Taifa lenye wabinafsi wengi zaidi duniani

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
Imechapishwa: Mon, Jul 4th, 2016



Kwa mujibu wa watafiti mmoja, Waingereza “…ndio watu wenye ubinafsi zaidi duniani, ndiyo jamii inayokazia zaidi faida za kibinafsi kuliko watu wa nchi nyingine yoyote duniani,” likaripoti gazeti Daily Telegraph la London, Uingereza.

Uchunguzi mwingine ulionyesha kwamba Waingereza wanapatwa na huzuni na mifadhaiko kuliko raia wa taifa jingine lolote duniani. Wataalamu fulani wanaamini kwamba mambo hayo mawili—ubinafsi na huzuni—yanahusiana.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Northwestern kilichoko Chicago, Marekani, ulilinganisha jamii mbalimbali duniani, kama zile zinazopatikana katika nchi za Ulaya, na zile za China na Taiwan.

Ilionekana kwamba kwa kuwa jamii za China na Taiwan zinathamini zaidi ushirikiano katika jamii badala ya ubinafsi, watu wanalindwa wasipatwe na matatizo ya kiakili.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mwanasaikolojia wa Uholanzi, Geert Hofstede, imegundulika kuwa katika nchi zilizo na jamii zenye watu wabinafsi zaidi, Uingereza ilishika namba moja katika orodha, ikifuatiwa na Marekani, Australia na nchi nyingine za Magharibi.

Katika nchi za Ulaya, “jamii yenye ubinafsi … inatufanya tuhuzunike,” linasema gazeti Telegraph.

Hata hivyo, kiwango cha huzuni na mfadhaiko katika jamii hizo ni cha juu sana kuliko mahali pengine popote duniani, kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uliojulikana kama ‘Depression: A Global Public Health Concern’.

“Tumegundua uhusiano wa ajabu sana kati ya ubinafsi, huzuni na mfadhaiko,” anasema Dk. Joan Chiao, mwandishi wa taarifa ya utafiti huo, na kuongeza, “Mataifa yenye watu walio na ubinafsi zaidi wameonyesha kiwango cha juu sana cha huzuni na mfadhaiko.”

“Kiasi cha mmoja kati ya watu 10 nchini Uingereza anateswa na ama huzuni au mfadhaiko ikilinganishwa na mmoja kati ya watu 12 katika Bara la Ulaya,” likaandika gazeti Telegraph na kuongeza hivi: “Inakadiriwa kuwa kiwango cha mfadhaiko na huzuni nchini China ni kiasi cha mmoja kati ya watu 25.”
 
Back
Top Bottom