Tajiri kuingia ufalme wa mbinguni ni ngamia katika tundu la sindano, vipi wanasiasa, tembo katika tundu la sindano?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,772
Kwanza naomba niwaombe moderators msipeleke huu uzi jukwaa la dini, kwa sababu lengo hasa ni kujadili maadili ya wanasiasa wetu Tanzania katika kuvumiliana na kudumisha maadili yao ya kidini.

Nimetafakari sana juu ya usemi kwamba kwa tajiri kuingia ufalme wa mbinguni ni sawa na ngamia kujaribu kupita tundu la sindano. Hata nikajiuliza, ikiwa ni ngumu hivyo kwa matajiri, vipi wanasiasa?

Tatizo la tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu bila shaka linatokana na tamaa ya kupata faida kwa dhuluma au ufisadi. Lakini si matajiri wote wako hivyo, na hata historia inaonyesha kuna matajiri wengi walikuwa katika mstari wa kupata ufalme wa Mungu.

Vipi wanasiasa? Hebu tuchukue hapa kwetu Tanzania. Mara nyingi sana nimeshuhudia, wanasiasa wa dini moja, huenda hata wanakwenda kanisa au msikiti mmoja, lakini katika mambo ya siasa wanakuwa ni maadui wakubwa! Mifano iko tele ya jinsi wanasiasa wetu wa dini moja, au kanisa moja, au msikiti mmoja, wakichukiana kwa kiwango cha juu kwa kuwa wako katika vyama mbalimbali. Hata imetokea kwamba wanasiasa wetu kwa tofauti za itikadi zao za kisiasa, wanaona ni kosa kutembeleana hospitali au misibani, japo wanaweza kuwa wa dini moja!

Na vipi basi kuhusu kusema uongo? Je inawezekana ukawa mwanasiasa na ukawa mkweli mbele za Mungu siku zote? Je kuwa mwanasiasa kunatoa nafasi ya kuwa mkweli kulingana na misaafu inavyotaka? Vipi ahadi kwa wananchi? Vipi kuambiwa kusema uongo ili kuepusha wananchi wasije juu dhidi ya chama au serikali?

Na vipi kuhusu kupanga mbinu za kukandamiza wanasiasa wengine, au vikundi vya kijamii, au taasisi, au kuwanyanyasa, mara nyingine hata kuamrisha wengine wafungwe jela au kupigwa pasipo makosa kwa kuwa tu mna uwezo wa kuwafanyia hivyo japo mnajua hamwatendei haki? Vipi yale tunayowatendea wapinzani wetu katika chama kimoja au cha upinzani pale tunapogombea nafasi za kisiasa kama ubunge au hata uraisi? Vipi suala la kulipiza kisasi, au hata tu kuwa na moyo wa kutaka sana nafasi itokee ili kulipiza kisasi!

Vipi suala la wizi, uwe wa fedha au wa kura, ili mwanasiasa mwingine, japo mko dini moja, asifanikiwe? Vipi udanganyifu kwa wananchi kuhusu matumizi ya fedha za serikali, hata kama ni kweli yalifanyika kwa faida unazodhani ni za serikali?

Kwa hiyo basi nimejiuliza, kwa namna siasa za nchi yetu zinavyokwenda, kwa kiasi kikubwa kukosa kuvumiliana, wanasiasa wetu wana nafasi rahisi zaidi kuigia ufalme wa Mungu kuliko matajiri, au ni tembo kupita tundu la sindano?

Kwa wanasiasa wote watakaosoma huu uzi, ningeomba mjitafakari sana, kuwa kwenu wanasiasa kunawaweka wapi katika suala na Ufalme wa Mungu, kulingana na mnavyowatendea wanasiasa na watu wengine, mara nyingine hata wale mlio dini moja, kanisa moja au msikiti mmoja! Kumbukeni huwezi kuwa na kipindi cha kuwa mtu wa siasa, na mtu wa dini, na ukadhani hilo ni sawa mbele za Mungu. Uko upande mmoja au mwingine.
 
Nikimkuta jiwe mbinguni nazama zangu chimbo kwa shetani Kula bange milele
Hewaaa. Kama mbinguni ni kwa wanasiasa, then sidhani kuna mtu atataka kwenda huko. Nilisikia kuna mmoja anataka kwenda kuwa raisi wa malaika huko.
 
Siasa kama tunavyozijua leo sio mpango wa Mungu kabisa.Nadiriki kusema ni mpango uliobuniwa kuzimu kama ilivyo dhana yeyote ya kushindana.Shetani ndiye muasisi wa ushindani alipotaka yeye aabudiwe badala ya Mungu na hatimaye akafukuzwa mbinguni.

What does this imply?It implies that anybody in politics is saving Satan's plan,kwa hiyo atafanya makandokando yote yanayoendana na ushetani kama tunavyoona katika tawala nyingi za dunia leo,so there is no chance for him to inherit the kingdom of God unless he/she repents.Mkuu this is sad,but true.

Mpango wa Mungu ni taifa kutawaliwa na Mungu mwenyewe.Soma 1Samuel 8:1-20 uone Mungu alivyowaambia wana wa Israel walipo kataa utawala wa Mungu kupitia kwa Waamuzi na kutaka Samueli awawekee mfalme.Yaliyowatakea ndicho kinachotutokea leo.
 
Do Mkuu umetisha! Hao kuna watu watakimb!a siasa kama wana masikio! Tatizo wengi huwa hawafikirii nvali juu ya vitu kama hivi, wanachoona ni mpinzani tu, atukanwe, apigwe, afungwe au hata auawe!
 
Huu ndio ukweli mkuu,hata kama hatuupendi.Politics is nothing but Satan's plan to cause havoc among peoples of the world whenever he wishes.
 
Kwanza naomba niwaombe moderators msipeleke huu uzi jukwaa la dini, kwa sababu lengo hasa ni kujadili maadili ya wanasiasa wetu Tanzania katika kuvumiliana na kudumisha maadili yao ya kidini.

Nimetafakari sana juu ya usemi kwamba kwa tajiri kuingia ufalme wa mbinguni ni sawa na ngamia kujaribu kupita tundu la sindano. Hata nikajiuliza, ikiwa ni ngumu hivyo kwa matajiri, vipi wanasiasa?

Tatizo la tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu bila shaka linatokana na tamaa ya kupata faida kwa dhuluma au ufisadi. Lakini si matajiri wote wako hivyo, na hata historia inaonyesha kuna matajiri wengi walikuwa katika mstari wa kupata ufalme wa Mungu.

Vipi wanasiasa? Hebu tuchukue hapa kwetu Tanzania. Mara nyingi sana nimeshuhudia, wanasiasa wa dini moja, huenda hata wanakwenda kanisa au msikiti mmoja, lakini katika mambo ya siasa wanakuwa ni maadui wakubwa! Mifano iko tele ya jinsi wanasiasa wetu wa dini moja, au kanisa moja, au msikiti mmoja, wakichukiana kwa kiwango cha juu kwa kuwa wako katika vyama mbalimbali. Hata imetokea kwamba wanasiasa wetu kwa tofauti za itikadi zao za kisiasa, wanaona ni kosa kutembeleana hospitali au misibani, japo wanaweza kuwa wa dini moja!

Na vipi basi kuhusu kusema uongo? Je inawezekana ukawa mwanasiasa na ukawa mkweli mbele za Mungu siku zote? Je kuwa mwanasiasa kunatoa nafasi ya kuwa mkweli kulingana na misaafu inavyotaka? Vipi ahadi kwa wananchi? Vipi kuambiwa kusema uongo ili kuepusha wananchi wasije juu dhidi ya chama au serikali?

Na vipi kuhusu kupanga mbinu za kukandamiza wanasiasa wengine, au vikundi vya kijamii, au taasisi, au kuwanyanyasa, mara nyingine hata kuamrisha wengine wafungwe jela au kupigwa pasipo makosa kwa kuwa tu mna uwezo wa kuwafanyia hivyo japo mnajua hamwatendei haki? Vipi yale tunayowatendea wapinzani wetu katika chama kimoja au cha upinzani pale tunapogombea nafasi za kisiasa kama ubunge au hata uraisi? Vipi suala la kulipiza kisasi, au hata tu kuwa na moyo wa kutaka sana nafasi itokee ili kulipiza kisasi!

Vipi suala la wizi, uwe wa fedha au wa kura, ili mwanasiasa mwingine, japo mko dini moja, asifanikiwe? Vipi udanganyifu kwa wananchi kuhusu matumizi ya fedha za serikali, hata kama ni kweli yalifanyika kwa faida unazodhani ni za serikali?

Kwa hiyo basi nimejiuliza, kwa namna siasa za nchi yetu zinavyokwenda, kwa kiasi kikubwa kukosa kuvumiliana, wanasiasa wetu wana nafasi rahisi zaidi kuigia ufalme wa Mungu kuliko matajiri, au ni tembo kupita tundu la sindano?

Kwa wanasiasa wote watakaosoma huu uzi, ningeomba mjitafakari sana, kuwa kwenu wanasiasa kunawaweka wapi katika suala na Ufalme wa Mungu, kulingana na mnavyowatendea wanasiasa na watu wengine, mara nyingine hata wale mlio dini moja, kanisa moja au msikiti mmoja! Kumbukeni huwezi kuwa na kipindi cha kuwa mtu wa siasa, na mtu wa dini, na ukadhani hilo ni sawa mbele za Mungu. Uko upande mmoja au mwingine.
Hiyo misemo ipo ili kuwafanya muachane na jitihada za kutafuta utajiri ili mtawalike vizuri kuanzia kichwani mpaka miguuni
 
Just a little education.... Ngamia inayoongelewa katika msemo huo si ngamia mnyama! naona mleta uzi amelinganisha na tembo. Be smart.. tafuta Kamusi ya kiswahili ikusaidie kujua maana nyingine ya neno "Ngamia". You will probably be shocked by the level of ignorance....
 
Neno ngamia lililotumika hapo si mnyama ni Kamba ya kufungia jahazi au boti pindi inapotia nanga ufukweni
 
Wewe jamaa una akili za yule ndege tunaekula na chips....kwa hiyo hilo "fundo" unalosema ndio lingetafsiriwa "camel" kwenye lugha ya kiingereza? Kwa maneno yako, neno "camel" katika tafsiri za kiingereza za Biblia lina maana fundo la uzi, kama vile tu ngamia? Kama neno ngamia katika tafsiri ya kiswahili lingemaanisha fundo la uzi, basi tafsiri ya kiingereza isingetumia neno camel, kwa sababu katika tafsiri huwa hatutafanyi direct translations; kwa mfano ndege turkey huwezi kumtafsiri "ndege wa uturuki" kwa kiswahili, bali bata mzinga. Nyie ndio mnaotafsiri majina kama Livingstone kuwa Jiwelinaloishi

You are probably shocked now by the level of your own ignorance

Mark 10:25 easier for a camel to go through a needle’s eye: Jesus is using hyperbole to illustrate a point. Just as a literal camel cannot go through the eye of an actual sewing needle, it is impossible for a rich man to enter the Kingdom of God if he continues to put his riches ahead of his relationship with Jehovah. Jesus did not mean that no wealthy person would inherit the Kingdom, for he went on to say: “All things are possible with God.”—Mr 10:27

https://www.jw.org/en/publications/bible/study-bible/books/mark/10/#v41010025

What did Jesus mean when He said it is easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich man to get into heaven?
Question: "What did Jesus mean when He said it is easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich man to get into heaven?"

Answer:
There are several different schools of thought on what Jesus was referring to in saying it was easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich man to gain eternal life (Matthew 19:24; Mark 10:25; Luke 18:25). The Persians expressed the concept of the impossible by saying it would be easier to put an elephant through the eye of a needle. The camel was a Jewish adaptation (the largest animal in Israel was a camel).

Some theorize that the needle Jesus was speaking of was the Needle Gate, supposedly a low and narrow after-hours entrance found in the wall surrounding Jerusalem. It was purposely small for security reasons, and a camel could only go through it by stripping off any saddles or packs and crawling through on its knees. The problem with this theory is there is no evidence such a gate ever existed. Beyond that, what sane camel driver would go through such contortions when larger gates were easily accessible?

Others claim that the word translated “camel” (Greek: kamelos) should actually be “cable” (Greek: kamilos). Then the verse would read that it is easier for a cable (or rope) to go through the eye of a needle. To believe this, however, brings up more problems than it solves, namely casting doubt on the inerrancy and inspiration of Scripture.

The most likely explanation is that Jesus was using hyperbole, a figure of speech that exaggerates for emphasis. Jesus used this technique at other times, referring to a “plank” in one’s eye (Matthew 7:3-5) and swallowing a camel (Matthew 23:24).

What did Jesus mean when He said it is easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich man to get into heaven?
 
Neno ngamia lililotumika hapo si mnyama ni Kamba ya kufungia jahazi au boti pindi inapotia nanga ufukweni
Nani amekuambia?

Kwa kifupi ni kwamba, neno la Kiebrania lililotumika hapa katika hii sentensi aliyoisema Yesu lilikuwa "kamelos", na lina maanisha ngamia mnyama. Sasa watu wakaja na theory zao kwamba hapana, Yesu hapa alikuwa ametamka neno "kamilos" ambalo ndio linamaanisha kamba.

Sasa suala ni kwamba, ikiwa tunaamini Biblia iliandikwa kwa roho ya Mungu, ina maana waandishi watatu wa hii sentensi aliyotoa Yesu, Mathayo, Marko na Luka, wote walikosea kwa kutumia neno ngamia badala ya kamba? Je turekebishe mistari hii ya Biblia iliyoandikwa na watu walioongozwa na Mungu kwa kuwa watu fulani ambao kwa maoni yao tu walipendekeza kwamba Mathayo, Marko na Luka hawakuwa na nia ya kuandika "kamelos" kama ngamia bali "kamilos" kama kamba?

Sasa be, amua mwenyewe sambi sako mie simo!
 
Tatizo matajiri ile kutoa moja kumi ya kila mwezi nishughuli aiseee.

Kuna watu moja yakumi ni milion 100 , sasa hapo inakuaje ??
 
Back
Top Bottom