Tajiri wa ajabu aibuka huko Ruvuma, Bilionea Barnaba Nyoni, anafanya biashara ya Mahindi

Kumeibuka tajiri mmoja huko Ruvuma wilaya ya Mbinga ambae ananunua mazao ya wakulima hususani mahindi. Tajiri huyo alianza kwa kununua mahindi kwa bei sh. Elfu sitini (60000/-)kwa gunia na kuyauza kwa wafanyabiashara mbalimbali kwa bei ya sh. Elfu arobaini na tano (45000/-)kwa sasa ameongeza bei ya kununua mahindi hayo ambapo ananua gunia la kg 120 kwa bei ya sh. Elfu sabini na tano (75000/-)na kuyauza kwa bei ya sh. Elfu arobaini na tano (45000/-).

Tukio hilo linaloendelea katika kijiji cha mkako Mbinga huko ruvuma limesababisha wafanya biashara wengi na wakulima kujazana huko na kusababisha msongamano mkubwa wa malori na watu katika kijiji hicho.

Kinachoshangaza wengi ni jinsi mfanyabiashara huyo anavyopata faida, na amekuwa na hela nyingi ambazo hazina idadi. Nadhani kuna walioifika huko watalielezea vizuri hili jambo.
==========

MWANDISHI: Kwa majina wewe ni nani? Mzaliwa wa wapi? Biashara hii ulianza rasmi lini?

NYONI: Kwa majina naitwa Barnaba Nyoni mzaliwa wa kijiji cha Mkako, biashara hii nimeanza mwaka huu mwezi wa tatu mpaka sasa na bado naendelea, tuko watu watatu. Hatuna kampuni isipokuwa sisi ni wakulima, wajasiriamali wadogo wadogo tumeamua kuungana na kufanya biashara ya kununua mahindi kwa wakulima na kumuuzia mtu yeyote, hata ikifika serikali.

Tunanunua gunia 60,000 ambalo sipimi lakini ukihitaji kwa kilo nakuuzia 410 yakiwa juu ya bodi.

MWANDISHI: Kwanini haupimi? Watu wengi wamekuwa wakihusisha na imani potofu.

NYONI: Imani potofu ni za kwao, sipimi naangalia gunia lenye ujazo wa kilo 120, 130 kwa sababu nafahamu mahindi ya ukanda huu ni mazuri sana na ni mazito kwa hio gunia nikiliona lina uzito ninaohitaji mimi naingiza kwenye gari lakini wakati nakuuzia wewe, nakupimia uzito wa kilo mia kila gunia, nakuuzia kwa kilo Tshs 410 sawa na 41,000 kwa gunia.

MWANDISHI: Faida mnaipataje?

NYONI: Mimi sipati faida isipokuwa nimeona afadhali nisaidie wananchi wawe na mzunguko, wafanyabiashara wawe na hela. Ilifikia mahala, mkoa wa Ruvuma wote kulikuwa na wimbi kubwa, hata muuza nyanya hana biashara, muuza maji hana kitu lakini sasa hivi ukitaka maji unapata, ukitaka chakula unakula kwa mtindo wa aina yoyote.

MWANDISHI: Umegawa ajira kwa upande mwingine?

NYONI: Tuko watu watatu ambao tumeamua kusaidia kwa wanaruvuma, sasa hivi ukienda Sodemo hukuti magari, hukuti wafanyabiashara, NMC ndio kabisa. Gari zote ziko hapa, gari za Dangote zote kama unavyoziona, ziko hapa. Kwa siku hapa najaza semi 20 na zinaondoka.

MWANDISHI: Wote wanalipwa cash?

NYONI: Hakuna mtu anaedai madeni, ungeliwahi mapema ungeona, kwenye daftari kulikuwa na watu 304 wa kuwalipa na mpaka sasa wamebaki watu 13, wote wamelipwa hela zao Mtu wa kwanza kumlipa nilipenda sana angekuwa mtu wa serikali, nilimpata. Alilipwa pesa zake na baadae aliwapa imani wananchi wote na wameleta mahindi. Mahindi sasa hivi napokea kutokea Peramiho, Songea na Mbinga.

MWANDISHI: Unafanya biashara ambayo haileti faida, madhumuni yenu ni nini?

NYONI: Lengo kuu kusaidia kwa sababu mtu ukibaki na pesa ndani, unadhulumika unaibiwa. Kwa hiyo zile pesa sisi tumeona afadhali ziwasaidie wananchi, watu wapate ajira na kama unavyoona, mkoa wa Ruvuma husikii wizi, hakuna ujambazi. Sehemu nyingine hapa ilibidi na askari. Kwa tunashukuru kwa sababu serikali inatambua.

MWANDISHI: Mna utajiri wa bei gani?

NYONI: Hatuna utajiri wa kusema tuna utajiri, isipokuwa tuliyokuwa nayo sisi inatufanyia mzunguko ile ile, kwamba tunanunua mahindi, tunauza mahindi, wateja wanaleta hela, hakuna mtu anaelalamika. Askari wanajaribu kuja barabarani, wanaona hamna tatizo lolote.

NYONI: Sasa hivi tunajenga Godown, wafanyakazi wanaojenga wako 80 na wote wanalipwa. Tukishamaliza, tunahitaji tuanze kuleta mbolea kwa bei elekezi ya serikali sio mambo ya ujanja ujanja kwamba mbolea umeambiwa uuze 46,000 wewe unauza 56,000 kisa usafiri, hapana. Sisi hii kitu tunataka tuvunje kabisa kwa mkoa wa Ruvuma isiwepo.

MWANDISHI: Mnafanya shughuli gani nyingine?

NYONI: Hatuna shughuli nyingine zaidi ya kilimo, sisi ni wakulima. Tumeshadhulumika sana, baadae tukaona kazi gani? Tukaungana ili tuweze kununua mahindi na baadae tulete mbolea.

Ninauhakika huyu anapata faida: anacheza na uzito
Hapo watu wanatakiwa kuwa makini sana, kabla sijawazia hilo la ndumba labda tujiulize bei ya gunia moja la mahindi halali kwa soko ni shilingi ngapi? Na yeye anaongeza cha juu shilingi ngapi? Inawezekana katika hao wanaonunua mahindi kwa huyo tajiri ni sehemu ya mtandao wake, kwamba amewapanga hao watu baadhi wanunue kwake kwa wingi then wahifadhi hayo mahindi. Kadiri muda unavyokwenda huyo tajiri atazidi kuongeza dau la kununua hayo mahindi, sasa mahindi yatakapopotea kabisa ataongeza bei juu sana, halafu hao watu wake wanaonunua kwa sasa wata anza kuuza huo mzigo kwa bei ghali..watu watanunua tu kwa hiyo bei ghali wakijua watarudisha pesa wakija kuuza kwa tajiri huyo...tajiri bila hiana atasema anataka mzigo mkubwa anunue kwa pamoja! hapo ndio kilio maana akishamaliza kuuza stock yake hiyo na kurudisha pesa yake atapotea na hivyo kuwa achia kilio huko.

Hii mbinu tulitumia kipindi flani huko mikoa ya Pwani, watu walinyoroshwa kweri kweri...
Hakuna ndumba hapo, its numbers
 
Hao wanatafuta hela za mambo ya Giza Halafu wanazibadilisha kwa hasara kwenda kwenye hela halali ndio masharti Ya hela hizo, wakipokea milioni Mia sita Ya uchawi wanaisafisha Kwa kuibadilisha kupata milioni Mia nne Ya kawaida, jiongezeni watanzania, Hakuna mtu duniani anaeweza fanya biashara Ya hasara hayupo
Bado nakupinga
 
Jichanganye uone unavyofilisika Sasa,

Huo uchawi wa miaka mingi Sana kule Burundi, skuhizi umeingia mpk kigoma na Morogoro ndani ndani wajuba wanautumia sana kutoboa.

Anatajirika kwa kuiba nyota yako,
Bila shaka hata manunuzi yake anatumia Cash Tupu.

Hakuna Cha mpesa,bank Wala Airtel money.

Ukishalipa kwa cash kununua kwake, inakua ndo imetoka iyo.
Nyota huwa inaibiwaje mkuu?
 
Gunia anazonunua yeye hapimi kwa kilo maama yake gunia la debe saba litakua na kilo 140 akija kuliuza yeye kwa bei ya kilo 450 maana yake atakua kauza gunia kwa TSH 63,000 Maana yake anapata gross profit ya TSH 3,000 kwa kila gunia analouza ukitoa matumizi lets say elfu mbili kwa kila gunia atabaki na net profit ya 1,000 kwa kila gunia

Kama semi linabeba gunia 200 maana yake ana faida ya laki mbili kwenye kila semi analopakia na kasema anapakia mpaka gari 20 kwa siku maana yake
20*200000=4,000,000 net profit kila siku ya kazi

Sasa watu wanachoshangaa hapo ni nini.
Basi jamaa ni genius
 
Kumeibuka tajiri mmoja huko Ruvuma wilaya ya Mbinga ambae ananunua mazao ya wakulima hususani mahindi. Tajiri huyo alianza kwa kununua mahindi kwa bei sh. Elfu sitini (60000/-)kwa gunia na kuyauza kwa wafanyabiashara mbalimbali kwa bei ya sh. Elfu arobaini na tano (45000/-)kwa sasa ameongeza bei ya kununua mahindi hayo ambapo ananua gunia la kg 120 kwa bei ya sh. Elfu sabini na tano (75000/-)na kuyauza kwa bei ya sh. Elfu arobaini na tano (45000/-).

Tukio hilo linaloendelea katika kijiji cha mkako Mbinga huko ruvuma limesababisha wafanya biashara wengi na wakulima kujazana huko na kusababisha msongamano mkubwa wa malori na watu katika kijiji hicho.

Kinachoshangaza wengi ni jinsi mfanyabiashara huyo anavyopata faida, na amekuwa na hela nyingi ambazo hazina idadi. Nadhani kuna walioifika huko watalielezea vizuri hili jambo.
==========

MWANDISHI: Kwa majina wewe ni nani? Mzaliwa wa wapi? Biashara hii ulianza rasmi lini?

NYONI: Kwa majina naitwa Barnaba Nyoni mzaliwa wa kijiji cha Mkako, biashara hii nimeanza mwaka huu mwezi wa tatu mpaka sasa na bado naendelea, tuko watu watatu. Hatuna kampuni isipokuwa sisi ni wakulima, wajasiriamali wadogo wadogo tumeamua kuungana na kufanya biashara ya kununua mahindi kwa wakulima na kumuuzia mtu yeyote, hata ikifika serikali.

Tunanunua gunia 60,000 ambalo sipimi lakini ukihitaji kwa kilo nakuuzia 410 yakiwa juu ya bodi.

MWANDISHI: Kwanini haupimi? Watu wengi wamekuwa wakihusisha na imani potofu.

NYONI: Imani potofu ni za kwao, sipimi naangalia gunia lenye ujazo wa kilo 120, 130 kwa sababu nafahamu mahindi ya ukanda huu ni mazuri sana na ni mazito kwa hio gunia nikiliona lina uzito ninaohitaji mimi naingiza kwenye gari lakini wakati nakuuzia wewe, nakupimia uzito wa kilo mia kila gunia, nakuuzia kwa kilo Tshs 410 sawa na 41,000 kwa gunia.

MWANDISHI: Faida mnaipataje?

NYONI: Mimi sipati faida isipokuwa nimeona afadhali nisaidie wananchi wawe na mzunguko, wafanyabiashara wawe na hela. Ilifikia mahala, mkoa wa Ruvuma wote kulikuwa na wimbi kubwa, hata muuza nyanya hana biashara, muuza maji hana kitu lakini sasa hivi ukitaka maji unapata, ukitaka chakula unakula kwa mtindo wa aina yoyote.

MWANDISHI: Umegawa ajira kwa upande mwingine?

NYONI: Tuko watu watatu ambao tumeamua kusaidia kwa wanaruvuma, sasa hivi ukienda Sodemo hukuti magari, hukuti wafanyabiashara, NMC ndio kabisa. Gari zote ziko hapa, gari za Dangote zote kama unavyoziona, ziko hapa. Kwa siku hapa najaza semi 20 na zinaondoka.

MWANDISHI: Wote wanalipwa cash?

NYONI: Hakuna mtu anaedai madeni, ungeliwahi mapema ungeona, kwenye daftari kulikuwa na watu 304 wa kuwalipa na mpaka sasa wamebaki watu 13, wote wamelipwa hela zao Mtu wa kwanza kumlipa nilipenda sana angekuwa mtu wa serikali, nilimpata. Alilipwa pesa zake na baadae aliwapa imani wananchi wote na wameleta mahindi. Mahindi sasa hivi napokea kutokea Peramiho, Songea na Mbinga.

MWANDISHI: Unafanya biashara ambayo haileti faida, madhumuni yenu ni nini?

NYONI: Lengo kuu kusaidia kwa sababu mtu ukibaki na pesa ndani, unadhulumika unaibiwa. Kwa hiyo zile pesa sisi tumeona afadhali ziwasaidie wananchi, watu wapate ajira na kama unavyoona, mkoa wa Ruvuma husikii wizi, hakuna ujambazi. Sehemu nyingine hapa ilibidi na askari. Kwa tunashukuru kwa sababu serikali inatambua.

MWANDISHI: Mna utajiri wa bei gani?

NYONI: Hatuna utajiri wa kusema tuna utajiri, isipokuwa tuliyokuwa nayo sisi inatufanyia mzunguko ile ile, kwamba tunanunua mahindi, tunauza mahindi, wateja wanaleta hela, hakuna mtu anaelalamika. Askari wanajaribu kuja barabarani, wanaona hamna tatizo lolote.

NYONI: Sasa hivi tunajenga Godown, wafanyakazi wanaojenga wako 80 na wote wanalipwa. Tukishamaliza, tunahitaji tuanze kuleta mbolea kwa bei elekezi ya serikali sio mambo ya ujanja ujanja kwamba mbolea umeambiwa uuze 46,000 wewe unauza 56,000 kisa usafiri, hapana. Sisi hii kitu tunataka tuvunje kabisa kwa mkoa wa Ruvuma isiwepo.

MWANDISHI: Mnafanya shughuli gani nyingine?

NYONI: Hatuna shughuli nyingine zaidi ya kilimo, sisi ni wakulima. Tumeshadhulumika sana, baadae tukaona kazi gani? Tukaungana ili tuweze kununua mahindi na baadae tulete mbolea.

Huyu ana pesa zisizo halali anazihalalisha, mana sijui kama anatoa hizo pesa benki au nyumbani.
 
Muhujumu na mtakatishaji!

Rushwa ya uchaguzi!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
Usione mtu anatoa msaada ukafikiri ni bure tu. Yaani ununue guni akwa elefu 75 alafu uuze kwa elfu 40?! Labda kama ni utoaji wa msaada lakini si biashara ila inawekuwa ni kafara. Kama unavyoona mtu ananunua mbuzi anampeleka kwa Shehe anasomewa gua alafu anaachiwa bila kuchinjwa ila wajuba wapambane naye mbele mbele kama kitoweo
 
Katika hali isiyo tarajiwa mwanaume mmoja mkoani Ruvuma wilaya ya Mbinga Kijiji Cha mkako amekuwa akifanya Mambo ya kushangaza kwa muda wa siku ya sita leo

Mwanaume huyo amekuwa akinunua gunia la mahindi la sado 35 kwa tsh 75000 Kisha anawauzia raia kwa Tsh 40000 pia baada ya kununua pesa zanazobaki huwa anazigawa kwa watu waliopo eneo la tukio

Pia kaenda mbali kutangaza kuwa endapo una mahindi yako na upo sehemu yoyote ndani ya Tanzania ukiyasafirisha mpka gharani kwake gharama za usafiri anakurudishi na atanunua kwa 75000 na ukitaka kununua Tena atakuuzia 40000

Ambapo akina mama tu wanaomsafishia mahindi anawalipa tsh 120000 kwa siku na ikiwa jioni atabakiwa na kiasi chochote Cha pesa huwa anazigawa hata zikibaki milion 20

Alipoulizwa pesa anatoa wapi hakutoa ufafanuzi na alipoulizwa kwanini anafanya hivyo akajibu Niayake Ni kusaidia
 
Back
Top Bottom