Taifa limeanza kupotea rasmi kiuchumi na kisiasa awamu ya kwanza kuanzia mwaka 1967 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa limeanza kupotea rasmi kiuchumi na kisiasa awamu ya kwanza kuanzia mwaka 1967

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Aug 5, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wafadhihina wa SIASA ZA UJAMAA na KUJITEGEMEA hoja hizi zinaweza kuwa mwiba usiong’oka kwa koleo ya chuma. UKWELI UTATUWEKA HURU, siasa ya Ujamaa na Kujitegemea zilikiuka kanuni ya usawa na demokrasia pevu.

  Fikra kama vile chama kushika hatamu (party supremacy) zimekiuka kanuni hizo. Mipango inayowapa binadamu au kikundi cha binadamu mamlaka makuu-enzi-kuu-(supremecy) ni mpango usiolingana na kanuni za usawa, demokrasia na Maendeleo.

  Leo hii mienendo na tabia za wananchi wa Tanzania imezungukwa na woga, hofu kwa sababu katiba ya nchi, mipango ya utawala na sheria za nchi zimewalazimisha watanzania kunyimwa uhuru kamili wa kutoa maoni yaon bila vitisho (rejea detention act) na hivyo kuleta changamoto za kimaendeleo.

  Ujamaa na kujitegemea ni maneno mawili yasiyo na uhusiano ni sawa na kuchanganya maji na mafuta (completely immiscible). Katika hali ya kawaida katika kipindi cha miaka mitano toka kupata uhuru kuanza kuhubiri siasa ya kujitegemea bila kujenga misingi imara ya uchumi ni maneno matamu yasiyo na kanuni imara za kiutendaji.

  Shabaha kuu za azimio la Arusha chini ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inahitaji nguvu, amri kali na utawala wa aina ya kijeshi. Siasa hizi hazijazingatia ule ukweli wa binadamu na hisia za ndania za asili ya watu. Ni siasa za kufikirika zaidi.


  Mashamba ya jumla (collective or communal farms) kuanzia vijiji vya ushirika mpaka kufikia kijiji cha ujamaa ni zao la misingi dhaifu ya kukua kwa uchumi na hatimaye maendeleo nadi ya Taifa letu.

  Utaifishaji na umilikaji wa shughuli tofauti za umma nje ya NJIA KUU ZA UCHUMI umechelewesha na kudhoofisha maendeleo ndani ya taifa letu.

  TUSIAMINI MAZINGAOMBWE, TUAMINI UHALISIA (REALITY)
   
 2. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nia ya Azimio la Arusha na siasa za ujamaa na kujitegemea ilikuwa nzuri. Nia ya Mwl. Nyerere ilikuwa nzuri ndo maana hakujilimbikizia mali kama akina Mobutu, Bokassa nk. jambo alilokosea ni moja tu; kutowapiga risasi viongozi walio endekeza rushwa na kufilisi na mali za umma.

  China, N. Korea, Urusi, Cuba na wajamaa wengineo waliofanikiwa, hawahamishi mwizi ili akaibe pengine, bali kesi inaishia hadharani peupe kila jicho linaona. Tusimlaumu na wala tusitafute kuwatetea genge la mafisadi la sasa kwa kumtupia lawama Mwl. Nyerere.

  Hawa viongozi wengi wa sasa tu-deal nao kwani ni wana utajiri haramu kuliko tunavyofikiri.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Unajua wenzetu kama kitu wanakiona ni tatizo wanatoa na suluhisho...sisi suluhisho letu la kiuchumi ni nini? Kulaumu azimio la Arusha? Kushangaa azimio la Zanzibar ambalo nalo limetengeneza tatizo kubwa kuliko lile la Azinmio la Arusha. What is your take mtoa thread?
   
 4. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,963
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Sawa kabisa, uchumi wa Taifa ulianza kudorora tangu azimio la Arusha lilipoanza mwaka 1967, zipo sababu kubwa za msingi zilizoporomosha uchumi wetu kwa kasi, nitajaribu kueleza chache:-

  a) Kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa.

  Nyerere alidhamiria wananchi wakae pamoja kwenye vijiji, ili waweze kupewa huduma muhimu kama maji, shule, hospitali, umeme nk. wakati huo serikali ilianza mpango wa kuwaondoa wananchi waliosambaa vijijini na kuwakusanya pamoja na kuanzisha vijiji vya ujamaa.

  Serikali haikufanya maandalizi yeyote, ambayo yangewawezesha hawa wananchi waendelee kuishi maisha ya kawaida bila usumbufu. Serikali iliwavyunjia wananchi nyumba zao na kusombwa na malori na kutupwa maporini maeneo ambayo hayakuwa na huduma yeyote ya kibinadamu kama nyumba, maji nk. Serikali ilichofanya ni kuwapimia kila mwananchi eneo lake la kujenga na kupewa ekari 2 za kulima, pamoja na mashamba ya ushirika.

  Maisha yalikuwa magumu na ya kikatili hakuna mfano, wananchi walikuwa hawana chakula na akiba ndogo waliyokuwa nayo haikutosheleza mahitaji yao. Kazi ilikuwa ngumu ya kuanza kufeka mapori kwa ajili ya kilimo pamoja na kujenga vibanda vya kuishi. Ni kipindi ambacho wananchi wengi walipoteza maisha kwa njaa, magonjwa na kuliwa na wanyama pori.

  Mazao ya chakula na biashara yalianza kuadimika, kwani kuazisha shamba jipya bila msaada wa serikali ilikuwa siyo kazi rahisi, hivyo serikali ilianza kuhemea chakula toka nje ya nchi kulisha wananchi wake.

  b) Kutaifisha viwanda na mashamba

  Kabla ya mwaka 1967 zao la mkonge ndilo lilikuwa likiongoza kwa kuingizia serikali pato la nje, wenye mashamba kwa ushirikiano na nchi zao wakaazisha kampeni za kutumia kamba za manila, meli zote zilikuwa zinatumia kamba za mkonge kufungia bidhaa kwenye meli na sehemu nyingine, ghafula bila ya kutarajiwa idadi kubwa ya meli wakaachana na mkonge na kutumia kamba za manila.

  Nyakati hizo magunia ya mkonge ndiyo yaliyokuwa yanatumika sana kwenye vyama vikuu vya ushirika kuhifadhi mahindi, kahawa, maharagwe, mpunga, nk. Wakati huo wakaleta mifuko na nailoni (viroba) ambayo bei yake ilikuwa ni nafuu kuliko mifuko ya mkonge kufungia nafaka, kuanzia kipindi hicho bei ya mkonge iliporomoka vibaya sana, hadi serikali ikayacha mashamba iliyoyatifisha kuwa mapori.

  Serikali ilipotaifisha mashamba makubwa ya kahawa, wazungu walitengeneza wadudu wa maabara na kuingizwa nchini, wadudu hao walikuwa wanauguza kahawa ikiwa changa, kukausha majani ya miti ya mibuni, hali iliyoporomosha uzalishaji wa kahawa kwa kiwango kikubwa.
   
 5. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kabisa A.A lilikuwa ni ukandamizaji wa fikra bunifu kwa malengo ya wachache ambao walidhani wanaweza kuwaamulia wana jamii nini cha kuzalisha whilst not considering individual choices. Hii ni namna moja ya ukandamizaji, lakini what is the different now? maana kuna vyama vingi wote wanalilia namna moja ya uzalishaji negating the concept of competing ideologies; wote wakiwa wajamaa kwa upande mkubwa.

  Serikali yetu bado aijabadilisha mfumo kusema kwamba sisi ni mabepari, maana at the fore front of capitalism ni market forces and maximising profit. Embu angalia kama sekta moja tu ya utalii and compare to our rivals in-terms of spectacle and services offered. Tazama nchi kama S.A, Kenya, Namibia and a few other countries that have similar national parks.

  Wenzetu wanatumia muda mwingi kuwekeza kwenye sector and appointing the competent to run those sectors. Maana kuna mlolongo wa mambo mengi ambayo management inabidi kufuata in terms of strategy ya kukuza mapato and attracting visitors. Sisi tunadhani ukiweka matangazo ulaya na ukienda kwenye mabanda ya maonesho is enough. Wakati huko nyuma uongozi auna mipango wala mikakati ya ushindani na namna zakuiba wateja wa wengine wao wapo pale kwa sababu wameteuliwa tu kwa sababu azijuazo mteuaji bila ya kuzingatia faida.

  Tanzania imejaza watu kwenye taasisi ambazo zinaweza kutuletea serious kipato ambao zimejaza wahalifu huyo CAG huko wala haendi sana. Hili taifa ni sikio la kufa, CCM ikiendelea kuongoza na kipindi hichi ambacho watu wameshaanza kuchoka. Na ukizingatia design zao za kutoa viongozi kimakundi regardless of their competency hata kama hafai, kisa katoka kundini hili kuweza kurudisha wapuuzi walewale madarakani tunakoelekea ni mitutu tu in the next 20years.

  Hii nchi inaenda kwa mwenendo wa mwendawazimu amna mipango ya kesho. You can not measure the success of MKUKUTA and the five years plan is heading into its third years amna matunda ya kupima.
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Stop your mental degradation of GREED... Kama tungeacha ARDHI kutommilikisha Mkulima Masikini hata kama

  Hakuendelea lakini alielezwa Umuhimu wake hata kama ni 70% tu ambao uwanajua Umuhimu wa ARDHI ni bora

  kuliko kama tungeiacha hii ARDHI kwa watu wachache; Kuacha nchi kuwa na Matabaka na Unajua wakati ULE

  Ndugu zetu Waislamu Wengi wao hawakua na ELIMU; Hawakuna Na ARDHI, SHULE NYINGI ZILIKUWA ZA DINI ya

  Kikristo Na MASHAMBA Makubwa ya Kibinafsi ambayo yalikuwa yanatafuta Wafanyakazi rahisi ambao Hawajasoma

  Hiyo ni DHAMBI... Sitalaumu hata kidogo Utaifishaji wa 1967 ilimkumba babu yangu Mzaa Baba haswa lakini imetuletea

  Umoja... Hata kama sasa hivi CCM inataka kuuondoa... lakini kwa miaka 50 ni ajabu... Sasa tuna MADINI na GAS

  Tutaweza kuijenga nchi yetu vizuri sana... ni kuleta viongozi wazuri tu...


  View attachment nyerere in action.docx View attachment nyerere in action.docx

  [​IMG]
   
 7. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Fikra na mitazamo mbadala ni vitu vyenye matumizi na manufaa yake vikichukuliwa kwa uangalifu. Dunia ipo kwenye riadha na maamuzi yoyote yale lazima yaangalie matarajio ya kesho na kuyapima kwa uangalifu zaidi.

  Ulimaji wa pamoja (collective farming) ni maneno rahisi ambayo hayazingatia mahitaji makubwa. Mfano kama kiijiji kina familia 2,000 na shamba la ekari 2,000 za mazao ya chakula. Kila familia itapata kiasi gani? Na itachukua muda gani mpaka zile familia ziwe na ekari 20,000 za mazao? Tazama upande wa pili, UCHUMI wa TAIFA na upime mahitaji, na hicho ndio kitakuwa kipimo cha mafanikio.

  Utazungumziaje DEMOKRASI, UJAMAA na MAENDELEO wakati umeweka vizingiti ambavyo vinamnyima raia uhuru kamili na kuhoji, kuamua na kushiriki kiakamilifu katika shughuli za kisiasa na kiuchumi? Tazama katiba ya nchi, mipango ya utawala na sheria za nchi, je zimetoa UHURU kamili wa kifikra katika dhana ya "UHURU na MAENDELEO"

  Iwapo utawala upo juu ya mahakama na bunge, je haki za raia ziko wapi?
   
 8. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ujamaa lazima uwe blended na Capitalism na kuweka policies ambazo zinakidhi mahitaji ya nyakati na matarajio ya baadae kwa kuzingatia ushindani wa dunia kisiasa,kiuchumi,kiteknolojia n.k. Kuepukana na propaganda na maneno rahisi na kukubali mabadiliko ndio kipimo cha uhai wa fikra zetu kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.

  Vilevile tunahitaji SHERIA ambazo zinazingatia HAKI na USAWA.

  Haya ni machache tu!
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  tatizo letu ni kuwa naona kama hatutaki kuchukua responsibility yetu kuhusu hapo tulipofika. Kusema mtu fulani au kitu fulani ndicho kimetufikisha hapa haitoshi. Kama tunataka mabadiliko lazima tuwe sehemu ya mabadiliko hayo kwa vitendo. Tuanze pale tunapoweza na taratibu taratibu nguvu ya matendo yetu itasambaa maeneo mengi makubwa.
  Kwa ufupi, tuongee kidogo na tutende zaidi.
   
 10. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
Loading...