Taifa Linatakiwa Kuongozwa Na Vijana Kama Corporate Entity | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa Linatakiwa Kuongozwa Na Vijana Kama Corporate Entity

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Mar 27, 2012.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Maneno haya niliyakuta kwenye moja ya majibu ya utetezi wa Ben Sanane humu JF kwenye thread moja ambayo ghafla nisivyotarajia thread ile ilifutwa na sikuona mabaki yake na sijui imepoteaje nimejaribu sana kuitafuta na kufikili ya kuwa uenda imebadilishwa kutoka jukwaa moja kwenda jingine lakini sikupata majibu.Nimeumizwa sana kwa kufutwa kwa thread ile kwakuwa ilikuwa na mchango mzuri sana wanajF na historia kuhifadhi kumbukumbu nzuri kwa vizazi, kama vile bunge linavyohifadhi hansard za maswali na majibu na miswada ndani ya Bunge .

  Nilivutika na maneno ambayo Ben Sanane alijitetea kuwa zimefika nyakati kuwa Taifa linaitaji vijana watakaongoza kama CORPORATE ENTITY.

  Niyapenda maneno haya mawili CORPORATE ENTITY ikabidi niingine kwenye kamusi ya kiingereza na kamusi ya kiingereza vs Kiswahili,nilipata tafsiri ambyo mimi binafsi nilielewa kama ifuatavyo

  Maana na tafsiri ya Neno Corporate Entity :
  Corporate
  means relating to business corporations or to a particular business corporation. (BUSINESS)
  An Entity is something that exists separately from other things and has a clear identity of its own. (FORMAL)

  Naomba kushare na wanaJF uenda nikasaidiwa ufafanuzi juu ya maneno haya kusema kuwa Taifa liundwe na vijana kama corportae entity, maana yake nini? Is this the business issues as usual? and who is the financier of the vision and mission? What are the Obejectives and Goals? Achievemnt and success of the so related Corporate entity?

  Manake mimi navyofahamu chama cha siasa dhumuni lake ni muungano wa watu wenye kusudio la kuomba dhamana ya umma ili kupewa nguvu au madaraka [mandate] ya kutawala.Ambayo tunaweza kusema ni kuomba dhamana ya kusimamia maendeleo na ustawishaji huduma za umma.

  Manake kwa style hii ya vision and mission binafsi napata picha tofauti sana ila kupitia wanajf uenda nikapata mengi zaidi na kujifunza siasa za ujana hasa ndani ya CDM manake siasa za vijana wa Tanzania zaweza kuwa ndio bora za kuwapa maziwa na asali watanzania tukajikuta wakati wengine tunasukumwa kuangalia uwezo na ufanisi wa Mwanasiasa wengine wanasukumwa na ujana wa mwanasiasa.

  Nawasilisha.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sijui kama nimeelewa vyema but nahisi akisema 'corporate entity'
  anamaanisha...
  mfano wa kampuni ya watu weengi binafsi
  wanaounda bodi ya kampuni ni wenye hisa nyingi...na bodi ndo inaamua nani awe meneja
  nani asiwe meneja na sructure ya kampuni..

  sasa ukija kwa Tanzania leo
  asilimia kubwa ya watanzania ni vijana tena zaidi ya asilimia 65
  ni kuanzia 25 kushuka chini

  wakati aslimia zaidi ya 80 ya viongozi ni miaka kuanzia 55 na kuendelea

  sasa maamuzi yao sio ya wengi kwa maana walio weengi hawapo kwenye maamuzi

  sasa corporate entity inawapa shareholder nguvu ya kuendesha kampuni hata kama hawana elimu ya kuongoza

  na nafikiri hapo anamaanisha vijana wapewe nafasi hata kama tunaona bado hawajawa tayari kwani wao ni part
  ya wananchi walio wengi.....
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  DSN,
  Sidhani ujana peke yake ni tija. Unaweza kuwa na viongozi vijana lakini ndio wakawa wa kwanza kusaliti maslahi ya Watanzania. Unaweza kuwa na viongozi vijana lakini ndio wakawa wa kwanza kubobea katika utafunaji wa taifa hili. Tunahitaji uzalendo na moyo wa kujitolea, iwe ni katika vijana au watu waliokomaa.
   
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Ujana peke yake siyo tija, na ujana vilevile isiwe kikwazo.
  Corporate entity inamaanisha majority(in terms of shares) ndiyo waamuzi.
  Vijana ni wengi kuliko wazee, na ndiyo force inayojenga uchumi wa nchi yeyote.
  Kwa hiyo sioni tatizo wakiongoza nchi.
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama kijana mwenye maadili na vision ya kuongoza nchi akitokea sidhani kama ujana wake utakuwa kikwazo kwa yeye kuongoza kwani umma utalazimisha kijana huyo apewe nafasi kwa kubadilisha taratibu ambazo zingemzuia kupata uongozi!! The important words are "INTERGRITY AND VISION" people will demand for visionary leadership irrespective of age; if that person will inspire the populace that he could deliver them to CANAAN! Lakini I am sorry to say such a person has not surfaced in our landscape!
   
Loading...