Taifa limelogwa na alieliloga kafa

mtima nyongo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,947
2,047
Watanzania tu watu wa ajabu sana na hatuna tofauti na watoto wadogo,
Ccm imekaa madarakani miaka zaidi ya 50 na viongozi wake ni wale wale wanaotokana na mfump wa ccm. Toka enzi ya mkapa mpaka sasa karibu wanaccm wote ni wale wale inamaana hata sera lazima wafuate za chama. Mkapa tuliambiwa ni mr.clean na kweli alifanya awezayo na kukaa pembeni,akaja jk huyu mpaka kitabu kikatungwa JK TUMAINI lililolejea nae akakaa madarakani na muda umefika kakaa pembeni.

Sasa kaja mr.jpm a.k.a chaguo la mungu a.k.a sokoine a.k.a malaika a.k.a kibao lakini huyu nae ni zao lile lile la ccm Kuna ufisadi kila sekta ndani ya taifa hili na katika uozo wote yeye alikuwepo na pia kwenye vikao vya baraza la mawaziri alikuwepo Ina maana katika wizara zote alizotembea akuliona hili la watumishi hewa? Ili tuweze ksonga tunahitaji kiongozi mwenye uthubutu na asie na chembe chembe za uccm

Kwa maana hata sasa jpm awezi kufanya zaidi ya matakwa ya chama kwa sababu hata sitta alikua vizuri kwenye misimamo lakini mwisho wa siku bado chama kilimmeza Kama kweli jpm angekua na uthubutu wa kukomesha ufisadi nchi hii kwanza angedili na watangulizi.kupitia mikataba ya gesi na migodi upya na baada ya hapo ndio aje kudili na hawa mabosi wa mashirika ya uma.

Kama mtakumbuka kipindi majaliwa anaelekea bandari na kukuta madudu kwenye mafuta na kuhoji lakini mama wa watu akajibu ki ufasaha ni maagizo toka juu lakini cha ajabu mama katolewa mtuma sms kaachwa Leo hii kuna kashifa ya lugumi lakini kwa mwendelezo ule ule wa uccm nayo itakufa kama zilivyokufa nyingine Leo hii ukiwa unaendesha gari mfano kuanzia kimara kuelekea moro barabara inakuvuta kwa sababu ya ubovu wake na hiyo ni moja tu ya barabara nyingi tu za nchi hii.

Lakini kwa ufinyu wa mawazo na kufikiri kwa watanzania wanashangilia lakini wanashindwa kujiuliza hivi hwa hawa ndio waliolifikisha taifa hapa lilipofika na kwa nini waahidi kisichofanyika? Leo kuna sera ya majipu lakini hii sera ya majipu ukiifutilia aina mantiki kwa mtanzania wa kawaida kwa sababu suala la kodi ni wajibu wa serikali na kama watu walikua awalipi huo ni uzembe wa serikali. Wajibu wa serikali ni kuboresha huduma za jamii kwa makusanyo ya kodi Ushauri wangu kwa jpm ni kuachana na chama kama alivyofanya mutharika lakini akiwa bado ndani ya ccm alafu aseme anapambana na ufisadi huo ni uongo hilo suala aliwezekani ndani ya ccm


karibuni kwa mjadala wadau
 
Ni kweli watanzania tuna matatizo na ndiyo maana kwenye uchaguzi 2015 tuliwekewa wagombea wawili wa vyama tofauti ila wenye chembe chembe za ccm.
 
Watanzania amjapata watu sahihi wa kuiondoa ccm yaan mnasahau lowassa pia alikua ccm kama ccm ni mafisadi lowassa ni nani watanzania tumelogwa kumshangilia dalali lowasa na kumpa jina la mabadiliko
 
Watanzania amjapata watu sahihi wa kuiondoa ccm yaan mnasahau lowassa pia alikua ccm kama ccm ni mafisadi lowassa ni nani watanzania tumelogwa kumshangilia dalali lowasa na kumpa jina la mabadiliko
Ni kweli kabisa mkuu. Tusubiri watoto waliozaliwa mwaka 1992. Hao pekee ndio watakao kuwa nje ya ccm
 
Back
Top Bottom