Taifa linalojali misingi ya demokrasia lazima litengeneze mazingira kuhakikisha Rais anashinda uchaguzi kihalali

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Lazima mfumo wa uchaguzi wa Rais kizamani ambao hauendani na misingi ya kidemokrasia usiwepo tena hapa Tanzania.

Kama kuna mgombea Urais ambaye hajaridhika na matokeo basi kuwepo na utaratibu wa kupinga hayo matokeo mahakamani. Ili kuhoji uhalali wa aliyeshinda.

Kuishi na taifa amabalo baada kila uchaguzi mkuu ukifanyika ni malalamiko juu ya matokeo ya urais yasiyopingwa ni kukosa demorasia iliyokomaa. Hivyo ni wakati wa kubadili katiba ya JMT na matokeo ya urais yawe yanahojiwa mahakamani.

Kama kuna mizengwe imefanyika na mgombea aliyeshinda akapata ushindi mnono kimazabe basi uchaguzi urudiwe. Hii ndio maana ya kuwa na demokrasia iliyokomaa.

Lazima tukubali ukweli tu kuwa rasimu ya katiba ya Warioba ilipendekeza mambo mengi yenye maslahi ya demokrasia ya nchi yetu.

EPrBZmyUYAI69-Q.jpg
image_search_1614906415874.jpg
 
Back
Top Bottom