Taifa linaendeshwa kama gari Bovu

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Hakuna tena utata kuwa sasa kama taifa tunazunguza Lugha moja kuwa tumepotezana angani na anaye jaribu kutudanganya kuwa tupo ktk njia salama na tuendelea kutulia ktk siti zetu bila ya kutafuata Majaketi ya kujinusuru huko Angani ni mnafiki au haopgopi madhara ya kupotezana Angani wakati chombo kinaendeshwa na Dereva asiye aminika na Abiria.

Kwa sio tuu kwamba Dereva anayumba na chombo chake bali hata taasisi yake inatiwa unajisi mbele ya jamii na Dunia ya kimataifa kuonekena kuwa taasisi ya hovyo kuliko kawaida.

Kumuamini huyu Dereva kunahitaji kuwa na Kichwa cha Mwenda wazimu na mwili wa Nungu nungu na mikono ya kinyonga na moyo wa Popo.

Kocha anaye fanya mabadiliko ya wachezaji kwa kubahatisha katika mechi muhimu ya kufuzu ujue hana kitu kichwani bali anafuata mayowe na hisia tuu ya mashabiki na ni hatari kwa usalama wa timu.

Yaani mpira umeanza Kocha anamtoa mchezaji dakika ya 30 na kuwaeleza kuwa mchezaji huyu hana kiwango. Halafu dakika ya 57 kocha anamuinua mchezaji yule yule aliyetolewa uwanjani na kuwaeleza kuwa huyu ndio mchezaji muhimu kwa timu yetu kupata ushindi hahaaa.

Hivi mtu gani mwenye Akili timamu anaweza kumuamini Kocha kilaza kama huyu? Halafu anawaambia Mashabiki shangilieni kwa Nguvu sanaa na kutembea kifua mbele kwa kumuingiza uwanjani mchezaji aliyetolewa kipindi cha kwanza.

Makocha kama hawa Mawe ya mashabiki na matusi huwa yatawandama mpka wanakufa. Watu tunahitaji uhakika wa mchezo uwanjani na sio kuleta zako za kuleta hapa. Hii timu sio yako wewe kocha umeikuta na utaiacha sisi ndio wenye uchungu nayo.

Unaonekana huna mbinu za mchezo na unatumia Nguvu kuliko Akili kupata ushindi wa lazima. Soka ni sayansi kaka kama hujui hujui tuu acha kujimwambafy.
 
Ukiacha kufuatilia mambo yao utaishi kwa amani sana mkuu. Nakushauri hangaikia familia yako, hangaika na Mungu wako, hakika utapata amani ya moyo
 
Hapo tatizo lipo kwenye Katiba ya mwaka 1977 iliyotoa mamlaka makubwa ya kiuteuzi kwa mtu mmoja tu na pasipo kuhojiwa na mtu yeyote yule au huyo mteuzi kuidhinishwa na chombo chochote kile .

Tupambane tu kuipigania Katiba mpya ya wananchi tuliyoipendekeza wenyewe mwaka 2012! Kupitia katiba mpya, huo udhaifu huenda ukaisha au kupungua kwa kiwango kikubwa.
 
Kuna mahali unawaza sasa watoto wameenda shule wamehitimu vizuri lakini hawapati kazi nawe unaishi mjini. Wengine walipata kazi lakini wenye kampuni wamefunga virago. Wote wako mitaani. Unajiuliza hii ni nini. Mjomba waliyemtegemea katumbuliwa. Akili inachaka joto linazidi. Kawaida binadamu atamlaumu hata muumba. Mola mbona hunioni shida zangu? Seuse mwanadamu!
La msingi tunapata akili mpyya lakini kusema hakutaisha
Ukiacha kufuatilia mambo yao utaishi kwa amani sana mkuu. Nakushauri hangaikia familia yako, hangaika na Mungu wako, hakika utapata amani ya moyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom