Taifa linahitaji sera, mipango na sheria kuhusu mapenzi ya jinsia moja

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Mimi Nitoe Mtazamo wangu, ambao Ninautoa Kwa Watu wa Taifa Fulani ambao Kwao Ushoga ni Swala ambalo sasa ati wanataka Kulihalalisha Mpaka Kwenye Ndoa. Bila Unafiki au hisia za aina yoyote Niseme Mashoga Wapo Kwenye Makundi.

Kundi la Kwanza ambalo Ni Kubwa Karibu 80(Kwa Mtizamo wangu) Ni wale Mashoga waliofikia Hapo Kutokana na influence ya Malezi, Kwa maana ya Manyumbani, Mashuleni, Mitaani watoto wanakokulia nk. Hawa Ni waadhirika, na wanaweka siri, siku ikigundulika na ndugu au wazazi inakuwa too late. Kundi Jingine ni la wale ambao Ukubwani sio watoto! Kwa Maamuzi yao tu wakaamua kwa ushetani wanaoujua wenyewe Kujihusisha na Ushoga kama ilivyo kujihusisha na maovu mengine kunavyokuwa. Kundi hilli Niseme laweza Kuwa Kama asilimia 15.

Lakini Kuna Kundi Lingine, (may be asilimia 5) ambao Mifumo yao ya Kimaumbile Ndio yana Dosari. Hapo Ndio Wenzangu Wakristo kama Mimi wananibishia, lakini Nikimaliza Mazungumzo wananiafiki. Nina Utetezi Gani? Mara Nyingi watu hawabishi Kuwa mtoto anaweza Kuzaliwa akiwa na Mguu mmoja, jicho moja nk Kwa Kuwa wapo Vilema na Tunawaona, ni fact.

Lakini Pia tujue upungufu Unaweza Usiwe Kwenye Viungo Vinayoonekana au Viungo vya nje. Mfano Kama Kuna Kilema anazaliwa na Jicho moja Pia Kuna Kilema mnisamehe, ni mwanaume lakini, Nanilii yake ina ukubwa wa sentimeta 3 (Njiti ya Kiberiti au sigara Uikate Nusu) Na pia huyuhuyu unaweza Kuta hormone zake za mwilini ni za Kike au Kike zaidi. Je Ni mara ngapi tumewaona Wanaume wenye maumbile ya kike mpaka matiti anayo? Niseme Tu Kama Kuna Ukilema wa Viungo pia Kunaweza Kuwa na Ukilema wa Hormone, sasa Wakristo wanaogopa Ukisema hivi unamlaumu Mungu, Kwani Mbona Nikisema Kipofu nisionekane namlaumu Mungu?

Kwa lile Kundi La Kwanza Sitalaumu Serikali, Kama inavyokabiliana na Vitendo vya Unajisi wa watoto Pia Kukabiliana Kwa Nguvu zote na watu au Taasisi zinazotaka Kupromote Usenge na Usagaji Katika nchi za Afrika. Hata Hivyo Ni Jukumu Complex la Kitaifa na Linaahitaji sera, Mipango na Sheria na Sio Maamuzi ya Mwendawazimu anayetafuta sifa za Kijinga jinga.

Kwa Makundi Mengine Iwekwe sheria ya Kumkataza Ndoa za Mashoga, Na hata pale inapokuwa wazi Mashirikiano ya Kiwazi ya Kuinfluence jamii.

Kwa Kundi La Mwisho Tunachoweza Kuwaomba na Hata Kushurutisha juu yao, Wasiwe influence kwa walio sawa, Kwa Maana Kipofu, Kiziwi angekitaka Kutoboa wengine Macho ili wawe Vipofu Kama yeye ingawa sio Kosa lake Kuwa Kipofu, Lakini Huko Kutaka Kupofusha wengine Kuwa Vipofu, hilo atambue ni Kosa! Zaidi ya Hapa, Kuna Matatizo Mengine au Maswali Mengine Duniani Tunatafuta Wazimu bure tukitaka Majibu!
 
TL. Kwa hiyo kama hormones za anaye onekana ni mwanaume ni za kike, huyo mwanaume kwa nini ASIWE na ka UKE? Kwa nini atumie Unyeo kukidhi haja ya mapenzi?
Kama hormones ni za kike mbona hapati mimba?
 
TL. Kwa hiyo kama hormones za anaye onekana ni mwanaume ni za kike, huyo mwanaume kwa nini ASIWE na ka UKE? Kwa nini atumie Unyeo kukidhi haja ya mapenzi?
Kama hormones ni za kike mbona hapati mimba?
Mkuu ukisoma mambo ya genetic mara nyingi hormone huwa zinaathiri tabia kwahiyo unakuta mtu anakuwa na hisia za kike, tabia za kike, hisia kwa wanaume wenzie hata kama ana uume. Kwahiyo mleta mada kama alivyoongea hili kundi la mwisho ni ngumu kulilaumu moja kwa moja .
Niishie hapa
 
Je Monsanto wameshafanya mavitu yao nini? Pia ni kwa nini ushoga unapigiwa vuvuzela sana?
 
TL. Kwa hiyo kama hormones za anaye onekana ni mwanaume ni za kike, huyo mwanaume kwa nini ASIWE na ka UKE? Kwa nini atumie Unyeo kukidhi haja ya mapenzi?
Kama hormones ni za kike mbona hapati mimba?
Mimi sitetei au kuhalalisha, Na Ukiniuliza Utakuwa Unanionea, Mimi sina jibu, Nasema tu observation zangu.
 
Watu hapa Msidhani Kuwa Nahalalisha au Kutetea Ushoga. Niseme Kwa Serious terms, Hata kama Bibilia Ninayoiamini Ingesema Kuwa Hiyo sio dhambi, Hata kama Kungekuwa hakuna Mungu, Bado Ningeendelea Kuamini Ushoga sio asili na sio sawa. Na Kama Mwanangu ningegundua anaushoga, Nitajifungia Ndani Bila Kula Nisali, Mawili abadilike au mimi nife nisiishi na kudeal na hayo. Nilichokisema, Ni Kuwa Huo Ndio Mwonekano na Makundi ya Mashoga. Sijatetea au Kuhukumu mtu.
 
Mnamzungumzia huyu?
2e9ccbc14df2f3666b337bb406959576.jpg
 
Kama tatizo linasababishwa na mapungufu ya hormone na maumbile tutakuwa tunakosea tukilaumu .
Lakini hawa wa kundi la kwanza na la pili hapa jamii tunabidi tuwajibike na Serikali kwa ujumla.
La sivyo kizazi hicho haramu kitaongezeka na baadae tutajikuta tunakosa mwelekeo.
 
Je Monsanto wameshafanya mavitu yao nini? Pia ni kwa nini ushoga unapigiwa vuvuzela sana?

Hakuna anayetetea ushoga ila tusiwe wanafiki kiasi hicho, hebu niambie hakuna mahusiano yoyote kati ya ushoga na hormone?
 
Kama tatizo linasababishwa na mapungufu ya hormone na maumbile tutakuwa tunakosea tukilaumu .
Lakini hawa wa kundi la kwanza na la pili hapa jamii tunabidi tuwajibike na Serikali kwa ujumla.
La sivyo kizazi hicho haramu kitaongezeka na baadae tutajikuta tunakosa mwelekeo.
Umeongea vizuri, lakini unakuta mnafiki mwingine eti kila ushoga ni wa kujitakia
 
Watu hapa Msidhani Kuwa Nahalalisha au Kutetea Ushoga. Niseme Kwa Serious terms, Hata kama Bibilia Ninayoiamini Ingesema Kuwa Hiyo sio dhambi, Hata kama Kungekuwa hakuna Mungu, Bado Ningeendelea Kuamini Ushoga sio asili na sio sawa. Na Kama Mwanangu ningegundua anaushoga, Nitajifungia Ndani Bila Kula Nisali, Mawili abadilike au mimi nife nisiishi na kudeal na hayo. Nilichokisema, Ni Kuwa Huo Ndio Mwonekano na Makundi ya Mashoga. Sijatetea au Kuhukumu mtu.
Ndugu usifikirie kujiua, dunia na changamoto zake ndio maisha yenyewe. Kama inatokea hali hiyo, Mwenyezi Mungu atuepushe, sali pamoja naye na kama kuna matibabu na ushauri nasaha ni kuwa naye bega kwa bega. Ikishindikana kubali matokeo, lakini angalau umejitahidi.
 
Back
Top Bottom