Taifa lilipofikia: Wa kulaumiwa ni Rais au ni System? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa lilipofikia: Wa kulaumiwa ni Rais au ni System?

Discussion in 'Great Thinkers' started by DSN, Feb 24, 2012.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naomba kujua kupitia Jukwaa hivi hapa tulipofika Je wa kulaumiwa ni Rais au ni System [mfumo] wetu. Manake hapa Taifa lilipofika system [A system is a way of working, organizing, or doing something which follows a fixed plan or set of rules.People sometimes refer to the government or administration of a country as the system.] kwa maana tajwa hapo juu au vinginevyo najiuliza Je system ndio chanzo cha Taifa letu kufika hapa lilipo au Rais ndiye chanzo cha Taifa kuwa hivi lilivyo?.

  Binafsi ningepewa nafasi ya kujiuliza kama system yetu angekuwa ni mwanaume je ni mwanaume wa aina gani kulinganisha na mwanaume yeyote toka mataifa mengine kama Marekani au kwingineko tathimini yangu kama Mtanzania wa kawaida mwenye ufahamu wa mdogo wa kitanzania ingekuwa kama ifuatavyo.

  Mwanaume huyu Mtanzania mwenye familia yani Mama na watoto [Watanzania] na Mwanaume Mmarekani na familia yake [Wamarekani]

  Mwanaume huyu Mtanzania angekuwa ni msomi wa elimu ya ngazi ya chuo kikuu kwa maana ya graduate asiyependa swala lolote linalohusu ubunifu kwa familia yake anaeamini kwenye ubinafsi wa kuwa yeye ndiye mtu wa mwisho kwenye hatima ya mafanikio ya familia na kuwa mkewe na watoto wake hawajui lolote lile kuhusu maendeleo na mafanikio ya familia iko miokoni mwa mwanaume huyo anaeitwa Baba.Pamoja na Wanafamilia yani mama na watoto [Watanzania] kuwa na akili na ubunifu ambao kama ungepata support ya Baba ungeifikisha familia pazuri matokeo yake Baba ameukata ushirikianao huo na uwachukulia wanafamila wake hao hawana cha zaidi na kazi yao ni kutengewa chakula na mavazi hivyo wasihoji chochote kile na kwa lolote lile na hivyo kutengeneza piramid life style ya maisha ndani ya familia hiyo muhimu yenye kushindania uimara wake wa kuweza kuhimili kusimama imara na kustawi kama familia ya kimarekani.

  Mwanaume huyu hayuko tayari kujua vipaji na uwezo wa mkewe, watoto wake,na hata vimada wake au mwanafamilia [Ndugu] yake yeyote yule anaemzunguka,ambae kwa namna yeyote ile aweza kuwa msaada kwa familia kwa siku zijazo na kuwa kwa kuunda ushirika huo na familia wanatayarisha maisha bora na ya uhakika ya baadae ya familia na vizazi vyao vijavyo.Mwanaume huyu uamini yeye ni yeye na kuwa amesoma na hakuna mwenye ufahamu wa ziada kuhusu familia au chochote kuhusu familia yake yani Tanzania.

  Kwa ujuma mwanaume huyu ningemaliza kwa kusema ni mbinafsi, mwenye kuamini kwenye sifa ya ubabe,japo ni msomi alielimika lakini ni mpenda kukumbatia uzamani [Conservative-right wing] yani kiswahili ningesame umwinyi,aliebahatika kuachiwa urithi wa mali na Mungu akamjalia Mke mwema na Watoto [Watanzania] wenye akili sana japo azitumiwi, wasikivu, wapole, wavumilivu, wabunifu, wacheshi na wasiopenda fujo, ingawa ni wanaposhikwa koo wanakuwa wakolofi wasioweza kutabilika kwa matokeo yao.

  Lakini kwa familia ya mwanaume mmarekani ni msomi,mjanja, mbunifu,mwenye kutafuta kwa ajili ya familia yake yaani mke na wanae [Wamarekani] kwa njia yoyote ile hata kwa kuvunja na kuiba yuko tayari ili mradi familia yake ipate mafanikio na maisha yao yawe bora.Japo yeye mwenyewe ni msomi mzuri na mjanja na kaenda shule kisawasasa baadhi ya watoto wake hawana ufahamu wowote zadi ya Baba yao kuwa mtundu wa kuhakikisha wanae na mkewe wanamaisha na uhakika bora kwa mbinu zozote zile zitakazo anzishwa na yeye binafsi na kisha kuja kuwarithisha wanae na watoto kwa faida ya vizazi vyao.

  Naomba kujua kupitia wanajf ni Je ni kosa la Rais au ni kosa la system [mfumo] kwa hapa tulipofika kama Taifa ambalo Viongozi wana lalamika,wabunge,watawala ,wanataaaluma, wasomi, wanafunzi, raia, wafanyakazi, wakulima wote kwa umoja wanalalamika anaelalamikiwa ni nani Je ni Rais au ni System [Mfumo]?

  Nawasilisha.
   
 2. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ulaumiwe wewe kwa kutotimiza wajibu wako!
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Are you really a responsible citizen of this Country?
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo napotaka kujua je Taifa linaanzia kwa umma au Taifa linaanzia kwa kikundi cha watu wachache wenye dhamira ya dhati pasipo kupindisha jambo.Wajibu upi huo ambao wewe unataka utimizwe pasipo kujua wajibu wangu na nani wa kunielekeza wajibu huo na msimamizi wa mimi ni timize wajibu huo ni nani wa wajibu huo ni kwa faida ya nani.
   
 5. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  VGL ndio tena kwangu Tanzania kwanza,jadili mada uraia unahusika nini hapa.Tunatafuta kujadiliana tupeane ufahamu na kisha kutoka hapo kuna wengine tutaondoka na ufahamu na kesho na keshokutwa jamvi linabaki na kumbukumbu ambayo wengine watajifunza na pengine kufanyia kazi.Usije ukawa sawa na baadhi ya watendaji mwanaume baadhi ambao hawataki haya usiyotaka kusikia hatimae tunakuwa watu wa kulalamika daima kumbe ubaya tunao wenyewe.Jadili kwa hoja acha ideology za kizamani,jadili kujenga Nchi uisiishi ndani ya Box think outside the Box kwa faida ya Taifa.
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Wa kulaumiwa ni CCM!!
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu how?Manake CCM kama CCM ni chama kama Chadema na na kuwa kina katiba na ilani zake,Je ni sahihi kulaumu chama au kulaumu Watendaji wa Chama.Manake kuna kama mchezo kalianzishwa na wajanja kaliko tushape Watanzania kuwa na tabia ya kulaumu ujumla wa kitu kuliko muhusika wa kitu.Yani kama wewe unavyosema tulaumu CCM kumbe tulipaswa kulamu watendaji wa chama tena ikibidi kila mmoja mmoja,kwa kuwa kwa tabia yetu ya kulaumu kwa ujumla kama unavyosema CCM matokeo yake hakuna anaewajibika [Responsible].

  Lakini tungekuwa kila lolote linaloharibika anashikiwa kidedea muhusika yeyote yule mwenye dhamana ya eneo husika na kutoa majibu yaliyo sahihi na yenye kuridhia mizani ya maono ya wananchi wahusika basi kila jambo lingekuwa na utatuzi na si misamiati tata tuliyozoea.Wenzetu waliotabngulia daima wana wajibika kwa kuahakiksha chochote kinapo kwenda kombo kuna mtu yupo kujibu kwanini jambo hilo limeenda kombo kwa kuwa dhamana ya kitu hicho kilikuwa mikononi hivyo mizani ya umma ikiona anawajibu wa kujibu basi anawajibika yeye kama yeye na si Taasisi.
   
 8. M

  MWananyati Senior Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa uelewa wangu mdogo, taifa lolote lile linaongozwa na system. hio system ndio inayoseti vision ya serikali inayokuwa madarakani. Hii system ndo inayotoa mwongozo kwa serikali katika utekelezaji wa majukumu yake kitaifa na kimataifa. Na hii system haifungamani na siasa za chama kinachotawala, na pia chama tawala huwa hakina mamlaka juu ya system. System inakuwepo for the interest of a state politically, economically, socially and religious-wise.

  Chama kinachotawala kinakua na ilani yake, lakini haiwezi kupingana na vipaumbele vya taifa ambavyo vinasimamiwa na system. Hiki chama kitafanya usanii wake katika mambo ambayo system inaona haitaathiri usalama wa taifa na maendeleo yake.

  Mfano. kila jambo ambalo rais wa USA anafanya ni maelekezo ya system ambayo inahakikisha national interests are safeguarded at any cost. Kwa hio usishangae masuala haya ya vita ambavyo USA imekua inavianzisha kuwa ni mipango ya muda mrefu ya system ambayo rais yeyote toka democrat au republican atatakiwa kuitekeleza na pia atafanya justification kwa umma ya matendo ya serikali (sio system)yake.

  Kwa yanayoendela hapa kwetu ni kuwa system has been weakened kwa kuruhusu wanasiasa kuwa part of the system. Wanasiasa wanakua wanaelewa system imepanga kufanya nini wakati gani. Hizi stratgy zinavorugwa kabisa mapema na huwa hazifanikiwi sababu zinavuja, na mara nyingine zinaanzwa kupingwa hadharani na wanasiasa wenyewe na hatimae zinakua abortive.

  Na wale waliozishika hizi system kwa sasa sio watu makini sababu wenyewe wana maslahi katika political arena. Normally, wana-system huwa wanatakiwa kujitenga na siasa za vyama. Lakini kwa sasa system iko porous, na ndo wapo mbele katika siasa.

  Usalama wa nchi yetu upo hatarini klwa hali hii. Kinachotakiwa ni general overhaul of the system so as to restore the lost national pride. Na njia pekee ni through assassination.

  TK
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  wananchi ndo wakulaumiwa.
   
 10. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  kila mtu anapaswa kulaumiwa system nzima mbovu,kwa maana ya serikali na taasisi zake, raisi kwa kutoongoza vizuri na kureshape system in way system ifanye vizuri na wananchi kwa kutowajibisha wanaolipeleka taifa hapa tulipo. kama system ipo mbovu basi wananchi wanapaswa kuact on the situation sisi kama wananchi tupo tupo tu.
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mimi ningependa ku take a different perspective. Wengi mme point nani wa kulaumiwa, mimi ningependa twende mbele zaidi, maana tukibali kulaumiana hatutafika kokote.

  High developed societies have morals, ethics and positive thinking. Do we have positive thinking in Tanzania?

  The answer is no. Jana nimeambiwa story ya watu wanaovamia mabweni na kuibia wanafunzi. Acha wanaokaba mitaani, wanaopora watu magari yakipata ajali. watu wanakata mabomba ya maji njia ya chalinze to segera? Wengine wanakula cha juu kwenye tender kama za Richmond. why? nani wa kulaumiwa? The social fabrics which hold society together are on the verge of collapsing.

  What is the Problems? Our mind. we think negatively. Kwa wengi wetu, wizi, utepeli umekuwa ni njia ya maisha. Mtu anayefanya kazi serikali na kustaafu bila kuiba anaonekana ni mjinga!

  what is the cause? Colonial mentality? Colonial hang over? Eevn after 50 years of independence, do we still have a colonial hangover? Kushindwa kuthamini mali ya uma? Is this the reason why Rev Mtikila said that we Tanzanians need mental emancipation?

  Tunahitaji kubadilika mtazamo wenu wa maisha/ Maendeleo. Tuache kutegemea serikali kufanya kila kitu. Tujitoe kufanya kazi kwa bidii.

  On the other hand, tunahitaji demokrasia na namna gani? Tumekuwa na demokrasia kwa miaka 50 ya Uhuru na ndio imetufikisha hapa, je tuendeleee vipi? Sometimes, unaweza kuona kwamba labda tunahitaji a strong man ambaye atarudisha nchi kwenye mstari. watanzania tunahitaji mtu strong, wa kutufokea, na kuturudisha kwenye mstari. Mtu atakayefanya system zifanye kazi inavyotakiwa, zenyewe bila kusimamiwa. Tuache kutafuta mchawi.

  Shida ni kwamba, kwa hali ya sasa, sio rahisi kumpata mtu kama huyo.
  Lakini hiyo ingeweza kuturudisha kwenye mstari.
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Na hii ni kwa sababu hatujazoea struggle za aina yoyote. Uhuru tumepewa bure na bada ya hapo serikali ilitoa almost kila kitu bure. Mawazo yameshindwa kubadilika. Bado tunategemea serikali ifanye kila kitu. serikali ikisinzia, wote tunalala.
   
 13. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wakuu kwa uelewa wangu Bila kusita nasema ni rais kwani:
  . Yeye ndiye tuliyempigia kura
  . Yeye ndiye anayeongoza vita ya kumkomboa mtanzania na hivyo anapoingia madarakani anatakiwa aipime system iliyo na machinery zote kama zinamsaidia katika azma yake hiyo mikakati ni kuziimarisha vinginevyo mkakati ni kuvibadili. Assumption ni kuwa wakati anaomba urais amekwisha utafiti wa kutosha na kuona jinsi ilani yake itakavyofit ktk current system laa sivyo pia akaona atakavyoweza kuishape iwe ya msaada na sio kikwazo katika utekelezaji wake wa ilani yake na chama chake.

  Nikichukulia case ya Tanzania rais ambaye pia ni amiri jeshi na mteuzi wa wateule wa ngazi zote za juu wakiwepo majaji, mawaziri, wabunge kumi, ma RC, maDC, maRAS, maDAS, wakurugenzi wa halmashauri zote, Wenyeviti wa board na tume zote muhimu, IGP, CDF,n.k. ambao hawa ni ujumla wao wachangia kwa kiasi kikubwa mwelekeo na function ya system. Lazima alijua wazi system iliyokuwepo na ameendelea nayo hadi leo (7 down the road)assumption ni kwamba kilichopo leo in terms of system it is very much his or a result of his work. Ndiyo maana sioni mantiki ya kuilamu system

  Wakuu nawasilisha
   
Loading...