Taifa Stars vs Uganda Cranes - Live

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
cornerflagJPG.JPG


TIMU ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) imepania kushinda mechi yake ya kirafiki na Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes' inayotarajiwa kutimua vumbi kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.


Akizungumza jana katika Hoteli ya Isamilo ambako Stars imepiga kambi, Meneja wa Timu hiyo Leopold Mukebezi alisema kuwa kwenye mchezo huo Stars imeupa umuhimu wa pekee kwa madai kuwa The Cranes ni timu bora katika viwango ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).


"Kucheza na The Cranes kwenye mechi ya keshokutwa ni faida kwetu kwa sababu ni timu iliyo katika kiwango bora kwa mujibu wa FIFA, na tuna imani Stars itafanya vizuri," alisema ingawa hakuwa tayari kuzungumzia masuala ya kiufundi kwa madai yeye anashughulikia zaidi mambo ya utawala.


Mukebezi alisema timu hiyo ya Uganda iko katika nafasi ya 80 kwenye viwango vya FIFA, na ikizingatiwa kuwa ndiyo bingwa wa Kombe la Chalenji.


Alisema baada ya mchezo huo na The Cranes, Stars inatarajia kukipiga tena na Timu ya Taifa ya Somali katika mchezo unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Aprili ambapo alidokeza kuwa endapo Stars itafanya vizuri kwenye mchezo yawezekana mchezo wake wa marudiano na timu hiyo ukafanyika jijini Mwanza.


"Stars ikicheza vizuri yawezekana mechi yake dhidi ya timu hiyo ya Somalia ikafanyikia huku Mwanza, ingawa hili jambo hatujalithibitisha," aliongeza. Mchezo wa Stars na Somalia ni wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).


Juhudi za kumpata Kocha wa The Cranes Robert ‘Bobby' Williamson jana ziligonga mwamba kwani timu hiyo ambayo ilikuwa iwasili jijini Mwanza saa tano kwenye Uwanja wa ndege wa Mwanza ilikuwa haijawasili kutokana na uwanja huo kufungwa kwa muda baada ya ndege ya ATC kupasuka matairi na hivyo haikuruhusiwa ndege kubwa kutua.


Stars tangu juzi ilipowasili jijini imekuwa ikiendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa chini ya Kocha wake Mbrazili Marcio Maximo.


Hata hivyo Kocha huyo alipofuatwa jana kuzungumzia hali ya timu hiyo na gazeti hili, hakuwa tayari kuzungumzia chochote kile kwa madai kuwa mambo yote yatazungumzwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliotarajiwa kufanyika jana jioni.
 
jamani wenye matokea watujuze basi, maana wengine tuko mbali kidogo na Mwanza
 
Dah game ya leo haina hata msisimko mi nilisha sahau.
Game ya England inaanza saa ngapi wakuu?
 
Fidel,
Uzalendo kwanza mkuu.
Taifa stars ni yetu bwana Fidel.

Mi maviongozi ya pale TFF siyapendi ndo yanarudisha nyuma soka letu mnisamehe uzalendo umenishinda bora kuchagua viongozi wanao penda mpira sio wanao penda pesa za mlangoni/viingilio washibe njaa zao.
 
any update on the scores?

Uganda cranes 1 taifa stars 0. goli limefungwa dakika za mapema kabisa

salum sued ameaga rasmi kuchezea taifa stars,

wanacheza kama hawana coordination kabisa

waganda wapo nafasi ya 74 kwa viwango vya FIFA, taifa stars wako nafasi ya 108.

dakika 45 kipindi cha kwanza
 
Naona tutazidi kuporompka sasa kwenye FIFA ranking....Maximo anataka atuache alpotukuta nini?
 
Naona tutazidi kuporompka sasa kwenye FIFA ranking....Maximo anataka atuache alpotukuta nini?

shemeji nadhani ndo hivo..sasa amekula bingo yetu , hakuna programu ya vijana wala nini

unadhani tutapata wachezaji wa maana from simba na yanga? ngumu!
 
shemeji nadhani ndo hivo..sasa amekula bingo yetu , hakuna programu ya vijana wala nini

unadhani tutapata wachezaji wa maana from simba na yanga? ngumu!

Bora aondoke shemeji...Ila ningependa Kocha ajaye atoke Ufaransa aisee..Makocha wa Kifaransa wanaweza khumili mikikimikiki ya soka la Afrika,pia hujitahidi kuwatafutia Timu Ufaransa(hata za madaraja ya chini) wachezaji wanaowafundisha katika timu za Taifa...Hili limefanyika sana katika nchi za Afrika Magharibi na Kati pamoja na Kaskazini mwa Afrika(angalia Algeria,Morocco na Tunisia wachezaji wao karibu wote wanakipiga Ufaransa)
 
Uganda 1 Taifa Star 0

Lakini kipi kigeni hapa?

Tungekuwa mafarao tungekuwa na haki ya kupiga kelele...maana wale kushinda kwao mazoea na wanafanya kila jitihada kustahili kushinda. Sie twaeka makalio chini twadhani ushindi wapatikana kirahisirahisi tu kaa kutoa ganda la ndizi.

Sidhani kaa kuna kitu kigeni hapa.
 
Bora aondoke shemeji...Ila ningependa Kocha ajaye atoke Ufaransa aisee..Makocha wa Kifaransa wanaweza khumili mikikimikiki ya soka la Afrika,pia hujitahidi kuwatafutia Timu Ufaransa(hata za madaraja ya chini) wachezaji wanaowafundisha katika timu za Taifa...Hili limefanyika sana katika nchi za Afrika Magharibi na Kati pamoja na Kaskazini mwa Afrika(angalia Algeria,Morocco na Tunisia wachezaji wao karibu wote wanakipiga Ufaransa)

Ni kweli kabisa, kule wameimporove sana na ukiangalia ndo wanadominate soka la africa. Shemeji fitna inayotembea hapo TFF si unaijua? utashangaa kocha atakayekuja..nasikia kuna Mwingereza alikuwa runner up kwa maximo, anataka kutia ubani naye.....hatuendi kokote!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom