TAJENI majina JF

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,546
843
Of recent kumekuwepo na tabia ya kama waandishi wetu wa habari (Print & electronic media) ambao wanakuwa na big headlines halafu hawataki kumtaja mtu jina

The difference kati ya JF na wao ni kuwa sisi hatuogopi tunataja majina. Lakini nimegundua kuwa hivi karibuni 'the fear of unknown' imeingia sana humu JF

Sasa kama kuna mtu anayo majina ya watuhumiwa wa ufisadi..nitumieni kwenye PM mimi nitaweka kama vile nilivyoweka jina la MWIKALO na MEMBE humu

Tuache tabia za kuficha ficha majina bila sababu za msingi otherwise ile motto yetu kuwa WEHERE WE DARE TALK OPENLY itakuwa haina maana hata kidogo
 
GT, well said!!!!
Don't hold your breath kwani members ambao hawapendi watu watajwe majina watakuja kukupa mlolongo wa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu

Sababu ya kutosoma IPPMEDIA na websites za magazeti ya nyumbanini mimi sipendi half baked info...esp pale wanapo andika (Waziri huyo ambaye jina lake linahifadhiwa....)

What a load of crap?

Siku hizi JF nako utaona mtu anaanzisha thread kisha anaandika (Jina nimelihifadhi)

Sikiliza kama kweli unapiga vita ufisadi kwa nini usiwataje? Unless na wewe unapenda sana huo ufisadi!

Nakwambia sie tunapigana vita na hawa watu kila kona
 
Kwa kifupi kutoa habari ambazo ni negative bila kutaja majina ni unafiki pure and simple. Zikiwa habari nzuri za sifa basi majina tutatajiwa yote na ikibidi ya nyongeza!

Mfano, majizi yetu yanayorudisha pesa za EPA kinyemela eti majina kapuni, what is that? Humu JF inabidi tuipige vita tabia hiyo kwa nguvu zote, kama mtu ana data mwaga unaogopaogopa nini? Haya mambo ya majina kapuni hayasaidii chochote zaidi ya kuwawekea uzio mafisadi. Ndio yaleyale ya "mikingamo" kwa wanaokumbuka "kiongozi fulani yuko mahali fulani anafanya hujuma fulani" hapo baada ya kutangaza "tuambie nani yuko wapi na anafanya nini kuhujumu taifa" yaani unafiki mtupu!
 
Of course ukija JF na habari zako uwe na facts za kutosha walau kutoa tetesi, siyo kujitungia tu, oh sijui nimeota usiku, sijui nini, that won't fly.
 
Kama unaona huwezi kumtaja jina mtuhumiwa wa ufisadi usianzishe thread kabisa, subiri hadi utakapopata ujasiri ndio uweke.
 
Of course ukija JF na habari zako uwe na facts za kutosha walau kutoa tetesi, siyo kujitungia tu, oh sijui nimeota usiku, sijui nini, that won't fly.
Nadhani hii ya kwako mwnkjj, hasa kama mzee wa watu amejiotea kwani ni sehemu ipi ya katiba ya jf inayomzuia asiwashirikishe wana jf wenzie katika kutoa tafsiri ya ndoto zake.
 
sasa kama nimeota nisiseme nimeota nitunge uongo ili JF wafurahi? gademu! Ok sikuota basi nimeambiwa na Steven Peter toka Ikulu!
 
sasa kama nimeota nisiseme nimeota nitunge uongo ili JF wafurahi? gademu! Ok sikuota basi nimeambiwa na Steven Peter toka Ikulu!

Mzee Manakijiji,

Kama tuakianza kutaja kila kitu nadhani hata hao ambao huwa wanatupa habari hizi wataacha kuongea nasi,

Nadhani GT anasema kama habari inamhusu mtu flani basi mtaje mtu anahusika bila kumtaja aliyekupa habari,
 
Habari ikiwa si ya uhakika na ina lengo la kuchokoza ili mtu apate habari zaidi ndio haweki jina na hio naona iko poa tu.

Sasa kumtaja mtu jina kwa habari za kusikia ndio uungwana hivyo mkuu GT au huko kwenu ndio mnavyofanya?

Kuwa mkweli, na kuna habari ziko kwenye utafiti na kutaja majina kunaweza kupelekea mhusika kubadilisha taabia yake sasa tutaje majina ili habari ikosekane?

Kuwa muwazi na hayo madongo yako kwa wakuu wetu wenye kuota ndoto wakiwa hawajafumba macho
 
Nafikiri tukifanya hivyo JF haitakuwa tena Behind the news maker maana habari zote zinazoletwa bila majina baadae zindhitika kuwa kweli na tunatangulia kuliko vyombo vyote vya habari, unakuta habari ya magazeti ya leo sisi tulishaijadili tangia siku tatu mpaka wiki.
kinachotusaidia ni kulinda majina ya watu wakati tunaendelea kutafiti hiyo habari kwa undani zaidi. ukisema bila kukamilisha habari isiandikwe then tutafanana na watu wa vyombo vya habari vingine.
 
Mi nafikiri ushauri wa GT ni mzuri tu.Kwa sababu,kwa watu wanaoishi nje ya Tanzania ni rahisi kutoa majina kuliko wanaoishi hapa.Kama ilivyotokea kwa wenzetu humu kushikwa na polisi,lazima mtu atakuwa na uoga flani,therefore ni vizuri kama mtu una story kumtumia PM GT
 
Pia ni lazima kuangalia kwamba huvunji sheria au humuharibii mtu jina lake kwa habari za uongo au kutunga.

Sisi JF tusijione tunastahili mno kuliko kile tunachostahili vinginevyo tunaweza kujikuta tunatumika kuharibu kazi za watu, familia zao, n.k

Kwa habari zinazohusu shuku ya kweli basi hakuna sababu ya kuficha jina alimradi uandishi unaonesha ni shuku na si habari au factual.
 
To me ukisema kitu alafu ukasema the name is with held huwa napata picha ya udaku?
Na JF haitakiwi kuwa ivyo ni kuweka mambo hadharani tuu mpaka kieleweke
 
Heshima mbele Wakulu... Mimi kwenye hili concerns zangu ni hizi:
1. Kama una issue unatajka uilete jamvini, lazima iwe justified with facts, names (even titles) ili kuruhusu wanaBaraza kuijadili kwa kina na kuangalia kama inahusu maamuzi, itapelekea watu kuwa na uhakika kama maamuzi hayo ni ya juu au ni ya "Vidagaa"

2. Sio lazima (na wala hatutaki) kujua source yako... Kikubwa ni hicho hapo juu

3. Kwa mtazamo wangu, kuleta habari Barazani bila kuweka something for people to grip on and make sensible contribution ni kufanya wanaBaraza wawe wanaweka comments based on speculation nao wanakuwa nothing but "Speculators" na hii sio mbali sana kutokea kwenye "UDAKU" na inaweza kuwa easily translated as one!!!

Nadhani uelewa wangu ni sawa.... These are just my thoughts though...........

Haya, wanaBodi tuendelee na shughuli iliyo mbele yetu!!!
 
Nadhani hii ya kwako mwnkjj, hasa kama mzee wa watu amejiotea kwani ni sehemu ipi ya katiba ya jf inayomzuia asiwashirikishe wana jf wenzie katika kutoa tafsiri ya ndoto zake.
jamani inawezekana mzee mwanakiji ni mtaalamu wa kumeditate,akaaa kutokana na ukubwa wake basi mipicha inakuwa inajengeka kichwani mara la Hosea,mara Kikwete mara Jacky Chen..then anatumwagia hapa then kesho yake mambo yanatokea..hahaha
 
Si kitu kibaya kutaja majina lakini juzi kulikuwa na debate nzuri sana BBC kuhusu new media yaani webblog na responsibility. Unajua hivi sasa Jamboforums is part of Tanzanian media, whether we accept it or not. Kwa kuwa tunapata habari hapa so it is chombo cha habari. Sasa katika traditional media, kuna editor, kuna researcher na owner or publication is liable. In the case of the blog, mambo ni tofauti, and it is up to the reader to sort out facts from fiction and half baked truths. Pia ni rahisi kwa blog kutumika kama revenge machine ya mtu dhidi ya mwenzake. So we have to set rules and then adhere to them.
Nimeona kwamba kumekuwa na kajitendency hivi karibuni hapa JF watu kuandika udaku alafu kuingia mitini. Inabidi tuchunge sana dhidi ya umbea kama huu.
Overall nadhani with time we will manage to police ourselves na newcomers will get the hang of it. Otherwise nakubali kabisa kwamba majina yatajwe kama kuna uthibitisho wa facts, ili sote tufahamu nani anazungumziwa na siyo kukisiakisia.
 
Huwezi kuamini how long it took us wengine kujua kama CHENGE ndiye watu humu walikuwa wanasema eti(jina linahifadhiwa)what ever hapenned to JF kuset the agenda?

Badala magazeti kujadili reference zetu utashangaa tunajadili yaliyoandikwa na hayo magazeti ambayo yanakuja kucopy data humu

 
Back
Top Bottom