Taji Liundi: Mama alitunywesha sumu, tuligundua neno Bongo Fleva

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Kwa mara ya kwanza mtangazaji nguli nchini Taji Liundi amefunguka kuhusu maisha yake binafsi na mchango wake katika tasnia ya muziki. Taji Liundi aka Master T ambaye amefanya kazi na vituo mbalimbali vya redio ikiwemo Redio one na Times fm toka miaka ya 1980 amefunguka mengi wakati akihojiwa na kipindi cha Salama Na cha Salama Jabir.

Taji Liundi amesimulia kisa cha kusisimua na kusikitisha ambapo mama yake mzazi aliamua kuwanywesha sumu yeye na wadogo zake watatu tukio lililopelekea wadogo zake watatu kufariki dunia huku yeye (taji) akiponea chupu chupu.

Tukio Hilo lilitokana na mgogoro wa ndoa baina ya mama yao na baba yao kutokana na kukosekana kwa uaminifu hasa upande wa mzee wake, baada ya mama Taji maarufu sana nchini Agnes Doris Liundi kugundua hilo aliazimia kujiua yeye na wanaye na ndiyo kisa cha kuwanywesha sumu wanaye.

Mama Taji alihukumiwa kunyongwa mpaka kufa na Mahakama kabla ya kupewa msamaha wa Rais na Hayati Baba wa Taifa J K Nyerere.

Baba yake Taji Liundi alikuwa mwanasheria, Jaji wa Mahakama Kuu na hatimaye msajili wa vyama vya siasa mwaka 1992.

Pia Taji Liundi ameeleza alivyoanza kutangaza Redio One, kipindi chake alichokianzisha cha DJ Show na kuwa mtangazaji wa kwanza kucheza Bongo Fleva kwenye redio, kabla ya kuwaachia mikoba akina Mike Mhagama baada ya kuikacha Redio one

Msikilize zaidi

Pia pitia uzi wa Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea?
 
Pole sana Master T.uwa namkubali Master T yupo makini sana huyu mtu.
Jamaa yupo humble sana.

.............ukisikiliza story hiyo, alipoponea aisee jamaa ana Mungu sana.

Anasema yy alikuwa anapenda sana mpira, so mama yao alipokuwa anawapa kile kinywaji alichochanganya na sumu yy alikuwa anakunywa then anaenda nje anatema lengo lilikuwa aonekane amemaliza haraka kile kinywaji ili awahi mtaani kucheza mpira...hapo ndipo alipoponea coz kutema kinywaji ili awahi kucheza mpira kulisababisha kunywa kiasi kidogo cha sumu tofauti na wengine ambao walifariki.

RIP ndugu zake wote Taji waliopotea katika hali ile.
 
Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia maisha marefu. Natamani kufahamu iwapo huyo mama yake bado yupo hai au la!!
 
Acha ubishi kati mtu wa Chato
Pitia huu uzi wa kitambo wakati JF iko na hadhi kama JF. Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea?
Duuh unabishana na muhusika mkuu aliyekuwepo kwenye tukio!!??
Nadhani hamjamuelewa huyo mnayesema ni mbishi! Jamaa hajabisha kuhusu simulizi ya Taji Liundi inayosema chanzo cha mgogoro ni baba kutokuwa mwaminifu bali anabisha simulizi ya Mtambuzi inayosema chanzo cha mgogoro ni mama kutokuwa mwaminifu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom