Taji Liundi: Mama alitunywesha sumu, tuligundua neno Bongo Fleva

Mimi JF nilijiunga sawa na Nyani Ngabu, William Malecela na wengine wengi. Sema ids zangu zote za enzi zile zilifutwa. Mimi ni kati ya member wa kwanza kabisa wa JF. Kabla ya hapo kilikuwa na discussion forum ya bcstimes.com enzi zile ambayo ni mama wa JF. Lkn mimi nilianzia billboard ya Tanzanet, enzi hizo unaipata kwa ftp wakati http bado changa.
 
Kwa mara ya kwanza mtangazaji nguli nchini Taji Liundi amefunguka kuhusu maisha yake binafsi na mchango wake katika tasnia ya muziki. Taji Liundi aka Master T ambaye amefanya kazi na vituo mbalimbali vya redio ikiwemo Redio one na Times fm toka miaka ya 1980 amefunguka mengi wakati akihojiwa na kipindi cha Salama Na cha Salama Jabir.

Taji Liundi amesimulia kisa cha kusisimua na kusikitisha ambapo mama yake mzazi aliamua kuwanywesha sumu yeye na wadogo zake watatu tukio lililopelekea wadogo zake watatu kufariki dunia huku yeye (taji) akiponea chupu chupu.

Tukio Hilo lilitokana na mgogoro wa ndoa baina ya mama yao na baba yao kutokana na kukosekana kwa uaminifu hasa upande wa mzee wake, baada ya mama Taji maarufu sana nchini Agnes Doris Liundi kugundua hilo aliazimia kujiua yeye na wanaye na ndiyo kisa cha kuwanywesha sumu wanaye.

Mama Taji alihukumiwa kunyongwa mpaka kufa na Mahakama kabla ya kupewa msamaha wa Rais na Hayati Baba wa Taifa J K Nyerere.

Baba yake Taji Liundi alikuwa mwanasheria, Jaji wa Mahakama Kuu na hatimaye msajili wa vyama vya siasa mwaka 1992.

Pia Taji Liundi ameeleza alivyoanza kutangaza Redio One, kipindi chake alichokianzisha cha DJ Show na kuwa mtangazaji wa kwanza kucheza Bongo Fleva kwenye redio, kabla ya kuwaachia mikoba akina Mike Mhagama baada ya kuikacha Redio one

Msikilize zaidi

Pia pitia uzi wa Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea?
Hivi kumbe Taji Liundi alikuwa mtoto wa msajili wa vyama Jaji George Liundi
 
Hiyo historia ya Mtambuzi siyo kweli. Mzee Liundi ndiyo alizaa na demu nje ya ndoa.
Ni kweli kuwa George Liundi alizaa nje ya ndoa. Ila kusema kuwa historia ya Mtambuzi si ya kweli itakuwa ni kutomtendea haki. Maana Mtambuzi amecopy na kupaste (kutafsiri) nyaraka za mahakama which is a very reliable source. Na ni Mama Liundi mwenyewe aliyesema mahakamani kuwa chanzo cha mgogoro wao ni Mzee Liundi kumtuhumu yeye kuwa si mwaminifu.

My take ni kuwa mambo yote haya yalitokea, mzee alizaa nje ya ndoa na pia alimtuhumu mke wake kutokuwa mwaminifu. Kuna kimoja kati ya hivi ndiyo kilianza ila si rahisi kwa sisi kujua kipi kilianza.
 
Ni kuwa Waswahili mnadai marehemu hasemwi vibaya ila kwa tunaoijua familia tokea enzi hizo kabla ya janga la sumu, Mr & Mrs Liundi wote walikuwa 'wajanja'(use your commonsense).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom