Tuachane na Forbes, nani tajiri namba 1 Tanzania?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,602
Hebu wakuu niambieni nani ndo bilionea (mtu binafsi ama taasisi binafsi) wetu number one Tanzania?

Wale wazungu wasitupangie nani tajiri namba moja nchini kwetu.

Hebu wenyewe tujadili kati ya hawa nani namba moja?

1. Yogesh Manek
2. Mustapha Sabodo
3. Reginald Mengi
4. Salim Bakhressa
5. Mohammed Dewiji
6. Yusuph Manji
7. Ali Mafuruki
8. Rostam Aziz
9. Jeetu Patel
10. Fidal Hussen
11. Davies Mosha
12. Oilcom
 
Davis Mosha ni billionaire namba moja bongo mbantu . Asset yake moja tu -ile Lamborghini - kwa maneno yake mwenyewe ni Tshs 1bn. acha zile garina zenye personalized IDs sijui davina?1-5
 
wakuu maana ya 'Billionaire' mnaijua lakini??au mnamaanisha Billionaire in Tsh!,,Billionaire ni mtu yeyote mwenye net worth ya at least a Billion 'Dollars',,walio na na mabilioni ya kitanzania hao sio mabilionaire, ni millionaires!! tuangalie kwenye Majarida ya kichumi kwa info zaidi,,
 
Rostam Aziz alisema kupitia gazeti wakati wa kashfa ya kuilipa Dowans,kampuni zake ninaingiza zaidi ya dola 140 kwa miezi minne.

Kama ni ubillionaire wa mali na roho ni mzee Mengi
 
Davis Mosha ni billionaire namba moja bongo mbantu . Asset yake moja tu -ile Lamborghini - kwa maneno yake mwenyewe ni Tshs 1bn. acha zile garina zenye personalized IDs sijui davina?1-5

umesoma wapi mkuu? lamborgin ni asset? au ushabiki tu, je unajua asset ni kitu gani? embu soma vitabu kama RICH DAD POOR DAD uongeze weledi mkuu, au wewe ni msanii wa bongo fleva ambaye vipodozi,gari na kiatu ndo asset kwako! ukishajua wat is an asset ndo urudi jamvini maana utajua je huyu jamaa yako ni tajiri au lah! SOMA acha kucheza cheza na shule, nyie ndo mnatuangusha kwenye hii nchi
 
Tajiri halisi ambaye hata mwenyezi Mungu anamkubali ni yule anayelipa kodi ya serikali kihalali, anawalipa wafanyakazi wake kihalali, anatoa dhaka kihalali na anasaidia masikini na wajane ipasavyo. Katika hao mliowataja wametimiza haya? Kinyume na hapo ni wachumia tumbo binafsi na mali zako zitawaacha kabla hawajaziacha.
 
umesoma wapi mkuu? lamborgin ni asset? au ushabiki tu, je unajua asset ni kitu gani? embu soma vitabu kama RICH DAD POOR DAD uongeze weledi mkuu, au wewe ni msanii wa bongo fleva ambaye vipodozi,gari na kiatu ndo asset kwako! ukishajua wat is an asset ndo urudi jamvini maana utajua je huyu jamaa yako ni tajiri au lah! SOMA acha kucheza cheza na shule, nyie ndo mnatuangusha kwenye hii nchi
nimeishia la saba tu mkuu. hebu nipe shule kidogo maana ya asset. naamini nyie cashier wa benki mnayajua sana haya mambo
 
We kweli huna info. Hiyo gari kwa taarifa yako aliuziwa na mtoto wa bahresa- yusuph!

Davis Mosha ni billionaire namba moja bongo mbantu . Asset yake moja tu -ile Lamborghini - kwa maneno yake mwenyewe ni Tshs 1bn. acha zile garina zenye personalized IDs sijui davina?1-5
 
Kama utajiri unapimwa kwa fixed assets. bussiness empire na banking transactions. then tajiri No.1 Tanzania ni mhindi mmoja wa Mtwara anayekwenda kwa jina la Yogesh Manek naomba nisiziseme assets zake humu.

Kama utajiri unapimwa kwa kuwa Philantropists, then Tajiri No. 1 ni Mhindi mwingine kwa jina la Mustapha Sabodo akifuatiwa na Mzee wetu Reginald Mengi.

Kama utajiri unapimwa kwa Chain of Industries, then tajiri mkubwa Tanzania ni Mhindi mmoja mwenye Sumaria Group of companies akifuatiwa na S.S. Bahressa.

Kama utajiri utapimwa kwa fleet ya expensive cars, then tajiri mkubwa Tanzania ni mhindi mmoja kwa jina la Fidda Hussein.

Kama utajiri unapimwa kwa fleet ya real estates hapa mjini, then Mwenye ABLA Appartments etc.

Ukiondoa hawa matajiri wa mali, pia Tanzania tunao matajiri kibao wa mafanikio na fani mfano

Reginald Mengi ndie tajiri mkuu wa media akifuatiwa Akimiliki IPP Media na Media Solutions akifuatiwa na Rostam Aziz akimilika African Media Group na New Habari ambayo pia amelinunua Jambo Leo!.

Tukija matajiri wa fani kuna Nimrod Mkono anaerun most successiful law firm.

Utajiri wa kumiliki yard ya makonteiner unashikiliwa na Dioniz Malinzi wa campuni ya Cargostars.

Utajiri wa vituo vya mafuta unashikiliwa na Oil Com.

Utajiri wa real estate investments unashikiliwa na Yusuph Manji.

Tuna matajiri wengi sana wa Tanzania katika kila fani mfano JF ndio mtandao tajiri kabisa Tanzania unaoongoza kwa wanachama!.

Kwenye fani ya utangazaji kuna kijikampuni fulani cha matangazo kinaitwa PPR, huwa kina rusha vipindi vyake kwenye TV zote na redio zote wakati wa maonyesho mbalimbali hivyo kinahodhi utajiri mkubwa wa watazamaji na sio utajiri wa pesa.

NB. Data hizi ni kutumia visibility tuu na sio quontified!. Hii inamaana kuna matajiri kibao wenye utajiri wa kutisha ambao sio visible openly wamejikalia kimya kwa ku lay low profile na kuishi down to earth lives ila bank statements zao ndizo usipime!.

Nashauri tuanzishe kiji forbes magazine chetu.

Pasco.
 
Forbes 2012, wamemtangaza Bw, Mafuruki kama nyota inayochipukia Tanzania.
Mmiliki wa maduka ya Woolworth hapa Tanzania na Uganda, akiwa na gawio la asilimia 45% woolworth Africa. Muaanzilishi na mmiliki wa infotech, na sasa mmiliki wa digital satelite tv (ZUKU).

Source: www.forbes.com
 
Rostam Aziz alisema kupitia gazeti wakati wa kashfa ya kuilipa Dowans,kampuni zake ninaingiza zaidi ya dola 140 kwa miezi minne.

Kama ni ubillionaire wa mali na roho ni mzee Mengi

Mwili na roho?
Sina uhakika kama kuwapa walemavu kula ya siku moja na kisha kuwarusha kwenye televisheni kwa muda wa lisaa lizima wakifakamia msosi na kucheza muziki ndio utajiri wa roho ulioumaanisha...
 
Back
Top Bottom