Taifa Stars ikisheheni nyota wa Yanga yaibamiza Somalia

Moshi25

JF-Expert Member
May 6, 2022
1,787
2,869
Jana nilitazama kiwango cha Taifa Stars ikicheza na Somalia nikafurahi jinsi timu ilicheza kwa balance ya hali ya juu huku ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, Sureboy, Farid na Feisal wakiharakisha mashambulizi mwanzo mwisho ukuta wa Mwamnyeto, Job, Kibwana na Msheri ukiwazuia Somalia kwa akili kubwa na kitaalamu zaidi nikashangaa imekuwaje tena huwa hatuchezi hivi baadae nikaona wazi kumbe Nabi alikuwa kwenye psychology ya wachezaji wa Yanga aliowafundisha kutulia na kucheza mpira.

Kuna muda niliona wachezaji wa Simba kutokuwa makini na wakipoteza sana mipira na kucheza kwa papara zisizo hitajika! Tshabalala hakuwa mchezoni na alibabaika mara nyingi na kugawa mipira kwa wapinzani wetu Somalia! Mzamiru alitoa pasi nyingi zisizo na macho na zikapotea na ilionekana kama vile Manula mechi ilimshinda kwa kutokuwa makini langoni akaomba kutolewa japo Kibu Denis nae alijitahidi kuruka ruka tu bila maajabu yoyote.

Pengo kubwa la wazi lilikuwa la Zawadi Mauya ambae nafasi yake ilichezwa na Mzamiru ambae alizembea sana na kupoozesha mashambulizi ambayo kila mara Dickson Job aliyaanzisha! Mzamiru alikuwa slow sana akikosa kabisa akili ya kushambulia kama wenzake wa Yanga yeye akiwaza kukaba, kupora mipira na kurudisha nyuma akifuata formula za Simba, Yanga wao formula yao daima mbele, peleka mpira mbele kafunge sio kuupakapaka rangi tu!

Jana nilihesabu wachezaji nikaona Yanga tulitoa karibu Robo tatu ya timu ya Taifa na ikatawala mchezo na kushinda vizuri tu, jee hii imekaaje? hii ina maana gani kwa mustakabali wa national team? Je Nabi na Eng Hersi waongezwe benchi la ufundi?

Huu msemo umejidhihirisha ni wa ukweli " Asikwambie mtu Yanga tamu" usipoila utainywa usipoinywa utaioga! ukiziba masikio utaiona kwa macho , ukifumba macho utaisikia tu mirindimo na fataki zake zikirushwa nchi nzima kutokea Sheikh Amri Abeid stadium!!
 
Jana nilitazama kiwango cha Taifa Stars ikicheza na Somalia nikafurahi jinsi timu ilicheza kwa balance ya hali ya juu huku ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga...
Yaani utopolo banah....

Haya waambie wadau hapa kuwa hao wachezaji wa uto walikiwa wakicheza dhidi ya Somalia ambayo wachezaji wake hawajashiriki ligi zaidi ya mwaka mmoja.

Halafu waeleze kuwa ni ubinafsi wa fei toto kujipigia mashuti bila akili uliotukosesha ushindi zaidi.

Pia waeleze uzembe wa Mapunyeto na kibwabwa uliopelekea hadi Manula kuumia. Na kama isingekuwa manula golini basi matokeo yangekuwa Tz 1- Somalia 3.
 
Yaani utopolo banah....
Haya waambie wadau hapa kuwa hao wachezaji wa uto walikiwa wakicheza dhidi ya Somalia ambayo wachezaji wake hawajashiriki ligi zaidi ya mwaka mmoja...
Feisal hukuona ule mpira aliopiga ukampita kipa na kugonga mwamba ulikuwa unasinzia?
 
Kama angetoa assist kwa Sopu au Kibu lile lilikuwa goli la wazi. Utaahira wa kujipigia ndio huo wa kupata off target nyingi zisizo na faida.
pale kama angekuwepo Ambundo au Nkane na Feisal kumpasia lingekuwa goli ila Kibu au Sopu wangepewa pande lile wangepaisha tu!
 
Uyanga na usimba umefika mbali sana hasa kwa mashabiki maandazi kama wewe.

Pale hawakucheza yanga wala simba ni taifa stars. Ndo maana yule mfungwa alisema wenye akili ji wawili tu pale utopoloni.
 
Jana nilitazama kiwango cha Taifa Stars ikicheza na Somalia nikafurahi jinsi timu ilicheza kwa balance ya hali ya juu huku ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, Sureboy, Farid na Feisal wakiharakisha mashambulizi mwanzo mwisho ukuta wa Mwamnyeto, Job, Kibwana na Msheri ukiwazuia Somalia kwa akili kubwa na kitaalamu zaidi nikashangaa imekuwaje tena huwa hatuchezi hivi baadae nikaona wazi kumbe Nabi alikuwa kwenye psychology ya wachezaji wa Yanga aliowafundisha kutulia na kucheza mpira.

Kuna muda niliona wachezaji wa Simba wakipoteza sana mipira na kucheza kwa papara zisizo hitajika!! ilionekana kama vile Manula mechi ilimshinda akaomba kutolewa japo Kibu Denis alijitahidi kuruka ruka tu bila maajabu yoyote.

Pengo kubwa la wazi lilikuwa la Zawadi Mauya ambae nafasi yake ilichezwa na Mzamiru ambae alizembea sana na kupoozesha mashambulizi ambayo kila mara Dickson Job aliyaanzisha! Alikuwa slow sana.

Jana nilihesabu wachezaji nikaona Yanga tulitoa karibu Robo tatu ya timu ya Taifa, jee hii imekaaje? hii ina maana gani kwa mustakabali wa national team? Je Nabi na Eng Hersi waongezwe benchi la ufundi?
Makolo watapinga

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Tujikumbushe
20220724_133629.jpg
 
Baada ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, ikafunga magoli mangapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom