Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,938
Habari wanajukwaa.
Katika pitapita yangu huku na kule, mitandaoni na hata katika mazingira halisi nazidi kuona vijana wako katika wimbi la ujinga.
Nimeona vijana wakishare pages na picha za watu maarufu kwa kuahidiwa kupewa zawadi mbalimbali hasa simu za iphone zenye gharama ya juu.
Mtu anasema nina simu 1000 kesho jioni nazigawa kwa watu 1000, ukishare mara nyingi utajinyakulia zawadi hii.
Wanashindwa hata kujiuliza maswali kama haya;
1. Simu 10000 zenye thamani ipatayo kama milioni 2 kila moja zitakuwa na gharama ya jumla ya sh. ngapi na je, nani aitoe bilioni mbili kwa vijana kama zawadi kwa kushare page yake tu?
2. Kama yeye atatoa zawadi zenye gharama ya bil.2 atapata faida gani ya ziada na kwa namna gani?
Halafu cha ajabu ujumbe ukiuangalia kwenye source yake kabisa ulitumwa miezi miwili nyuma ukisema zawadi zinatoka kesho lakini wao wanasambaziana kila leo.
Kama kijana anamtukana mwenzake kisa Manchester United au Arsenal huku ameusahau undugu wa kitaifa utasemaje huyo kijana yuko timamu?
Tusipoomba kwa nguvu mapema taifa litazidi kuzalisha vijana wa ajabu.