Taifa litasimama imara kama tutakuwa na moyo wa kujitolea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa litasimama imara kama tutakuwa na moyo wa kujitolea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by environmental, May 5, 2012.

 1. e

  environmental JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  KILA MTU KABLA HAJAPATA NAFASI YA KULITUMIKIA TAIFA ANAWAZA JE NI PESA KIASI GANI ANASTAILI KULIPWA KAMA UJIRA WAKE, HALI HII INASABABISHA KUMALIZA KIPATO CHA TAIFA NA UPUNGUFU WA BAJETI YA MAMBO MUHIMU KATIKA UJENZI WA TAIFA. kUNA MAMBO MUHIMU YA MATUMIZI YA FEDHA KAMA MATIBUBU,CHAKULA MALAZI NA MAVAZI. KAMA KUNA WATU WAMEJITOSHELEZA KWA HAYO TUNAOMBA WATUSAIDIE KUJENGA NCHI BILA MSHAHARA. NCHI ZILIZOENDELEA ZINATAGEMEA KWA KIASI KIKUBWA NGUVU KAZI ZA KUJITOLEA. KWA UPANDE WA SIASA NI CHADEMA LABDA NA VYAMA VINGINE AMBAVYO VIONGOZI WA CHAMA HAWALIPWI. kAMWE HAMNA MSHAHARA UNAOTOSHA MATUMIZI YANA UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA NA KIPATO CHA MTU. WAGENI WAZUNGU WANAKUJA KUJITOLEA KWENYE NCHI ZETU SISI TUNAKUFA NA MAUJUZI YETU SABABU HATUNA KAZI. TUJITOLEE KWENYE KATA ZETU HASA SWALA LA ELIMU. TUFUNDISHE WATOTO NA WAKUBWA WENYE NIA YA KUSOMA BURE HUO NDIO UTAKUWA MWAZO WA KUJIKOMBOA. ELIMU TUNAYOIPATA KISIWE CHANZO NA KUJENGA MATABAKA YA KUHESIMIANA AU KUZARAULIANA.
   
 2. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mi nina moyo mmoja tu nikiutoa nitaishi vipi labda kama figo ntatoa.

  uliwahi kuona wapi mtu ana njaa akajitolea ndugu?

  hata kule vijijini watu wanajitolea kuja kukuvunia mpunga wako kama umechinja kondoo na wakawa na uhakika wa kula.

  watu hatujitolei moyo tunajitolea nguvu na lazima in return kuwepo na shukrani.


  Kuhusiana na mchakato mzima wa matumizi ya fedha za uma hapa hakiitajiki moyo bali ueledi uaminifu ushupafu huruma na uongozi bora.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Moyo wa kujenga nchi utatoka wapi? Wakati unapanga tofali tatu wenzio wanashusha tofali mbili na nusu!
   
 4. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  asante sana, maneno haya yameugusa moyo wangu.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Naomba kukuuliza mleta mada ueleze ni kazi gani wananchi wanapaswa kuzifanya bila malipo yoyote? Mi ningependa tuanzie mjadala hapa
   
 6. e

  environmental JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Elimu wengi tumesoma angalau elimu ya form six tunaweza kuanzisha utaratibu wa kufundisha majirani zetu bure wakati wa weeked au holidays au siku yeyote tupatayo nafasi.
   
 7. e

  environmental JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  akiwazacho mtu hakionekani hata ukisoma maneno ya dini kuna mahala anauliza je umekutana na wema anasema hana uhakika hata kama mmoja yupo lakini kila mtu ananafasi yake binafsi tenda wema nenda zako, kweli wengi ni wakatisha tamaa na waharibifu wa maendeleo tukipata hata mmoja kujitolea ni mwanzo tuu maana hata namba inaanza na moja. Moyo wa dhati ni muhimu.
   
Loading...