Taifa Stars yabaniwa kufanya mazoezi ya mwisho taifa. Kocha Paulsen ang'aka

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,134
2,311
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen akizungumza kuelekea mchezo wa kufuzu CHAN dhidi ya Somalia utakaochezwa kesho Jumamosi Julai 23 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Polsen ameshangazwa na kitendo cha timu ya Taifa ambayo inajiandaa na mechi ya CHAN kunyimwa uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mazoezi angalau ya session moja.

“Maandalizi ni muhimu sana, inashangaza wakati tunajiandaa kuwakilisha nchi kwenye CHAN tunanyimwa nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye dimba la Mkapa, kama uwanja haupo kwenye hali nzuri sasa inakuwaje timu kutoka Ulaya wamepewa nafasi ya kufanya mazoezi hapo!?”

- Kim Poulsen, Kocha wa timu ya taifa

Stars wameambiwa haiwezekani kufanya mazoezi hapo lakini uwanja unatumika kwa ajili ya mechi za Vijana na wengine wanafanyia mpaka mazoezi
 
magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
6,609
10,453
Kwani mazoezi ya mwisho lazima iwe kwa Mkapa? Kocha anataka kufukia nini?
Tuna safari ndefu sana ya kuelewa. Huyu anaandika kwa kujiamini kabisa. Like serious hujui mazoezi ya mwisho yanatakiwa kufanyika kwenye uwanja gani? Na bado unakejeli!

Sasa naanza kuelewa vizuri vile vipaumbele vitatu vya Lowasa.
 
man dunga

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
2,260
3,749
Tuna safari ndefu sana ya kuelewa. Huyu anaandika kwa kujiamini kabisa. Like serious hujui mazoezi ya mwisho yanatakiwa kufanyika kwenye uwanja gani? Na bado unakejeli!

Sasa naanza kuelewa vizuri vile vipaumbele vitatu vya Lowasa.
Elewa neno 'lazima' wewe mbumbumbu. Kwamba wasipofanya mazoezi ya mwisho hapo kwa mkapa watapungukiwa nini kiufundi kama ambavyo wakienda kufanyia Azam Complex? Usikariri tumia akili yako kufikiri ewe mbumbumbu.
 
Mdukuzii

JF-Expert Member
Jun 27, 2022
2,565
6,163
Tuna safari ndefu sana ya kuelewa. Huyu anaandika kwa kujiamini kabisa. Like serious hujui mazoezi ya mwisho yanatakiwa kufanyika kwenye uwanja gani? Na bado unakejeli!

Sasa naanza kuelewa vizuri vile vipaumbele vitatu vya Lowasa.
Wao sio wageni,sheria hiyo inahusu wageni sio host,kitu gani hawakijui pale uwanjani su wanataka kuroga
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom