Taifa Stars waliwatoroka polisi Abidjan kimya kimya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa Stars waliwatoroka polisi Abidjan kimya kimya

Discussion in 'Sports' started by BAK, Feb 27, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,442
  Trophy Points: 280
  Date::2/26/2009
  Taifa Stars waliwatoroka polisi Abidjan kimya kimya
  Na Saleh Ally, Abidjan
  Mwananchi

  UAMUZI wa kikosi cha Taifa Stars kuamua kutokula chakula kwenye hoteli ya Golf ya mjini hapa ili kukwepa hujuma, kulizua tafrani kubwa baada ya askari Polisi aliyepewa dhamana ya kuwalinda kutaka kuwalazimisha kupanda kwenye basi kwa nguvu.

  Stars juzi iliibuka na ushindi wake wa kwanza wa mashindano ya CHAN kwa kuwachapa wenyeji Ivory Coast kwa bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Ngassa kwa kichwa cha kuchupa.

  Kamati maalum iliyo jijini hapa ilichukua uamuzi wa kuhakikisha Stars hawali chakula cha hotelini hapo na maandalizi yakafanyika kwenda kula mafichoni ili kuepuka hujuma hasa suala la kuwekewa 'vitu' mbalimbali kwenye chakula.

  Lakini ilibidi ifanyike kazi ya ziada kuwatoroka walinzi ambao wamekuwa wakitembea na timu hiyo tangu imewasili jijini hapa, wakiwamo askari Polisi wawili wa usalama barabarani wenye mbwembwe za kila namna.

  Wachezaji Stars walitoroka kimya kimya kutoka hoteli ya Golf ndani ya Taxi sita kwenda kula huko walikopangiwa, baada ya hapo walinzi hao walianza kuwasaka kila kona ya jiji na mwisho walifanikiwa kuwapata pale walipokuwa kitu ambacho kilimshangaza kila mmoja.

  'Kila mtu alishangaa jamaa wamepajua vipi, tulibaki tumepigwa na butwaa na mara moja wakaanza kutulazimisha kupanda kwenye gari, lile basi tunalotumia lakini viongozi pamoja na (Crescentius ) Magori na Teddy Mapunda wakazuia. Hatukupanda.

  'Walitaka kuanza kutumia nguvu na sisi tukagoma, ikawa mshike mshike, lakini mwisho jamaa wakakubali kufuatana na sisi. Tukaingia kwenye zile taxi na kuanza kurudi hotelini huku wakitusindikiza kwa ving'ora na basi likiwa tupu,' anaeleza mmoja wa wachezaji wa Stars.

  Lakini hali ya kuwalazimisha wachezaji kupanda kwenye basi hilo tayari ilionyesha kulikuwa na walakini na askari mmoja aliiambia Mwananchi kwamba ule ni utaratibu ingawa mmoja alikiri kwamba ilikuwa ni amri kutoka ngazi za juu zinazoshughulikia masuala ya usalama katika michuano ya CHAN ambao walitaka kuona lazima wachezaji wa Stars wapande basi hilo.

  Kumekuwa na hujuma katika mechi nyingi hasa katika nchi za Afrika kitu ambacho kimeifanya Stars kuongeza umakini hasa inapokua mbali na nyumbani.

  Hali hiyo pia ilijitokeza wakati wa mechi yake ya mwisho kufuzu katika michuano ya CHAN dhidi ya Sudan mjini Kharthoum ambako wenyeji walilala kwa mabao 2-1.

  Imeelezwa kumekua na tabia ya kupulizia dawa kwenye vyumba au kwenye chakula na wachezaji baada ya muda mfupi wanachoka hivyo kuwafanya washindwe kucheza kwenye viwango vyao. Ingawa Caf imeshindwa kuthibitisha hilo hadharani lakini imekua hali inayojitokeza mara kwa mara.
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "Ingawa Caf imeshindwa kuthibitisha hilo hadharani lakini imekua hali inayojitokeza mara kwa mara..." sasa mbona ulitaka uthibitisho wa CAF kama unajua hilo tatizo lipo mara kwa mara?

  "Hali hiyo pia ilijitokeza.. dhidi ya Sudan mjini Kharthoum..." Nini kilitokea Kharthoum, hebu taja kimoja!

  "Kamati maalum iliyo jijini hapa ilichukua uamuzi wa kuhakikisha Stars hawali..." kamati maalum ya nani, CAF, UMISHUMTA au kamati maalum ya bunge la Jamhuri?

  "Kumekuwa na hujuma katika mechi nyingi..nchi za Afrika..." Taja timu moja iliyojumiwa, ilihujumiwa vipi!

  "...ilibidi ifanyike kazi ya ziada kuwatoroka walinzi..." Ungewauliza CAF halafu ukaripoti ni utaratibu gani huo unaosema wageni hawatakiwi kukanyaga nje ya hoteli kwenda wanapotaka kula mpaka watoroke.

  Eti mwandishi anaenda kuuliza wahusika kama tatizo lipo, hapati uthibitisho, anaamua kutangaza tatizo lipo!

  Udaku!
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hizi ndio mbinu za Medani, nawatakia kila la heri katika kutupatia ushindi. Sijui mechi ijayo wale jamaa wa Senegal wanaoonesha TVyao online watatufanyia tena kama siku ya TZ na Ivory Coast, manake walionesha tu kpindi cha kwanza.
   
 4. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ,,,,Mzee inaonesha umekua mkali sana kwa huyu REPORTER,lakini kama wewe ni mpenzi wa soka la KIAFRIKA,mbona hizi ni habari za kweli tu ingawa FACTS zake ni vigumu sana kuzianika.:rolleyes::rolleyes:
   
 5. S

  SkillsForever Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio twajua wanawewkewa dawa wanachoka haraka sana...na kuishiwa nguvu kabisa.maji na chakula ndio vibaya zaidi ya vyumba kubadilishia nguo
   
 6. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  mimi hapa ndio huwa nawakubali watu kama akina Mhe. Magori
  huwezi kupelekwa pelekwa tu na wenyeji wakati huo huo unatakiwa
  kucheza nao game jioni.
  Nimekipenda kitendo hiki 100%
  BIG UP TO BRAZA MAGORI NA JOPO LAKE...
   
 7. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 60
  Fitna ya mpira ipo sana Afrika na hasa Afrika magharibi. Hongereni sana kwa kuwa makini na fitna hizo. Nakutakieni kila la kheri na mafanikio. Tujitahidi Kombe lije Tz.
   
 8. N

  Nahene Member

  #8
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 32
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa meza ya ufundi kung'amua mbinu hizo mapema, Enzi za mwalimu wangeliondoka na Mwanamalundi/shekhe Yahaya.

  Endeleeni kususia misosi yao ili mrudi na ushindi kwani watu wa magharibi ni hatari sana kwa mazingaobwe.
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Timu za kiafrika visingizio viiingi
   
 10. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mechi ya kesho ni saa ngapi wadau?
   
 11. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Amwamba, ratiba ni hiyo chini utaona na muda, nikiipaste haikai vizuri, lakini utaipata hapa Fixtures: CHAN 22/02-08/03/09 - African Nations Championship 2009 - CAF

  No Match Gp Date time Venue:
  16H00
  1. Cote D’Ivoire V Zambia A 22.02.09 Abidjan
  19H00
  2. Senegal V Tanzania A 22.02.09 Abidjan
  15H00
  3. Ghana V Zimbabwe B 23.02.09 Bouake
  18H00
  4. RD Congo V Libya B 23.02.09 Bouake
  16H00
  5. Zambia V Senegal A 25.02.09 Abidjan
  19H00
  6. Tanzania V Cote D’Ivoire A 25.02.09 Abidjan
  15H00
  7. Zimbabwe V RD Congo B 26.02.09 Bouake
  18H00
  8. Libya V Ghana B 26.02.09 Bouake
  16H00
  9. Cote D’Ivoire V Senegal A 28.02.09 Abidjan
  16H00
  10. Zambia V Tanzania A 28.02.09 Bouake
  16H00

  11. Ghana V RD Congo B 01.03.09 Bouake
  16H00
  12. Zimbabwe V Libya B 01.03.09 Abidjan

  Semi-Finals/½ Finale

  13. 1st B V 2nd A 04.03.09 15H00 Bouake

  14. 1st A V 2nd B 04.03.09 19H00 Abidjan

  3rd Place match/Match de classement

  15. Loser-Perdant: 13 V Loser-Perdant: 14 07.03.09 16H00 Abidjan


  Final match/Match final

  16. Win./Vainq.:13 V Win./Vainq.: 14 08.03.09 16H00 Abidjan
   
 12. k

  kile New Member

  #12
  Feb 28, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ahsante kwa ratiba
   
 13. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 60
  VIJANA TUPENI RAHA WATANZANIA, waTanzania sote tuko nyuma yenu.

  Mungu Ibariki Taifa Stars, Mungu Ibariki Tanzania.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kweli nakumbuka tulienda kule shinyanga kwenye mashindano ya shule za Sekondari basi unajua mchana watu wakishakula wanalala basi walitumwagia upupu si kawaida ndani ya vyumba ,ilibidi tushindwe maana ni kujikuna tu hakuna kutliza mpira.
   
Loading...