Takribani watoto 800 hugundulika kuwa na saratani kila mwaka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, leo Septemba 23, 2022 ameweka wazi kuwa, kila mwaka takriban watoto 800 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani nchini Tanzania hivyo kuchangia ongezeko la vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

FdVZgO-WQAgSdgx.jpg

Waziri Ummy amesema hayo katika kikao na Taasisi ya Global HOPE iliyoko Texas nchini Marekani katika mkutano wa pembezoni baada ya Mkutano Mkuu wa 77 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea New York, nchini Marekani.

"Kila mwaka takriban watoto 800 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani nchini Tanzania, lakini kama Serikali tumeendelea kuboresha matibabu ya Saratani kwa watoto ili kuokoa maisha yao." Amesema Waziri. Ummy.

Ameendelea kusema kuwa, inakadiriwa kuwa watoto wenye saratani wanaoendelea kuishi zaidi ya miaka miwili kuanzia kugundulika ni kati ya 20% hadi 40%, huku katika nchi zilizoendelea ni zaidi ya 80%, hii ni kutokana na kuchelewa kufanya uchunguzi, kuasi matibabu, gharama za usafiri na malazi, uchache wa vituo vinavyofanya uchunguzi na uhaba wa watumishi wenye ujuzi.

Aidha, Waziri Ummy alimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Hope Dkt. David Poplack Kwa msaada wanaoipatia Serikali ya Tanzania ambapo wanaoendelea kufadhili programu na kuwajengea uwezo watumishi hususan katika fani za ubingwa bobezi wa matibabu ya Saratani na magonjwa ya damu zaidi ya 10, na kutoa vifaa vya uchunguzi katika hospitali ya Muhimbili.

Sambamba na hilo, Waziri Ummy ameiomba Taasisi hiyo kuongeza idadi ya watanzania wanaopatiwa ufadhili wa mafunzo ya utoaji huduma za Saratani Kwa kada za Uuguzi, Madaktari ,Wafamasia na Wataalamu wa maabara.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwomba kujengea uwezo hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya katika kutoa huduma hizo Kwa kujenga na kuipatia vifaa vya kisasa vya huduma za Saratani.

Kwa upanda wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Hope Dkt.Polack alieleza kuwa, Taasisi hiyo ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya kuimarisha huduma za Saratani nchini.
 
Kansa ni hatari aisee "it is silent killer".Ila mtoa thread unapaswa kutoa credit kwa source ya habari it is copy and paste.all in all vizuri sana
 
Ni Kwanini watoto wengi wanakuwa na saratani? Wajiulize hilo swali kabla ya kuongelea kuhusu matibabu. Hiyo namba ni kubwa sana.

Halafu vyakula vyetu vinapigwa madawa mengi sana huko mashambani. Miaka ya nyuma ardhi yetu haikuwa na hiyo shida sijui ya wadudu. Mimea ilikuwa bila madawa mengi kama ilivyo sasa.

Cha muhimu kufanyike uchunguzi. Hao watoto 800 ni waliogundulika. Wanaweza wakawa zaidi ya hapo. Ni wengi.
 
Ni Kwanini watoto wengi wanakuwa na saratani? Wajiulize hilo swali kabla ya kuongelea kuhusu matibabu. Hiyo namba ni kubwa sana.

Halafu vyakula vyetu vinapigwa madawa mengi sana huko mashambani. Miaka ya nyuma ardhi yetu haikuwa na hiyo shida sijui ya wadudu. Mimea ilikuwa bila madawa mengi kama ilivyo sasa.

Cha muhimu kufanyike uchunguzi. Hao watoto 800 ni waliogundulika. Wanaweza wakawa zaidi ya hapo. Ni wengi.
Kwahiyo mkuu nani unapaswa kumlaumu hapo? Tuanzie hapo sasa
 
Daaah! vifo na maambukizi ya saratani kiukweli levo yake itakua juu sana,ni vile tu,vipimo na wataalamu kwa kiwango stahki.
 
Back
Top Bottom