Na Emmanuel J. Shilatu
Tukiwa tunaelekea maadhimisho ya miaka mitatu tangu utawala wa Serikali ya awamu ya tano unaoongozwa na Rais John Pombe Magufuli uingie madarakani hauwezi kuacha kutaja suala la rushwa na ufisadi.
Vipindi vya awali suala la rushwa na ufisadi vilijaa wingu zito vikipambwa na misamiati mbalimbali ya sakata ya matukio yaliyoonyeshwa kukubuhu kwa himaya ya Mafisadi nchini pasipo hatua za kuridhisha kupambana nayo.
Ilifika wakati Watanzania wakawa wanamkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye katika kipindi chake wala rushwa na ufisadi walikuwa wakifungwa miaka 2 jela pamoja na kuchapwa viboko 24. Hii ilitia hofu na kupunguza matukio ya rushwa na ufisadi kipindi hicho.
Tukiwa tunaadhimisha miaka 3 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, Serikali yake imeitendea haki ibara ya 11, 12 na 13 iliyopo ukurasa wa 6 katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 - 2020 inayoelezea namna itakavyopigia vita dhidi ya rushwa nchini.
Leo hii tunaona mapambano ya dhati ya kutokomeza rushwa na ufisadi nchini tukishuhudia "Mapapa" ya rushwa na ufisadi wakipandishwa Mahakamani, kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi.
Hata upande wa Watumishi wa umma, suala la uadilifu na uwajibikaji limeimarika zaidi kutokana na kupungua kwa matukio ya rushwa na ufisadi miongoni mwao.
Hayo yamepelekea leo hii Tanzania kupanda kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na 2017 na pia ikishika nafasi ya pili (2) katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mapambano haya ya rushwa na ufisadi nchini yamepelekea zaidi ya Tsh. Bilioni 127 kuweza kuokolewa tangu Serikali ya awamu ya 5 iingie madarakani.
Katika hili, Watanzania tunasema *Ahsante sana Rais Magufuli*, Serikali unayoiongoza imetekeleza vyema Mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini.
*Shilatu E.J*