Taifa letu linaharibiwa na watoto wa vigogo wa CCM waliorithiswa madaraka na wazazi wao. Tabia za kulifanya taifa letu la kisulutani inatugharimu

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Kasumba ya chama cha CCM kuwarithisha madaraka watoto wa viongozi inaligharimu taifa letu.

Yawezekana huko nyuma wazazi wao walikuwa na uzalendo wa kweli lakini hawa watoto baada ya kuona kuwa siasa inalipa hasa baada ya CCM kuingiwa na na kubadilika kukumbatia ufisadi wazazi wao wakawalithisha wawe viongozi.

CCM ya leo imetuletea viongozi wabaya na wasiofaa kabisa ambao wao kujaza matumbo yao ni kipaumbele kuliko maslahi ya taifa letu.

Mfano ni January Makamba na Nape Nauye hawa vijana hawafai kuwa viongozi bali warithishwa na sasa ni mwiba kwa taifa.

Usulutani wa CCM unaligharimu taifa letu.
 
Yaani ww ni kama wale walio rithishwa madaraka,, hakuna chochote mnachokifanya zaidi ya matumbo yenu na mapambio mtafikiri hii nchi ni ya kwenu na ndugu zenu, Hamna dira yoyote kwa nchi hii!!!
Hata chadema asili wanataka chama kitoke kwenye mikono ya ukoo!
 
Acha ubaguzi wewe mleta mada. Kwahiyo kuwa mtoto wa kigogo hastahili ajira? Mimi sioni huo upendeleo bali ni hurka ya watoto wengi kupenda career za wazazi wao.
 
Ccm kwa ujumla wake ni saratani kwa nchi hii. Kwasasa ccm imeshajua haina ushawishi kwa umma, hivyo imetengeneza uhusiano wa kihalifu na vyombo vya dola ili kupora chaguzi za nchi hii, kisha wakiingia madarakani wanaachiana mazingira ya kupora nchi.
sumba ya chama cha CCM kuwarithisha madaraka watoto wa viongozi inaligharimu taifa letu...
 
Binafsi sioni shida kuongozwa na watoto wa viongozi walioandaliwa vema! Ila kupata viongozi kwa kukurupuka ni mbaya zaidi, kama JPM tulikurupuka, hata mwenyewe hakutgemea kufika pale, kuna wenye ndoto kufika hapo, kuna baadhi ya vijana kama 7ya, Bashite.

Hawakuandaliwa na hawakutegemea kufikia pale, ila kwa Nape, January, Makamba sehemu kubwa watu wanawachukia kwa kuwahofia, ila ni vijana walioandaliwa kuwa Marais hawawezi kutuaibisha, hawawezi kuwa washamba, si rahisi kuwa na vikosi vya kijambazi, mfano mzuri Uhuru Kenyatta!
 
Back
Top Bottom