Taifa la watu wajinga likikosa au likifichwa taarifa/habari, hugeuka kuwa taifa la watu wapumbavu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Kabla sijaandika lolote kuhusiana na hii mada, niseme tu tuvumiliane kwa matumizi ya neno "wapumbavu " kwani hilo si tusi na hata Baba wa Taifa alikuwa akilitumia inapobidi.

Tukirudi kwenye mada, kuna Taifa fulani huko kusini mwa bara la Afrika limedhihirisha pasipo shaka kuwa, watu wajinga wakikosa au kunyimwa taarifa, watu hao hugeuka wapumbavu.

Hii ni kwasababu, katika Taifa hilo alitokea mtawala mmoja alieminya uhuru wa habari na kuhakikisha propaganda za kumtukuza ndio zinapewa nafasi katika media, matokeo yake baadhi ya raia wamekuwa wapumbavu kwa kuamini kiongozi huyo katika utawala wake, hapakuwa na wizi wala ufisadi na kama uliotokea, basi yeye hakuhusika.

Wapumbavu hawa wanalinganisha awamu zilizopita na hiyo awamu wanasahau (kwasababu ni wajinga) kuwa awamu zilizopita ziliacha media na hata Bunge lifanye kazi yake ndio maana maovu na madudu katika awamu hizo yalijulikana kwa umma.

Pia, wajinga hawa ambao sasa wamegeuka wapumbavu, wanasahau katika awamu ziliotangulia, hata whistleblowers walikuwa na nafasi Bungeni, kwenye Media na hata kwenye majukwa mbalimbali yawe ya kisiasa au vinginevyo.

Wajinga hawa walio-gradute na kuwa wapumbavu, walifikia hatua ya kushangilia kila aina ya mradi bila hata kujiuliza kwanza mikataba inayosimamia miradi hiyo ina nini ndani yake, wao wanachofurahia ni kuona structures zinasimama na vitu vinanunuliwa wakiamini hayo ndio maendeleo.

Wapumbavu hawa pia wanasahau mtu pekee aliekuwa akiibua tuhuma za wizi na ufisadi alikuwa ni Mkaaguzi na Mdhibiti Mkuu wa fedha za umma katika nchi hiyo, mtu ambae, hata hivyo, nae alifanyiwa zengwe na kuondolewa katika nafasi yake ili wahusika waendelee kula bila kunyooshewa vidole.

Tunajua kuna baadhi walikuwa ni wanufaika wa moja kwa moja wa utawala huo, hivyo hawa wamejitoa akili kutetea kila jambo hata kama ni baya, ila wapo wengine ni kwasababu tu walifichwa yaliyokuwa yanaendelea sasa wametoka kuwa wajinga na wame-graduate na kuwa wapumbavu. Inasikitisha.

Kweli nimeamini "information is power ."
 
Niseme taifa hili linaharibiwa na wasomi. Wasomi ndiyo wapumbavu. Wasomi hawajui kusimamia ukweli. Leo unakuta mtu anasema zuia sukari tujenge viwanda then mwingine anakuja kusema nonsense agiza tu sukari toka nje hata kama viwanda vya ndani vife. Hakika kuna kizazi mpaka kife chote ndiyo tutapata maendeleo. Na hicho ni kizazi cha michwa na wachumia tumbo kinachoamini ktk mtandao na siyo Tanzania na wananchi wa kawaida.
 
Daah kweli aisee Zilankende ameliharibu kabisa taifa, wajinga wameongezeka kwa kiasi kikubwa mnoo.

Kuna mimtu ina amini kuongozwa kwa kukandamizwa, kunyanyaswa na kudhalilishwa ndio kuongozwa vizuri shame on them.

Huu ulikuwa utawala wa zama za mawe za kale, katka karne hii ya 21 ya sayansi na technologia watu wanajiongoza wenyewe tu sababu wote wanajielewa kiongozi mkuu wa nchi anakuwa kama icon tu taifa na kufuata sheria za nchi basi.

Mkuu wa nchi sio Mungu,kwamba hapigwi or hakosolewi, hata katika nchi za kifalme mambo hayako hivyo pia.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom