Taifa linatengeneza vijana wakatili kwa kuwanyima fursa za ajira

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,944
Habari,

Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza,

Mimi ni mtanzania kijana ninayeipenda nchi yangu na niko tayari kwa lolote ili tu niilinde nchi yangu. Suala la vijana kuwanyima ajira kwa sababu ambazo hata mtoto mdogo hawezi kuziunga mkono ni ukatili na ni sawa na kuwaandaa vijana kuwa wakatili. Kwa upande wa walimu wa sanaa ambao ni wengi zaidi mtaani na vyuoni (vikuu &kati) kutotiwa moyo na serikali yao kwamba labda itawatafutia ajira, au itawapa mikopo wapate kujiajiri ni sawa na kuliandaa bomu wakati hujui soko lake ni wapi, litalipuka mahala si sahihi.

-Walimu wa sayansi na hisabati pia serikali inawaandaa kuwa wakatili kwa nchi yao.Haiingii akilini idadi ya sekondari na uhitaji ulivyo mkubwa wa walimu hawa ili kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda serikali kudai kuwa iko mbioni kuajiri only 400's teachers tena idadi hiyo ikiwemo na wataalamu wa maabara.

Yaani walimu ni kama 300's, huu ni mchezo wa kulichezea taifa kwa maslahi ya kundi lisilojulikana. Sekondari za serikali Tanzania ziko elfu kadhaa ikumbukwe.

-Walimu wa Grade A wako utitiri mtaani na hawajui hatma yao.
* Wahitimu wa masuala ya afya, kilimu n.k ambao ajira zao zilikuwa za awamu nao wamesahaulika licha ya kauli na matamko yasiyotekeleza. Hospitali hali ngumu, upungufu wa wataalamu ni mkubwa.

Note: Kutokuajiri vijana, hamumkomoi mtu bali taifa, kwani taifa litakaliwa na wasomi wenye hasira. Please mili si mchochezi hasi bali mchochezi chanya kwaajili ya taifa.
Taifa kwanza mtu baadaye. We shall pass but Tanzania will remain till the doom day.
God bless Magufuli, God bless Tanzania.
 
ni kweli ukiangalia nchi bado inakuwa pole pole sio kusema imefika kama ulaya.serekali inaweza kuboresha fursa na michango kwa fursa hizi kwa haraka kabla wenye pesa na wageni kuzikumbatia
 
Tatizo sio ajira, tatizo ni elimu tuliyofunzwa haikuwa kwaajili ya kujikomboa kifikra bali kwa ajili ya kupata ajira! Hapo ndipo muundo mzima wa elimu yetu ulipovurugika. Sikulaumu wewe bali naulaumu mtaala mzima wa elimu yetu. Nakumbuka wakati nasoma Agribusiness pale SUA walimu wengi walikuwa na tabia ya kusema " we are preparing you to become managers". Unategemea nini kama ndio ulifundishwa mambo ya namna hiyo....
 
Mm nadhani tusiwe watubwa kulaumu sana, kazi ya serikali ni kuandaa mazingira ya ajira kwa watu wake lkn sio kuajili watu, shida ni kwamba tulishazoea toka karne na karne mtu akimaliza chuo anasubiri ajira

Nakumbuka kuna awamu moja ya rais watu walikaa home miaka sita bila ajira lkn huyu hata miaka miwili haijatimia watu tunapiga kelele sana
 
Unaongea ongea tu kwa sababu hujakutana na majaribu ya dunia hii..utakua ni mtoto mdogo wewe.mmelewa AMANI waTanzania wenzangu.
Hyo kijana ana rahisisha sana wakati hata siraha zenyewe hajawahi kuzishika anazionaga tu ziko na mapolisi

Al shabab anawajua hyo dogo?
 
kwani ulipoenda shule uliambiwa maliza kuna ajira serikalini,umepata elimu jiongeze sio kulia lia tu
 
Habari!
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, Mimi ni mtanzania kijana ninayeipenda nchi yangu na niko tayari kwa lolote ili tu niilinde nchi yangu.
Suala la vijana kuwanyima ajira kwa sababu ambazo hata mtoto mdogo hawezi kuziunga mkono ni ukatili na ni sawa na kuwaandaa vijana kuwa wakatili.
Kwa upande wa walimu wa sanaa ambao ni wengi zaidi mtaani na vyuoni(vikuu &kati) kutotiwa moyo na serikali yao kwamba labda itawatafutia ajira, au itawapa mikopo wapate kujiajiri ni sawa na kuliandaa bomu wakati hujui soko lake ni wapi, litalipuka mahala si sahihi.
-Walimu wa sayansi na hisabati pia serikali inawaandaa kuwa wakatili kwa nchi yao.Haiingii akilini idadi ya sekondari na uhitaji ulivyo mkubwa wa walimu hawa ili kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda serikali kudai kuwa iko mbioni kuajiri only 400's teachers tena idadi hiyo ikiwemo na wataalamu wa maabara.Yaani walimu ni kama 300's ,huu ni mchezo wa kulichezea taifa kwa maslahi ya kundi lisilojulikana.Sekondari za serikali Tanzania ziko elfu kadhaa ikumbukwe.
-Walimu wa Grade A wako utitiri mtaani na hawajui hatma yao.
* Wahitimu wa masuala ya afya, kilimu n.k ambao ajira zao zilikuwa za awamu nao wamesahaulika licha ya kauli na matamko yasiyotekeleza.Hospitali hali ngumu ,upungufu wa wataalamu ni mkubwa.
Note: Kutokuajiri vijana ,hamumkomoi mtu bali taifa ,kwani taifa litakaliwa na wasomi wenye hasira.
Please mili si mchochezi hasi bali mchochezi chanya kwaajili ya taifa.
Taifa kwanza mtu baadaye. We shall pass but Tanzania will remain till the doom day.
God bless Magufuli,God bless Tanzania.
Mkuu Tanzania ina rasilimali nyingi sana na Bado Mbichi sana Kifursa...Kutegemea Ajira sa Serikali ni hatua za Awali za kuupokea umasikini kwa mikono miwili hasa katika serilikali hii ya Magu...
 
Hyo kijana ana rahisisha sana wakati hata siraha zenyewe hajawahi kuzishika anazionaga tu ziko na mapolisi

Al shabab anawajua hyo dogo?
Ni wa kumtazama tu na kumuacha.anadhani MUNGU ni mzee Jolijo mpaka kuidharau amani tuliyonayo
 
Ajira sio lazima itoke serikalini, serikali inarekebisha miundombinu kama barabara, huduma za maji, umeme, afya nk, inabaki kazi ya vijana kutumia fursa hizo kujiendeleza
 
Inabidi vijana tuumizeni akili jinsi gani tutatoka. Serikali haiwezi kuajiri wasomi wote wanaomaliza vyuo vikuu. Inabidi tuchemshe bongo jinsi gani ya kuendana na mzingira.

La si hivyo, hali itakuwa mbaya sana kwa upande wetu.
 
Habari!
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, Mimi ni mtanzania kijana ninayeipenda nchi yangu na niko tayari kwa lolote ili tu niilinde nchi yangu.
Suala la vijana kuwanyima ajira kwa sababu ambazo hata mtoto mdogo hawezi kuziunga mkono ni ukatili na ni sawa na kuwaandaa vijana kuwa wakatili.
Kwa upande wa walimu wa sanaa ambao ni wengi zaidi mtaani na vyuoni(vikuu &kati) kutotiwa moyo na serikali yao kwamba labda itawatafutia ajira, au itawapa mikopo wapate kujiajiri ni sawa na kuliandaa bomu wakati hujui soko lake ni wapi, litalipuka mahala si sahihi.
-Walimu wa sayansi na hisabati pia serikali inawaandaa kuwa wakatili kwa nchi yao.Haiingii akilini idadi ya sekondari na uhitaji ulivyo mkubwa wa walimu hawa ili kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda serikali kudai kuwa iko mbioni kuajiri only 400's teachers tena idadi hiyo ikiwemo na wataalamu wa maabara.Yaani walimu ni kama 300's ,huu ni mchezo wa kulichezea taifa kwa maslahi ya kundi lisilojulikana.Sekondari za serikali Tanzania ziko elfu kadhaa ikumbukwe.
-Walimu wa Grade A wako utitiri mtaani na hawajui hatma yao.
* Wahitimu wa masuala ya afya, kilimu n.k ambao ajira zao zilikuwa za awamu nao wamesahaulika licha ya kauli na matamko yasiyotekeleza.Hospitali hali ngumu ,upungufu wa wataalamu ni mkubwa.
Note: Kutokuajiri vijana ,hamumkomoi mtu bali taifa ,kwani taifa litakaliwa na wasomi wenye hasira.
Please mili si mchochezi hasi bali mchochezi chanya kwaajili ya taifa.
Taifa kwanza mtu baadaye. We shall pass but Tanzania will remain till the doom day.
God bless Magufuli,God bless Tanzania.
Fahamu yafuatayo:-
-Serikali haiwezi ajiri kila mtu
-Serikali huajiri kulingana na mahitaji
-Jitahidi upate ajira sehemu nyingine nje na serikalini
-Jiajiri usingoje kuajiriwa.
 
Unasubiri ajira za serikali? Kaa hapo hapo mkuu Angela anakuja muda si mrefu mle matunda ya nchi!! Hivi umeshawahi kupiga hesabu ukaona ni graduates wangapi wanaoingina mtaani kila mwaka? Je, serikali itaweza kuwaajiri wote hao? Tatizo mavi-jana ya sasa hivi yana uvivu fulani hivi. Unakuta li-baba lizima linasubiria chai kwa wazee likishakunywa chai hilo kwenda ku-bet likisubiri muda wa lunch. Chekecheni vichwa vyenu jinsi gani mtaweza kutoka bila kutegemea ajira za Magufuli ambazo hazitabiriki! Namwomba Magu abane hivyo hivyo tuone kama akili hazitawarudi wavivu nyie!
 
Kuhusu walimu wa sayansi na hisabati na mafundi sanifu wa maabara, tulikuwa tunasubiri walimu waliomaliza nyuma ya 2015 wamalizie kutuma maombi yao hadi 30/03/2017. Kimsingi ni wachache sana. Hivyo maombi yao tunayafanyia upembuzi yakinifu ili tuweze kutoa ajira kwa pamoja.
Tunaomba subira yenu kama mlivyoionesha kwa kipindi chote cha takriban miaka miwili toka mlipomaliza masomo yenu mwaka 2015. Kufikia Jumatano ya wiki hii tutakuwa tumemaliza na kutangaza ajira mpya.

Back
Top Bottom