Taifa lina haki ya kuwajua viongozi wakuu wa upinzani waliopata mgao ESCROW

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
kuna tetesi ambazo kila mahali zinazimwa kwamba kuna viongozi wakuu wa upinzani waliopata mgao,kama taifa tuna haki ya kuwajua
 

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
2,660
1,225
WAKULU ---stanbic bank waliochukulia kwenye viroba; Sandalusi na mabagi ya rambo. Ndg yangu kwa hakiri ndogo tu Kama pesa zilizochukuliwa kwenye hiyo bank zingechukuliwa na Upinzani au mtu wa Kawaida isingechukua hata dakika ukajua majina. Tumia hakiri Kidogo tu utajua zimechukuliwa na kundi gani la watu.Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ndo hao majina hayatajulikana hadi mkojo wa kuku uonekane duniani.
 

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
kuna tetesi ambazo kila mahali zinazimwa kwamba kuna viongozi wakuu wa upinzani waliopata mgao,kama taifa tuna haki ya kuwajua
Yaani kwa hali ilivyo na kwa jinsi CCM walivyo juu ya sakata hili kungekuwa na kiongozi wa upinzani aliyepewa fedha hizo yaani wangekaa kimya? Tafakari kwa makini ndugu kwa hiki ulichokiandika.
 

wabuyaga

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,685
1,225
Mkuu nguvu yako yote ingekuwa ni kuhakikisha walioiba wachukuliwe hatua! kumbuka kuwa bila mkono wa serikali hakuna member wa upinzani anaweza kupata hata sh moja
 

kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,785
2,000
kuna lile genge la vyama visivyokuwa na wabunge likiongozwa na chama cha ccj,wale wamechukua
 

kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,785
2,000
kuna lile genge la vyama visivyokuwa na wabunge likiongozwa na chama cha ccj,wale wamechukua
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
kuna lile genge la vyama visivyokuwa na wabunge likiongozwa na chama cha ccj,wale wamechukua
Mbatia kajengewa nyumba ya ghorofa kule nyumbani kwao hili nalo lipo wazi sana huhitaji kutumia akili nyingi lipo wazi sana.
 
Nov 26, 2014
19
0
kuna tetesi ambazo kila mahali zinazimwa kwamba kuna viongozi wakuu wa upinzani waliopata mgao,kama taifa tuna haki ya kuwajua
Tumia akili ya kawaida na wewe ndugu yangu. Hivi kwa mile kibano walichopata serikali kwa ule mjadala bungeni..kama kuna mpinzani angekuwepo unahisi wasingetaja ili kupunguza kasi ya kibano? Wao wana orodha yote ya wakwapuaji ndo maana hadi kesho hutaisikia orodha. Tumia common sense na wewe bhana..
 

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,324
2,000
kuna tetesi ambazo kila mahali zinazimwa kwamba kuna viongozi wakuu wa upinzani waliopata mgao,kama taifa tuna haki ya kuwajua
iparamasa, pole sana. Unaonaje kama mada yako ingesomeka hivi; kuna tetesi ambazo kila mahali zinazimwa kwamba kuna viongozi wakuu Ikulu waliopata mgao, kama taifa tuna haki ya kuwajua! Hakuna Kiongozi wa Upinzani mwenye uwezo wa kuzima tetesi kama unavyodai; wenye uwezo huo hata wewe unawajua vizuri sana. Pamoja na ukweli huo, wengi wetu hatuangalii itikadi, mwizi ni mwizi tu awe anatoka Chama tawala au Upinzani ila mpaka sasa wale wote, ambao ushahidi umepatikana kwamba walilamba, hakuna wa kutoka Upinzani.

Kweli unaamini angekuwepo mpinzani, hiyo habari haingekuwa "breaking news" si mtaani tu bali hata humu JF; yaani wewe iparamasa, pamoja na wenzio MSALANI, gsu, MwanaDiwani, FaizaFoxy, Lizaboni, T2015CCM, jMali, thatha, Elungata, Ritz, Simiyu Yetu et al, mngekaa kimya? Mimi ninataka yeyote yule aliyehusika kwa namna moja ama nyingine awajibishwe bila kujali itikadi, cheo, wadhifa au dini. Najua CCM inahaha ikitafuta kaupenyo ka kutokea na hii mada yako ni ushahidi wa jitihada hizo...kuihusisha Upinzani, kalaghabaho!
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
29,989
2,000
kuna tetesi ambazo kila mahali zinazimwa kwamba kuna viongozi wakuu wa upinzani waliopata mgao,kama taifa tuna haki ya kuwajua
mleta mada nihakikishie kuwa uko timamu kwanza.coz kwa akili ya kawaida hilo lingekuwa ni chance ya kuharibu mjadala.unaona hata Zito alivyokuwa attacked na Lusinde ila ikakosa mashiko
 

Bwiru boy

Member
Nov 29, 2014
88
95
Sina hakika kama umeandika kwa ushabiki wa kisiasa au ukiwa huru kiitikadi za kisiasa. Siku chache nyuma kabla ya report ya PAC kulikuwa na uzi humu ndani ukimtaja Mbowe kwamba kapata mgawo, sijui kama ni kweli au la! Lakini kama kuna viongozi wa upinzani wamepata mgawo, Report ya CAG na TAKUKURU zimeshindwa nini kuwataja hawa wapinzani wao ambao kila siku wanawasema ubaya wao na udhaifu wao kwenye majukwaa ya siasa na hata bungeni?

Katika masuala yanayoliingiza taifa katika aibu na hata kusababisha maisha magumu kwa wananchi ni vema tukaweka mapenzi yetu ya vyama mbali kabisa. Kama wapo ni vema wakatajwa ili na wenyewe tuanze kuwachuja ni nani anatufaa na ni nani hatufai. Tunaomba hii serikali yetu yenye police na Takukuru iwataje wote (kama wapo, siyo majungu na kuchafuana tu) na hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom