MpigaFilimbi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,169
- 182
Hivi , wadau Usalama wa Taifa bado upo?
Hicho kitu usalama wa Taifa hakipo kabisa Tanzania! Kwa mtazamo rahisi kabisa hawa walitakiwa kuwa watu wa kwanza kujua kuhusu lolote linalohatarisha usalama wa nchi, kiuchumi, kijamii na kwa namna yoyote. Walikuwa wapi wakati watu wanaiba tena kwa kufoji vielelezo, inawezekana deal zote hao jamaa ndio wanatumika kuzichonga. Madawa ya kulevya kila kona, tena watu wazito wanajihusisha nao, ufisadi ndio huo, bado tuamini tunaweza kulala tukiamini kuna usalama hapa? Ndio maana yule mshikaji akaamua hata aende Ikulu aibe ua, kwani nchi hii haina usalama wowote!!