Takriban watu 50 wamekatwa vichwa na wapiganaji wa Kiislamu nchini Msumbiji

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
8,596
2,000
Takriban watu 50 wamekatwa vichwa na wapiganaji wa Kiislamu nchini Msumbiji, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Wapiganaji hao waliugeuza uwanja wa kuchezea kandanda kuwa 'kichinjio' , ambapo walikatakata miili ripoti nyengine zinasema.
Watu kadhaa pia walikatwa vichwa katika kijiji chengine , vyombo vingine vya habari viliripoti.

Uchinjaji huo ndio tukio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi ya kutisha ambayo yametekelezwa na wapiganaji hao katika eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi la mkoa wa Cabo - Delgado tangu 2017.
Hadi takriban watu 2000 wameuawa na takriban 430,000 wengine wamewachwa bila makao katika mzozo huo katika mkoa huo ulio na Waislamu wengi.

Wapiganaji hao wanahusishwa na kundi la Islamic State , ambalo limeingia kusini mwa Afrika. Kundi hilo limetumia sababu ya umasikini na ukosefu wa ajira kuwasajili vijana wengi katika vita vyao vya kutaka kuwa na utawala wa Kiislamu katika eneo hilo.
Wakaazi wengi wanalalama kwamba wamefaidika kidogo na madini pamoja na viwanda vya gesi vilivyopo katika eneo hilo.

Map of Mozambique

Mwandishi wa BBC Jose Tembe kutoka Maputo anasema kwamba mashambulizi hayo ya hivi karibuni ndio yaliokuwa mabaya zaidi kutekelezwa na wapiganaji hao.

Watu wengi wameshangazwa na sasa wametoa wito ya makubaliano ya amani kuhusu mzozo huo, anaongezea. Wapiganaji hao walisema 'Allahu Akbar' , [Mungu ni Mkubwa} , wakafyatua risasi na kuchoma baadhi ya nyumba wakati walipovamia kijiji cha Nanjaba usiku wa Ijumaa , kilisema chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali cha Mozambique News Agency kikiwanukuu manusura wakisema.

Watu wawili walichinjwa katika kijiji hicho huku wanawake kadhaa wakitekwa , kilisema chombo hicho cha habari. Kundi jingine la wapiganaji lilitekeleza shambulio jingine katika kijiji cha Muatide, ambapo waliwakata vichwa zaidi ya watu 50 , kulingana na chombo hicho cha habari.

Wanakijiji waliojaribu kutoroka walikamatwa na kupelekwa katika uwanja wa kuchezea soka ambapo walikatwa vichwa na miili yao kukatwa katwa vipande vipande katika mauaji yalioanza Ijumaa usiku hadi Jumapili , kilisema chombo cha habari cha kibinafsi The Pinnacle News.

Maelezo ya video,
Ni kwanini wanaume hawa wanampiga risasi hadi kumuua mwanamke mtupu?

Serikali ya Msumbiji imeomba usaidizi wa kimataifa ili kusaidia kukabiliana na mashambuliaji ya wanamgambo , ikisema kwamba wanajeshi wake wanahitaji mafunzo maalum.

Mwezi Aprili , zaidi ya watu 50 walichinjwa na wengine kupigwa risasi katika shambulio la kijiji kimoja katika mkoa wa Cabo Delgabo mapema mwezi huu , watu wengine tisa walikatwa vichwa katika mkoa huohuo.

Makundi ya haki za kibinadamu pia yanasema kwamba wanajeshi wa Msumbiji pia wamedaiwa kutekeleza unyanyasaji wa kibinadamu , ikiwemo kuwakamata watu kiholela mateso na mauaji wakati wa operesheni za kukabiliana na wapiganaji hao
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,187
2,000
Watoaji wa taarifa hizi ndio maadui zetu.Wana nia mbaya na wanafanya mambo mabaya kwetu kwa faida zao.Nimeona aliyeandika taarifa hii wa BBC yuko Maputo mbali sana kusini mwa Msumbiji anasema wapiganaji hao wa kiislamu walikuwa wakitamka Allahu Akbar.Aliwasikia wapi?
Wewe unaepinga ulikuwa eneo la tukio na hukusikia wakisema "Allah Akbaru"?
 
Nelson nely

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
4,227
2,000
Watajuana huko. Kama nia yao Tz tujichanganye wamebugi. Tunafanya yetu huku. Labda waje huku upande wa tz, na wakija tunachinja kimyakimya tunawala supu. Hata hatutangazi.
 
LIKE

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
4,705
2,000
Watoaji wa taarifa hizi ndio maadui zetu.Wana nia mbaya na wanafanya mambo mabaya kwetu kwa faida zao.Nimeona aliyeandika taarifa hii wa BBC yuko Maputo mbali sana kusini mwa Msumbiji anasema wapiganaji hao wa kiislamu walikuwa wakitamka Allahu Akbar.Aliwasikia wapi?
ami..

inaonyesha unafurahia badala ya kuomboleza maafa ya wasio hatia

haya kanywe kisusio huko Cabo Delgado,si ndio hamu na kiu chako.!?
 
Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,510
2,000
Wewe unaepinga ulikuwa eneo la tukio na hukusikia wakisema "Allah Akbaru"?
Mimi sikuwepo lakini nikiwa mfuatiliaji wa habari za aina hii kote duniani nimepata uzoefu sana wa kujua wapi ni kweli na wapi ni uwongo.

Habari za kutunga kama una akili timamu ni wepesi sana kuzishika.Mfano hapo mwandishi yuko Maputo karibu na Afrika kusini lakini ana mdomo mrefu kuhusu eneo lililompakani na Tanzania.Na kila siku kukamilisha njama zahadhithi zao lazima waseme waliouwa walisema Allahu Akbar na eti walikuwa wakiwakata vichwa watu.

Inajulikana wareno wakristo ni watu makatili sana lakini nao pia hawakuwa wakiuwa watu kwa kuwakata vichwa kwenye viwanja vya mpira.

Itakuwaje waislamu wafuasi wa dini inayopinga kuuliwa watu wafanye matendo haya tena kwa watu wanaowakamata tu.
Uwezekano tukio hilo halikuwepo na kama liltokea halikutekelezwa na waislamu na hao waliotekeleza si kwa kiasi hicho wala kwa namna hiyo.

Jimbo la waislamu la Cabo lina mafuta na gesi na madini muhimu.Hicho ndio chanzo cha fitina ili ipatikane sababu ya kuwaondoa waislamu kikatili na kusiwe wa kuwaonea huruma kote duniani. Watekelezaji wa ukatili huo ni wachina,mayahudi na wamarekani.

Kwa ushahidi wa walioathirika na kulazimika kuhama ni kwamba kila walipohamishwa kwa namna hiyo haichukui muda eneo linachukuliwa na kujengwa majengo makubwa ya mbabeberu wa kichina na wenzao kila mmoja kivyake.
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
19,783
2,000
Hawa watu wanafanana na aliyeanzisha Operation No Living Thing huko Sierra Leone. Alianzisha mapinduzi ya kijeshi ili achukue madaraka aongoze nchi.

Kisha akaanzisha hiyo operation iliyolenga kuua kila mtu Sierra Leone (in case ulishangaa kwanini iitwe vile).

So alipambana aje kutawala kisha anaua kila aliye hai now unajiuliza sasa atamtawala nani? Same na hawa. Wanataka kuunda utawala wa kiislamu lakini watachinja na kuua kadri wanavyoweza sasa huo utawala utamtawala nani?
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,424
2,000
Me nimeona video waliojirekodi Wanatanka Allah Akbar and then wanachinja na wanasema muili iachwe watu waone...

Nimegundua utetezi mwingi wa haya mauaji yanafurahiwa na wenye imani kali. . Na mtu yeyote anayefurahia anakuwa na ushetani ndani yake hivyo huyo ni adui yako na sio wa kumchekea kabisa ni kijutenga nae ataweza kukudhuru.

Hata Marcon alishangazwa na Erdogan kumshambulia japo Marcon alisema ya moyoni mwake. .. we Ami kuna Muslim anayeweza kuchinja au kuua bila kutaka jina la Allah Akbar? Tuache unafiki kuna kitu hakipo sawa na kinatakiwa tiba. . Na kama hamna ni bora kunyamaza washughulikiwe hao
 
Lailah ila Issa

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
977
1,000
Mimi sikuwepo lakini nikiwa mfuatiliaji wa habari za aina hii kote duniani nimepata uzoefu sana wa kujua wapi ni kweli na wapi ni uwongo.Habari za kutunga kama una akili timamu ni wepesi sana kuzishika.Mfano hapo mwandishi yuko Maputo karibu na Afrika kusini lakini ana mdomo mrefu kuhusu eneo lililompakani na Tanzania.Na kila siku kukamilisha njama zahadhithi zao lazima waseme waliouwa walisema Allahu Akbar na eti walikuwa wakiwakata vichwa watu.
Inajulikana wareno wakristo ni watu makatili sana lakini nao pia hawakuwa wakiuwa watu kwa kuwakata vichwa kwenye viwanja vya mpira.Itakuwaje waislamu wafuasi wa dini inayopinga kuuliwa watu wafanye matendo haya tena kwa watu wanaowakamata tu.
Uwezekano tukio hilo halikuwepo na kama liltokea halikutekelezwa na waislamu na hao waliotekeleza si kwa kiasi hicho wala kwa namna hiyo.
Jimbo la waislamu la Cabo lina mafuta na gesi na madini muhimu.Hicho ndio chanzo cha fitina ili ipatikane sababu ya kuwaondoa waislamu kikatili na kusiwe wa kuwaonea huruma kote duniani. Watekelezaji wa ukatili huo ni wachina,mayahudi na wamarekani.Kwa ushahidi wa walioathirika na kulazimika kuhama ni kwamba kila walipohamishwa kwa namna hiyo haichukui muda eneo linachukuliwa na kujengwa majengo makubwa ya mbabeberu wa kichina na wenzao kila mmoja kivyake.
Nashangaa mpaka karne ya 21 the age of information bado mnatudanganya kitoto hivo....inajulikana kabisa muislam imani kali huwa ni katili kwahyo uislam wa kweli ni ugaidi..
Muhammad mwenyewe na genge lake walibaka watu,waliua watu walitesa watu ili wabadili dini...inshort walikuwa makatili zaidi ya hao wa msumbiji
 
abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
907

Vip waroma nao na genge lao walifanya nn unajua kama toka Zaman Roman empire ndio bado inashikilia rikod ya kuuwa watu wengi mpaka Sasa wakifatiwa na Mongolia
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,424
2,000
Takriban watu 50 wamekatwa vichwa na wapiganaji wa Kiislamu nchini Msumbiji, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Wapiganaji hao waliugeuza uwanja wa kuchezea kandanda kuwa 'kichinjio' , ambapo walikatakata miili ripoti nyengine zinasema.
Watu kadhaa pia walikatwa vichwa katika kijiji chengine , vyombo vingine vya habari viliripoti.
Uchinjaji huo ndio tukio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi ya kutisha ambayo yametekelezwa na wapiganaji hao katika eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi la mkoa wa Cabo - Delgado tangu 2017.
Hadi takriban watu 2000 wameuawa na takriban 430,000 wengine wamewachwa bila makao katika mzozo huo katika mkoa huo ulio na Waislamu wengi.
Wapiganaji hao wanahusishwa na kundi la Islamic State , ambalo limeingia kusini mwa Afrika. Kundi hilo limetumia sababu ya umasikini na ukosefu wa ajira kuwasajili vijana wengi katika vita vyao vya kutaka kuwa na utawala wa Kiislamu katika eneo hilo.
Wakaazi wengi wanalalama kwamba wamefaidika kidogo na madini pamoja na viwanda vya gesi vilivyopo katika eneo hilo.
Map of Mozambique

Mwandishi wa BBC Jose Tembe kutoka Maputo anasema kwamba mashambulizi hayo ya hivi karibuni ndio yaliokuwa mabaya zaidi kutekelezwa na wapiganaji hao.
Watu wengi wameshangazwa na sasa wametoa wito ya makubaliano ya amani kuhusu mzozo huo, anaongezea.
Wapiganaji hao walisema 'Allahu Akbar' , [Mungu ni Mkubwa} , wakafyatua risasi na kuchoma baadhi ya nyumba wakati walipovamia kijiji cha Nanjaba usiku wa Ijumaa , kilisema chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali cha Mozambique News Agency kikiwanukuu manusura wakisema.
Watu wawili walichinjwa katika kijiji hicho huku wanawake kadhaa wakitekwa , kilisema chombo hicho cha habari.
Kundi jingine la wapiganaji lilitekeleza shambulio jingine katika kijiji cha Muatide, ambapo waliwakata vichwa zaidi ya watu 50 , kulingana na chombo hicho cha habari.
Wanakijiji waliojaribu kutoroka walikamatwa na kupelekwa katika uwanja wa kuchezea soka ambapo walikatwa vichwa na miili yao kukatwa katwa vipande vipande katika mauaji yalioanza Ijumaa usiku hadi Jumapili , kilisema chombo cha habari cha kibinafsi The Pinnacle News.

Maelezo ya video,
Ni kwanini wanaume hawa wanampiga risasi hadi kumuua mwanamke mtupu?
Serikali ya Msumbiji imeomba usaidizi wa kimataifa ili kusaidia kukabiliana na mashambuliaji ya wanamgambo , ikisema kwamba wanajeshi wake wanahitaji mafunzo maalum.
Mwezi Aprili , zaidi ya watu 50 walichinjwa na wengine kupigwa risasi katika shambulio la kijiji kimoja katika mkoa wa Cabo Delgabo mapema mwezi huu , watu wengine tisa walikatwa vichwa katika mkoa huohuo.
Makundi ya haki za kibinadamu pia yanasema kwamba wanajeshi wa Msumbiji pia wamedaiwa kutekeleza unyanyasaji wa kibinadamu , ikiwemo kuwakamata watu kiholela mateso na mauaji wakati wa operesheni za kukabiliana na wapiganaji hao
Me nimeona video waliojirekodi Wanatanka Allah Akbar and then wanachinja na wanasema muili iachwe watu waone...

Nimegundua utetezi mwingi wa haya mauaji yanafurahiwa na wenye imani kali. . Na mtu yeyote anayefurahia anakuwa na ushetani ndani yake hivyo huyo ni adui yako na sio wa kumchekea kabisa ni kijutenga nae ataweza kukudhuru... Hata Marcon alishangazwa na Erdogan kumshambulia japo Marcon alisema ya moyoni mwake. .. we Ami kuna Muslim anayeweza kuchinja au kuua bila kutaka jina la Allah Akbar? Tuache unafiki kuna kitu hakipo sawa na kinatakiwa tiba. . Na kama hamna ni bora kunyamaza washughulikiwe hao
 
Lailah ila Issa

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
977
1,000
Vip waroma nao na genge lao walifanya nn unajua kama toka Zaman Roman empire ndio bado inashikilia rikod ya kuuwa watu wengi mpaka Sasa wakifatiwa na Mongolia
sasa hii ina'justify nini?
kama waliua miaka 1000 iliyopita huko kwa malengo yao mimi yananihusu nini?
Basi tuanze kusema mpaka Alexander the great nayeye aliua watu wengi..so what?ilishatokea inadhuru nini maisha yetu ya kawaida?
(BTW hizo roman empire na Mangolian zilikuwa za kipagani na hawakuwa na guiding principles za ku'justify mauaji yao ndomana leo hakuna wafuasi wanaofanya mauaji kwa jina la Roma takatifu au mfalme wa Roma miaka hii.)

Hii reasoning ni kama mtu aseme kwasababu babu yake na jirani yangu alikuwa jambazi sugu..ngoja namimi nianze wizi??

So kwa kusisitiza ili uelewe
*Roman Empire iliua watu wengi lakini cha kushukuru haikuacha ideology/dini inayohalalisha mauaji ndomana mpaka leo haitudhuru
Lakini muhamad na genge lao walifanya mambo na kuyahalalisha kidini na kujiita wao ndo mfano wa kuigwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom