Taja "character" uliyemchukia kupita kiasi katika filamu au tamthilia

George Betram

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
4,018
4,907
Nimepita twitter nimeona kuna mtu amemtaja Arturito wa kwenye TV Series ya Money Heist kama "character" ambaye amewahi kumchukia tangu aanze kuangalia "movies" na "tv series".

Inawezekana wapo wengine humu ambao wanamchukia Arturito, of course jamaa ni fala sana, yaani anakera kwelikweli.
Lakini mimi binafsi "character" ambaye nimewahi kumchukia kiasi kwamba nikawa najisahau kabisa kuwa jamaa alikuwa anaigiza tu ni hii mashine hapa chini:

Ramsay_S06E09_RESZIED_FOR_INFOBOX.jpg

Anaitwa Ramsay Bolton, anapatikana katika "TV Show" ya Game of Thrones, huyo mpuuzi alikuwa ni katili balaa.
Nilikuwa namchukia huyu boya kiasi kwamba nilikuwa natamani niwavutie waya watayarishaji wa Game of Thrones ili niwaulize huyo mpuuzi atakufa kwenye season ya ngapi na episode namba ngapi.

Mambo yasiwe mengi, taja "character" uliyewahi kumchukia mpaka ukajisahau kuwa yupo kwenye kazi yake, yaani anachokifanya ni maigizo tu na anaifanya vyema kazi yake.
 
  1. King Joefrey
  2. Ramsey Bolton
Hawa watu siwapendi wamenitendesha dhambi sana wakati naangalia GOT. Sitaki kuona hata muvi zao zingine..Walinikera sana aisee sijawahi kukerwa kama wao walivyonikera.

Utamu wa Ramsey anaujua Theon...itamu wa Joefrey anaujua Sansa.

Mwingine ni Brad Belick na Wyatt Mathewson hawa watu waliniuzi sana kwenye PB. Belick mbea hadi anakera..Wyatt alivyokua anawadungua akina maiko alikua ananidhi sana na limkono lake la shoto.
>>>>
My review of a song of Ice and Fire: Game of Thrones series - JamiiForums
 
Ahahaaaaah.
Bwana Da'Vinci, huyo Joffrey kwangu ni nambari mbili ndiyo maana sijamtaja.
Ila wamepishana kidogo sana na Ramsay, halafu mimi nahisi uigizaji wa Ramsay Bolton na huyo dogo Joffrey katika Game of Thrones kuna namna umeathiri "careers" zao za uigizaji, hao watu walichukiwa balaa.
 
Movie ya 1999.
Jina la movie Bridge of the dragon
Star - Dolph Lundgren akicheza kama warchild.
Valerie show akicheza kama princess halo
Gary Hudson akicheza kama emme rich

Sasa tabu kwa huyu mpuuzi cury hiroyuki tagawa akicheza kama General, aliniboa sana.
ef45e6896c5387283bf8815d5929fe0e.jpg
 
Movie ya 1999.
Jina la movie Bridge of the dragon
Star - Dolph Lundgren akicheza kama warchild.
Valerie show akicheza kama princess halo
Gary Hudson akicheza kama emme rich

Sasa tabu kwa huyu mpuuzi cury hiroyuki tagawa akicheza kama General, aliniboa sana. View attachment 1444424
Kwa huyo mjomba nakubaliana na wewe mzee. Kuna huyu na mjomba mmoja wa kuitwa Billy Drago, hawa wakicheza majambaka inakuwaga ni cheche mzee.
billy-drago-photo_102773_6213.jpg

BILLY DRAGO
 
Back
Top Bottom