Taifa libadilishe fikra la sivyo meli inazama wa wasomi wakiwemo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa libadilishe fikra la sivyo meli inazama wa wasomi wakiwemo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by peter tumaini, Feb 3, 2012.

 1. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari watanzania,

  napenda nitoe changamoto kwa taifa letu linavyoyumba kwa kukosa mwelekeo nikikazia katika suala la kilimo kwanza;Taasisi kama SUMA JKT wamenunua matrekta na wamejaribu kuuza kwa bei kubwa soko gumu na kuamua kupunguza bei ili kupata wateja na pia wakulima hawakopesheki hawana dhamana je lipi la maana kuacha matrekta yakae yard yakisubiri wanunuzi au wapewe wakulima kwa mikataba maalum ili waboreshe uzalishaji ili kusaidia kupunguza hata inflation.Naamini mmiliki ni chombo cha serikali hata kama wamepata kwa mkopo mwisho wa siku pesa ya mvuja jasho itatumika kulipa. wasomi wetu wa kilimo ni muda sasa wa kujitokeza na kuweka mipango inayokubalika kunusuru hii meli inayoelekea kwenye mwamba.tatizo langu huenda tukaangamia huku tiba ikijulikana.
  LETA SULUHISHO KWA KUCHANGIA HOJA.
  NAWAKILISHA KWENU

  By Peter.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa la Tanzania sio plans pekee bali ni mfumo. Hakuna maendeleo ya maana yatapatikana Tanzania kama Watanzania hwata jibu hili swali hapa chini. Cha kushangaza hata hapa wanajamii bado wako nyuma kidogo kwenye hili swala muhimu.

  Swali: Je Watanzania wanataka kazi ya serikali iwe ni nini??. Je ni vitu gani hasa tunataka serikali ifanye na vitu gani tunataka serikali isifanye?. Majibu yatatofautiana lakini bila jibu hapa Tanzania itakuwa inapiga danadana tu.

  Mfano katiba ya USA inasema: Serikali inatakiwa kufanya vitu ambavyo wananchi hawawezi kufanya wenyewe.

  Serikali na hata wananchi wa Tanzania hawajajibu hili swali bado. Hivyo serikali inafanya mambo mengi ambayo kwa mawazo yangu si kazi ya serikali? Mfano ununuzi wa matrekta ungeweza kufanywa na mashirika binafsi kama TFA, ATC, Tanesco, Afya n.k
   
Loading...