Taifa Stars

Mujuni2

Senior Member
Jun 11, 2008
142
195
Wana JF
Wandugu, mi ni mfuatiliaji wa maswala ya michezo hasa soka.Ila sasa naona mambo ya soka, yameingiwa na siasa hivi magazeti kuandika 'Taifa Stars yafa kiume" maana yake nini? Kwa msiosoma habari hii ni juzi tuu timu yetu ya Taifa imefungwa 2-1 na Cameroon, sasa inaandikwa kuwa tumefungwa kiume.Nyie mliobobea kwenye maswala ya soka hebu niambieni kufungwa kiume na kike nini tofauti yake? ni kwa idadi ya magoli au?au ni mlolongo wa viini macho vya aserikali ya awamu ya nne?
Mujuni2
 

Jobo

JF-Expert Member
May 15, 2008
587
225
Wanachekesha! Wafa kiume wakati majirani zao wanashinda nyumbani na kutoka droo nje! Yaani Cape Verde inatufunga, tunatoka droo na timu dhaifu ya Madagascar na tunafungwa na Cameruni bado tunajiona wanaume!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom