Halima Mwidadi ambaye alikuwa mtunza hazina na kwamba awali aliwaeleza wanakikundi wenzake kuwa fedha hizo zimepotea kimazingara kwa kuchukuliwa na chuma ulete


Wengine waliodaiwa kuhusika na upotevu wa fedha hizo ni miongoni mwa wanakikundi saba waliokuwa wanashikilia funguo ambao wanapaswa kulipa kila mmoja sh,milioni 2.5.
IMG-20200221-WA0041.jpeg
IMG-20200221-WA0039.jpeg
IMG-20200221-WA0040.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app

Soma

 
Haa. Mama ameona mbinu yake ya kusingizia ushirikina haifanyi kazi akaamua kurudisha fedha. Pengine alikuwa amezificha na kuamua ku-test zali.
 
Nimekuja kukurukukuru nikijua imeokota kumbe imeokoa😂😂
kiswahili nacho kinamaneno pacha pacha,kinazingua!
 
Mavikoba haya ni matapeli tu, yani mtu anakutunzia hela yako wewe umekaa nyumbani tu, tena mtu au taasisi ambayo hawana ujuzi wowote na mambo ya fedha, na wakati benki zimejaa kibao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom