Taifa linakosea kuwaamini Maprofesa wengi kuwa Wabunge na Mawaziri

The Senetor

Member
Aug 23, 2014
41
23
Ni vibaya Taifa kuamini maProfesa wengi kukimbilia bungeni au kuwa mawaziri yaani ni sawa na kutumia gari la kubebea makontena/mchanga kubebea mikate.Duniani kote ni gharama kuandaa maprofesa hawa,hapa kwetu wanakimbilia bungeni kwa sababu ya masilahi yao mabovu.Hawa ni thinktanks za nchi ndio maana nchi zingine mfano Marekani na ulaya hutegemea maprofesa walio vyuoni kupata majibu ya matatizo ya nchi kwa kutumia research zao na wana ulinzi wa kutosha,sio rahisi kuonana na profesa wa Nyukilia au mambo ya anga au wa fani yoyote pasipo sababu maalum lakini

Kkwetu hapa wewe pita mtaani utagombania nao hata daladala,hivi kwa mfano inakuja akilini kuwaweka mbunge wa darasa la saba au form four na Professor Msola au
Prof. Mark James Mwandosyawajadiliane namna ya kuondoa umaskini?Kinachotokea maprofesa hawa wanakubali kuacha utaalamu wao kwa maslahi ya vyama au kigezo cha kusema wengi wasikilizwe au kila mtu ana haki ya kuzungumza na ndio maana wanaonekana wa hovyo kwenye utendaji wao.This is nonesense and stupidity in utilization of resources.

Kuzuia maprofesa wengi kwenda bungeni serikali iwalipe vizuri na kufanyia kazi tafiti zao na wimbi kubwa la wao kukimbilia bungeni litapungua.Narudia tena kumtumia profesa kuwasemea wananchi ni sawa na kutumia gari la kubeba makontena kubebea mikate maana hata mtu wa kawaida anaweza kusema kuwa jimboni kwao hakuna maji.
 
Hata Rais wetu anautafuta uprof kwa kila namna! Nafikiri powa tu manake wameshindwa tafiti inabidi wakimbilie sihasa. Huko ndiko kuna pesa ya kirushwa rushwa.
 
Hivi hapa Tanzania ni Research gani Professor anayoweza kufanya akaingiziwa Shilingi Bilioni 1.6 bank kwa mkupuo tena ambazo hazina kodi ? Je Maprofesa waliopo kwenye vyuo vyetu vikuu hawafanyi tafiti ? hawalipwi ? Tofauti ni kwamba wanalipwa kiasi gani, Je tafiti zao zinathaminiwa na kufanyiwa kazi ? Je Professor aliyeko pale MUHAS anaweza kuandika barua kwa mtu akaomba msaada wa kale kadispensary kake pale Gongolamboto akaingiziwa pesa ya kutakata kama ile ya Mkombozi Escrow bank ? Acheni Maprofesa wakimbilie bungeni bana !!!
 
Kwani bungeni wanaenda wenyewe Au sisi ndio tunaowapeleka, hata kama wanton rushwa lakini wanaopokea hiyo rushwa ni sisi wenyewe. Sasa tuamue kutokupokea rushwa tuone prof. Kama anaweza kuwa waziri.
Na pia tuikatae katiba ya six inayokubali mbunge awe waziri
 
Ni vibaya Taifa kuamini maProfesa wengi kukimbilia bungeni au kuwa mawaziri yaani ni sawa na kutumia gari la kubebea makontena/mchanga kubebea mikate.Duniani kote ni gharama kuandaa maprofesa hawa,hapa kwetu wanakimbilia bungeni kwa sababu ya masilahi yao mabovu.Hawa ni thinktanks za nchi ndio maana nchi zingine mfano Marekani na ulaya hutegemea maprofesa walio vyuoni kupata majibu ya matatizo ya nchi kwa kutumia research zao na wana ulinzi wa kutosha,sio rahisi kuonana na profesa wa Nyukilia au mambo ya anga au wa fani yoyote pasipo sababu maalum lakini

Kkwetu hapa wewe pita mtaani utagombania nao hata daladala,hivi kwa mfano inakuja akilini kuwaweka mbunge wa darasa la saba au form four na Professor Msola au
Prof. Mark James Mwandosyawajadiliane namna ya kuondoa umaskini?Kinachotokea maprofesa hawa wanakubali kuacha utaalamu wao kwa maslahi ya vyama au kigezo cha kusema wengi wasikilizwe au kila mtu ana haki ya kuzungumza na ndio maana wanaonekana wa hovyo kwenye utendaji wao.This is nonesense and stupidity in utilization of resources.

Kuzuia maprofesa wengi kwenda bungeni serikali iwalipe vizuri na kufanyia kazi tafiti zao na wimbi kubwa la wao kukimbilia bungeni litapungua.Narudia tena kumtumia profesa kuwasemea wananchi ni sawa na kutumia gari la kubeba makontena kubebea mikate maana hata mtu wa kawaida anaweza kusema kuwa jimboni kwao hakuna maji.

Uko sahihi kabisa. Ningekuwa na uwezo ningefanya kada ya siasa kama ya ualimu iwe kiwito zaidi, nafikiri tutapata wazalendo. Sasa hivi sote tunakimbilia siasa kwa sababu ya dili vyuoni tunafundishana wenyewe.
 
Katiba ya Warioba ilipendekeza elimu ya mbunge iwe at least 1st Degree, haya sasa imeondolewa, ngoja wajichanganye la saba na Permanent Head Damage (PhD)
^^
 
Hivi hapa Tanzania ni Research gani Professor anayoweza kufanya akaingiziwa Shilingi Bilioni 1.6 bank kwa mkupuo tena ambazo hazina kodi ? Je Maprofesa waliopo kwenye vyuo vyetu vikuu hawafanyi tafiti ? hawalipwi ? Tofauti ni kwamba wanalipwa kiasi gani, Je tafiti zao zinathaminiwa na kufanyiwa kazi ? Je Professor aliyeko pale MUHAS anaweza kuandika barua kwa mtu akaomba msaada wa kale kadispensary kake pale Gongolamboto akaingiziwa pesa ya kutakata kama ile ya Mkombozi Escrow bank ? Acheni Maprofesa wakimbilie bungeni bana !!!

Mkuu Nndu wa Selote niankuelewa una maana gani! Lkn turudi nyuma, huyu prof sijui Dr gani alipohitimu alitakiwa kufanya kazi gani? kama kweli ni prof wa kweli basi afanye kitu kwenye field yake na awaombe watu wa nje watampa fedha kuliko zile za wizi huko bungeni. Hivi mkuu kama kweli ni prof unashindwa kufanya kitu ambcho kita attract baadhi ya watu na kuweza kujenerate income? Sasa wewe unasema syijui Dispensary pale Gongo la mboto, hiyo ni biashara na inabidi akachukue mkopo benki kama wengine. Kama ni dispensary ya kutoa huduma bule basi hapo akaombe kwa NGOs za kigeni na atapata tu ili mradi asiwe msanii! Ndugu yangu kuna wasanii hata ma prof hapo Dar!
 
Back
Top Bottom