Taifa Stars kutokufikia mafanikio ni kwa sababu ya Usimba na Uyanga?

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu nimeona Katika gazeti la Mwanasport toleo la leo, Jumamosi, September 3, 2022.
.
Kupitia safu inaitwa Mpapaso ya Mwandishi Masau Bwire ametoa sababu Kuu mbili za timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars kutokufikia mafanikio makubwa
.
Mwandishi kwenye makala yake anadai KwaMba Usimba na Uyanga ndio kikwazo kikubwa.
.
Je hizi ndio sababuu Kuu za Taifa Stars kutokufanya Vzr?

Ahsante.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wanazungukazunguka Kenya Kuna Kuna timu mbili kubwa na wamefumgiwa na FIFA pia hakuna uwekezaji mkubwa lakini timu yao ya taifa ni Bora kuliko yetu, Uganda pia Kuna vilabu vikubwa lakini timu yao ya taifa ni Bora.
Kitu. Kinachochangia ubovu wa timu ya taifa I mfo mbovu wa kupata viongozi wa soka, kama yule mwenyekiti wa biashara fc sijui alikuja kutafuta nini kwenye mpira.
Wakati stand united wamepata udhamini wa Barick tuliona fujo iliyotokea baada ya kina Tishoboroha aliyekuwa kiongozi wa yanga na Azam pamoja na kina malinzi kuingiia na kutaka viongozi wawe wasomi mpaka udhamini ukafutwa na baada ya kufutwa sijawasikia TFF kuwafata na kuwaambia waweke viongozi wasomi.

Burundi wamepiga hatua kubwa Kwa kusomesha makocha na marefa wao lakini sisi makocha wetu tunawapa kozi za kuungaunga na waliomaliza hakuna hata mmoja anayejatibu kufundisha timu za nje wanabaki hapahapa kuwa wachambuzi.
TFF imeweka vigezo vya makocha wa ligi kuu lakini hakuna vigezo Kwa makocha wanaofundisha timu za vijana.
Huwezi kuwa na timu nzuri ya taifa kama hujawekeza soka la vijana.
 
Hapana sio kweli bali huku kwenye team ya taifa ya wanaume kuna majangili mengi ya mpira kuliko kule kwa wanawake ambao wao wanafanya vizuri kule kwa wanawake hakuna connection kwasababu hamasa ni ndogo.
 
Back
Top Bottom