TAKUKURU Arusha yaokoa bilioni 1.7 zilizokuwa zimetafunwa na wajanja wachache

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Arusha{TAKUKURU} imejipambanua kufanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 1.7 ikiwa ni kodi za serikali na fedha za vyama vya Ushirika Mkoani Arusha zilizokuwa zimeliwa na wajanja wachache na kuzikabidhiwa kwa wahusika.

Akizungumza na vyombo vya Habari jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoani Arusha,James Ruge alisema kuwa kufanikisha kurejeshwa kwa kiasi hicho cha fedha ni kufuatia operesheni iliyofanywa na taasisi hiyo na kufanikiwa kuikamata kampuni ya utalii ya uwindaji Eshkesh Safarina iliyokwepa kulipa kodi ya serikali na fedha za mauzo ya chama Cha Ushirika cha ACU.

Ruge alisema kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.4 ni kodi ya serikali ya mizigo mbalimbali ambayo ilikuwa haijalipwa na kampuni ya uwindaji na Utalii ya Eshkesh ya Jijini Arusha.

Alisema kiasi cha shilingi milioni 235 ni sehemu ya shilingi milioni 904 za Chama Kikuu Cha Ushirika{ACU} zilizokuwa zimefanyiwa ubadhilifu baada ya mali za chama hicho kuuzwa kwa watu wasiokuwa waaminifu.

Kamanda aliendelea kueleza kuwa kiasi cha shilingi milioni 45.4 ambazo zilikuwa fedha za vyama vya msingi vya ushirika,posho zilizolipwa zaidi ya stahili na fedha za makusanyo ya Halmashauri ambazo hazikuwasilishwa kwenye akaunti za Halmashauri husika.

Alifafanuwa kuwa vyama vya msingi vya ushirika na sacos wilaya za Arumeru,Karatu na Longido shilingi milioni 37.7 ,makusanyo ambayo hayakuwasilishwa benki ni shilingi milioni 1.6 na posho zilizorejeshwa baada ya kulipwa isivyostahiki ni shilingi milioni 6 .

Ruge alisema kuwa TAKUKURU Mkoani Arusha katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria kwa kutumia njia kuu tatu ambazo ni pamoja na uchunguzi wa mashtaka,uelimishaji umma na utafiti na udhibiti huku ikiwashirikisha wadau ilifanikiwa kupokea taarifa 275.

Alisema katika taarifa hizo TAKUKURU ilifanikiwa kufungua majalada 127 ya uchunguzi na majalada hayo yanaendelea kuchunguzwa na uchunguzi zake zipo katika hatua mbalimbali na ushauri yakinifu umekuwa ukitolewa kwa watoa taarifa kwa malalamiko yanayoonekana kutoangukia katika sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kamanda alisema kuwa katika kipindi hicho cha aprill na juni mwaka huu TAKUKURU Mkoani Arusha imefungua mashitaka mapya matatu mahakamani.mashtaka 53 yaliendelea mahakamani yakiwa katika hatua za mwisho mwisho za kimahakama.

Alisema katika miradi ya maendeleo,TAKUKURU imetembelea na kukagua miradi hiyo iliyotelekezwa kwa fedha za serikali ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa.


IMG-20200730-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom