Taja instrument(s) au sehemu ya beat ya wimbo inayokuburudisha

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Oct 31, 2017
7,621
16,372
Katika muziki kuna miguso ya ajabu sana, yaani unaweza kusikiliza instrument(s) Fulani ukatekwa kabisa na kufanya uzidi kuupenda muziki husika. Hebu tutumie huu uzi kuzitaja hizo sehemu au instrument(s) katika nyimbo ambazo zinakonga nyoyo zetu.

Kwa kuanza mimi kuna hizi hapa
Zile strings zinazoambatana na kick pale mwazoni mwa wimbo wa ‘knock you down’ wa keri hilson ft. kanye west & Ne-Yo. Na pia huwa zinabamba sana pale kanye west anapoanza kuchana kabla beat halijachanganya. Huwa naburudika sana kwa kweli.

Kile kimluzi cha kwenyechou ya wiggle ya Jason derulo ft. snoop dog, yani nikisisikia najikuta nachezesha kichwa.

Ile sijui ni piano ama kitu gani inayosindikiza chorus ya kwenye wimbo wa swallah (samahani kama imekosea spelling) ya Jason derulo ft. nick minaj na Yule jamaa mwingine tola y nani sijui, jina lake linanishinda kuandika.

Trumpet iliyopo kweye chourus na baadhi ya sehemu kwenye verse ya wimbo wa kill yourself ya nikki mbishi ft. Godzilla & cliff mitindo. Producer sijui alitumia kilevi gani kutengeneza hiyo kitu, so amazing.

Ile violin ya kwenye wimbo wa kababaye wa chin bees halafu huwa kuna ka string flani kanapita kwa chini, dah ni noma sana.
Ile piano ya mwanzoni kwenye wimbo wa see you again ya wiz khalifa ft. Charlie puth, huna inagusa moyo sana.

Ile string iliyopo mwanzoni mwa mimbo wa sofia by ben pol.

Kuna ka instrument flani kana mlio kama wa kengele hivi kwenye chorus ya kadogo ya ali kiba.

Zipo nyingi, tuendelee kuzitaja.
 
Dr Dre ft Snoop dogg - Still Dre
Dr Dre ft Eminem - Foget about Dre
Reggae zote za Nesta Marley
Reggae za Peter Tosh
Nyimbo za Msondo Ngoma
Beats nyingi za Mandugu digital
Hao niliotaja hapo juu kwenye miziki yao kuna vionjo vya kipekee ambavyo huvikuti popote.

"Cᵒᵃᶜᵏʳᵒᵃᶜʰ ⁿᵘʰ ᵇᵘˢˢⁱⁿᵉˢˢ ⁱⁿⁿᵃ ᶠᵒʷˡ ᶠⁱᵍʰT"
 
Dr Dre ft Snoop dogg - Still Dre
Dr Dre ft Eminem - Foget about Dre
Reggae zote za Nesta Marley
Reggae za Peter Tosh
Nyimbo za Msondo Ngoma
Beats nyingi za Mandugu digital
Hao niliotaja hapo juu kwenye miziki yao kuna vionjo vya kipekee ambavyo huvikuti popote.

"Cᵒᵃᶜᵏʳᵒᵃᶜʰ ⁿᵘʰ ᵇᵘˢˢⁱⁿᵉˢˢ ⁱⁿⁿᵃ ᶠᵒʷˡ ᶠⁱᵍʰT"
Mandugu digital huwa ana touches flani tofauli sana...yule jamaa ana mziki wa aina ya peke yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom