Taifa stars imewashinda mnahangaika na Simba Sports Club mtaiweza?

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,124
11,113
FIFA ilivyokataza serikali kuingilia maswala ya michezo hasa kwenye uendeshaji wa vilabu haikukosea walikuwa na maana kubwa, fikiria timu ya taifa ilivyokuwa na hali mbaya mtu badala adeal na timu ya taifa yeye anataka kuuwa vilabu michezo irudi nyuma.

Ukienda nchini England, timu kama Liverpool,Man u, Man city, Derby country, Chelsea, ni vilabu ambavyo vilianzishwa na wananchi pamoja na manispaa miaka ya 1800-1900--- kuendelea lakini jinsi miaka ilivyozidi kuendelea mpira ukawa ni pesa bila pesa uendeshaji wa club ukawa mgumu hivyo wenzetu wakaamzisha sysytem ya kuvikabidhi vilabu kwa matajiri ili visonge mbele.

Manchester city ilikuwa sio timu inayotisha lakini baada ya kukabidhiwa kwa mwarabu wa abudhabi na kumwaga pesa ulimwengu mzima umeona balaa lake, manchester city imekuwa ni timu inayosumbua ligi kuu ya england na ulaya nzima yote hayo ni sababu ya mwekezaji.

Simba msimu uliopita kuanzia ligi hadi CAF imefanya vizuri sababu ya uwekezaji wa MO , bila pesa timu isingeweza kuwalipa akina Kagere,Okwi na wachezaji wengine, mpira wa sasa ni pesa bila pesa kuendesha vilabu ni ngumu, huyo mzee kilomoni MO akimuachia klabu hana hata mia ya kumlipa hata manula tu, wazee hawa ndio waharibifu wa soka letu.

Naishauri serikali ipambane na timu zake za Serengeti boys,Taifa stars zinazopumulia gesi waachane na vilabu, Simba msimu uliopita kufika robofainali na kubeba mabilioni haikuwa hatua ndogo wala kazi rahisi, uwekezaji ndio umeifikisha timu pale, Now tumebakiza siku 14 tu kuingia kwenye mashindano makubwa ya CAF so msituvurugie timu pambaneni na hali zenu.
 
Wanasiasa wanaogopa sana vilabu vikubwa ili wasipoteze madaraka na ushawishi, wanavihujumu, eti Rostam ndo alitumwa kumkosoa MO!
 
mzee kilomon hana hata Mia kweli? kumbuka ni m/kiti wa bodi ya wadhamini wa simba sc...mzee yupo vizuri kiuchumi hashindwa kulipa milioni 100 kwa mwaka hapo msimbazi.
 
Kwamba umeona BMT ( Serikali ) imeingilia Vilabu vyenu? Punguza Chuki dhidi ya Serikali
 
Back
Top Bottom