Tajiri Sambodo Kuchimba Visima 1000 vya Maji Tanzania Mwaka 2011

Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
80
Yule Tajiri mwenye kujiamini ameahidi siku ya tarehe 31 Dce 2010 kuwa anatarajia kujichimba visima 1000 vya maji katika wilaya zote za Tanzania isipokuwa Dar es Salaam. Gharama ya kila kisima ni karibia mil 5 na ameitaka serikali isijihusishe kwa namna yoyote na wapi visima hivyo vichimbwe. Ameahidi kutumia utaratibu wake yeye mwenye kutafuta sehemu ya kuchimba kulingana na mahitaji watu na uwingi wao.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwataka mafisadi waliopora mali za wananchi wazirudishe na kuomba msamahama ili mwaka 2011 uwe wa amani kwao na waanze upya kuishi kwa amani. Source (gazeti la mwananchi la tarehe 01 Jan 2011)
 
Mungu ambariki mzee wa watu, kwa uamuzi huu atawasaidia sana wanawake wanaotaabika kupata maji. niliwahi kusoma mahali akigawa mali zake ili atakapokufa kusiwe na mtafaruku wa kuzigombea na aligawia charities misikiti etc. mzee huyu ni muwazi na mwema sana na namtakia kila la heri na maisha marefu. Mungu amzidishie amani
 
Sabodo ataka mafisadi warejeshe fedha Send to a friend Saturday, 01 January 2011 11:37 0diggsdigg

Festo Polea
MFANYABIASHARA maarufu wa jijini Dar es Salaam, Mustafa Sabodo, amesema kama viongozi wanaotuhumiwa kuhusika katika ufisadi wa namna yoyote nchini wanataka kusamehewa na Mungu na wananchi katika mwaka huu, lazima watoe fedha walizoibia nchi ili zielekezwe katika kusaidia wananchi.

Sabodo alitoa kauli hiyo jana ofisini kwake jijini Dar es salaam, wakati akitangaza kuchimba visima 1,000 katika wilaya zote nchini, isipokuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.


Katika hotuba yake, Sabodo aliitaka serikali isiingilie matumizi visima hivyo vyenye lengo la kuwasaidia wananchi kupata huduma za maji bila masharti.


Alisema ni jambo la ajabu kwa viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kuendelea kuhodhi fedha nyingi na kushindwa kuisaidia jamii inayowazunguka.

"Mimi ni tajiri na nina fedha nyingi kwa sasa na si fisadi, lakini nasaidia wananchi wa aina yote kwa kuwa naipenda Tanzania na watu wake. Kwa upande wao, mafisadi wanakumbatia fedha nyingi za kuiba lakini wagumu kuzitoa, halafu wanataka kusamehewa, hawatasamehewa kamwe," alisema Sabodo.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni muumini wa falsafa za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere, alisisitiza kuwa mwaka huu ni mwaka wa viongozi mafisadi kujisafisha kama wanahitaji kweli wanataka msamaha wa Mwenyezi Mungu na wananchi wa Tanzania.

"Mafisadi katika nchi hii ni kero, wana fedha nyingi, wameiba fedha na kuzificha halafu wanataka Mungu na Watanzania wawasamehe, hakika wakitaka kusamehewa watoe fedha walizoiba," alisisitiza
Kuhusu visima 1,000 atakavyovijenga katika wila zote nchini, Sabodo alisema kila kisima kitagharimu zaidi ya Sh5 milioni na ujenzi wake utakamilika Julai mwaka huu.

"Visima hivyo ninavyosaidia katika wilaya hizo sitapenda serikali iingilie kwa chochote kwa kuwa matengenezo madogo madogo yatafanywa na wananchi wenyewe. Hakuna yeyote atakayelipia katika kutumia visima hivyo," alisema.
 
Nsololi,
Huyu mzee anaitwa SABODO na sio Sambodo kama uzi wako unavyosomeka.
Edit tafadhali
 
Only Mhindi pekee anaye kuwa na uchungu na nchi yetu is SABODO, shivji pia, wengine wote Fisadi characters dominate them,
Mungu akubariki.
 
Komboa Watanzania kama unauwezo maana viongozi wakiingia wanatusahau kabisa
 
Anataka kugombea urais nini?

People are very funy, sadaka itangazwayo hupoteza maana
 
kama siyo fisadi anafanya biashara gani?hivi kweli inawezekana nchi hii mtu asiwe na biashara isiyojulikana na asiwe fisadi?Bakhresa,mo enterprise,munif wa oilcom nk ni matajiri na biashara zao zajulikana.nijuzeni biashara ya sabodo
 
kama siyo fisadi anafanya biashara gani?hivi kweli inawezekana nchi hii mtu asiwe na biashara isiyojulikana na asiwe fisadi?Bakhresa,mo enterprise,munif wa oilcom nk ni matajiri na biashara zao zajulikana.nijuzeni biashara ya sabodo
 
Back
Top Bottom