Taifa la Wale Waliwao, Wakila, Wakilia na Kulilia huku wakiliwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa la Wale Waliwao, Wakila, Wakilia na Kulilia huku wakiliwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 22, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Lipo taifa – sitolitaja – ambapo watu wake huliwa huku wanalia na wale wanaowala nao wanaliwa huku wakilia na kuliliana huku na wao wenyewe wakililiwa. Taifa hili - ambalo sitolitaja – linaongozwa na watu wanaopenda kula sana. Wanakula kila kilichopo mbele yao na wanakula kama wasiojua kushiba. Wanakula hadi vya watoto! Wanakula huku hakuna wa kuwauliza kwani hata wale ambao wanapaswa kuwauliza na wenyewe wanapiga mahesabu ya jinsi gani wataingia mezani nao kula! Ni taifa la walao na wale waliwao!  Mtu yeyote anapotembelea taifa hili - nisilolitaja – anaweza kuona mara moja tofauti kati ya wale wanaokula, wanaoliwa, wanaotaka kula na wale wanaolilia kutaka kula – au wanalia wakiliwaau vya kwao vikichukuliwa kuliwa. Wapo ambao – kwenye hili taifa lisilo na jina - wameshikilia masufuria na mabakuli makubwa ya kula wakilia kwa sauti za kukoroma (zenye mikwaruzo ya kuudhi) “ongeza ongeza!” wakiwalilia watu wasio na uwezo wa kuwapa cha nyongeza. Wafanyakazi na wakulima katika taifa hili wanaambiwa – tena kwa kupigiwa kelele – “fanyeni kazi kwa bidii na maarifa” ili pato liongezeke.


  Wasichoambiwa maskini hawa wa Mungu ni kuwa wanaaambiwa waongeze uzalishaji ili mabakuli ya walaji yazidi kuongezewa. Songombingo huja pale maskini hawa wenye kuliwa wanapoamua siku moja na wao waamue kudai nyongeza kidogo ya kula – hata kama ni tumifupamifupa. Walaji wakubwa huja juu; wanang’aka na wakati mwingine na vitisho! Nilisimuliwa kisa kilichotokea kwenye hiyo nchi – nisiyoitaja – pale kundi moja la walaji wadogo wadogo lilipojaribu siku moja kutishia kuacha kuwapikia walaji wakubwa!


  Msimamizi mkuu wa walaji wakubwa alichukizwa sana na aliamua kuwapiga mkwara hadharani wale walaji wadogo na kuwaambia wasikubali kutumiwa na watu wabaya hata wakafika mahali wakakataa kuwapikia walaji wakubwa. Katika mkutano wake na Wazee wa Walaji Mlaji yule mkubwa alizungumza kwa hasira sana na kuwaambia kuwa wakiendelea kutishia maslahi ya walaji watapigwa virungu. Maskini wa Mungu wale wapishi wakuu walibakia wanatetemeka hasa walipokumbushwa kisa cha ndege fulani, kisa ambacho kwa kweli kiliwalazimisha kufikiria mara mbili.


  Walaji wakubwa waliendelea kula na kutafuna huku wakicheua mafuta; wakikumbatiana na kupongezana huku wakifanya mpango mwingine wa kujiongezea kula zaidi. Kilichowatibua wanaoliwa zaidi ni siku ile ambapo walaji wakubwa walipoamua kujiongezea ulaji zaidi huku wakiwaambia wananchi wa taifa lile – nisilolitaja – kuwa taifa lao liko kwenye hali mbaya ya uchumi. Wakaamua kujiongezea ulaji huku wakitetea kuwa walaji wote wakuu wamekubaliana kula!


  Ndipo kundi jingine la watengeneza chakula cha walaji wakubwa lilipoamua na lenyewe kuomba kidogo liongezewe kwenye sinia lao la ulaji. Ndugu zangu hawa walikataliwa kwa mbinde na upinde, kejeli na dharau. Lilikuwa kosa ambalo walaji wakuu hawalikutarajia. Kwani wanaohudumia walaji wakubwa wakaamuka kugoma! Kama utani hivi. Walaji wakuu walikuwa na uhakika wa kutosha tu kuwa walaji hawa wadogo hawana umoja na hawawezi kusimamia mgomo kwa muda mrefu. Oh, walijikuta wanashangazwa pale abapo walaji wale walipong’ang’ana wakang’ang’ania!


  Ndipo mmoja walaji wakubwa alipojitokeza kwenye luninga akiwa amekasirika, na akiwa amezungukwa na walaji wengine mahiri wote wakiwa na nia moja kuwalazimisha wapishi warudi jikoni! “Msiporudi kutupikia mtajifukuzisha kazi” alitamka mlaji mkuu msaidizi. Kesho yake hakuna aliyerudia! Mambo yalianza kuwa mabaya kwenye taifa la lile nisilolitaja.


  Waliokuwa wanaliwa sana na ambao walijikuta wanazidi kulia wakati mgomo ukiendelea walipoamua kufanya kweli. Wakajitokeza na kuandaa umati kuwapinga walaji wakubwa! Wakubwa wakashtuka kwani hilo hawakulitarajia. Walitarajia kuwa wakipiga mkwara, mabomu na vitisho basi wanaoliwa watanyamaza - kwani kwenye taifa lile mikwara hufanya kazi sana. Huku nyuma mlaji mkubwa akisema kitu basi watu hufyata mkia. Haikuwa hivyo safari hii. Wanaoliwa hawakuwa tayari kukaa kimya; waliamua kubanana na watawala wao kwenye taifa hili nisilolitaja.


  Mambo yalipozidi kuwa magumu na wanaoliwa zaidi walipozidi kulia na kuanza kupiga mayowe ndipo walaji wakubwa walijikuta hawana jinsi bali kukaa na wapishi wao kujaribu kutafuta suluhu. Wakakubali kuwaongezea kidogo kwenye masinia yao. Lakini hawakuwa tayari kuwanyanganya ulaji walaji wenzao wakubwa! Na uwezekano wa walaji wale wakubwa waliosababisha tafruku hiyo kuhamia na kupelekwa kwingine kula ni mkubwa kwani kwenye taifa la walaji hakuna anayenyang’anywa sahani! Wanahemishwa meza au viti! Ukihamishwa meza unaweza kupelekwa kwenye kula kwa kunyemelea lakini ukihamishwa kitu umehamishwa mkao wa kula tu! Kula kunaendelea!


  Ni mpaka pale wale waliwao watakapoamua kukataa kuwa sababu ya kula kwa wale walao ndipo mabadiliko ya kweli yanaweza kuanza kutokea. Vijana wanaojitahidi kila siku kufanya kazi watakapokataa kuwa sehemu ya mfumo wa kuliwa ambao wenye kula hula wakirithisha hadi watoto wao kula; watakapokataa kuwa watetezi wa mfumo huo wa ulaji ndipo vijana wa taifa hilo – ambalo sijalitaja – watakapoanza kutafuta sehemu yao katika maisha ya nchi yao.  Walaji watakapokataliwa kula au kujiongezea vya kula ndipo wale wanaoliwa nao watapata nafasi ya kutafuta chakula! Nje ya hapo, walaji wakubwa, watetezi wa walaji na chama chao kikuu chao ulaji wataendelea kula bila kuulizwa huku mamilioni ya wananchi wenzao wakiendelea kubakia kunawa mikono na kuitwa kuja kutoa vyombo! Wale wengine ambao wamegundua kuwa nje ya chama cha walaji hakuna nafasi wanajikuta wanaamua kuanza kuimba wimbo wa kusifia walaji ili na wao hata kama hawatakula sana wawekwe mahali ambapo wanaweza kuambulia makombo! Kumbuka, makombo ya walaji wakubwa ni chakula tosha kwa maskini mwombaji!


  Aliyeko kwenye taifa lile nisilolitaja!
  Nitafute: Facebook “Mimi Mwanakijiji”

  Twitter: “mwanakijiji”
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Nimeona umepost facebook.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pumba ndeeefu hazina kichwa wala miguu.

  Zamani ilikuwa kula na kulipa, siku hizi kula uliwe. Jee, wewe huko uliko unakula bila kuliwa?
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Ashakum sii matusi....Haya matusi makubwa kusema watu wanaliwa huku wakililia na wao pia wakiliwa huku wakililiwa..tumekuwa taifa la mashoga basi..Kumradhini!
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwakijiji nakuunga mkono as long as hiyo ni hadithi tuu, ukweli halisi kwa taifa ninalolijua mimi ni kuwa kuna makundi matatu,
  1. Wala Nchi- ni wale ambao kazi yao ni kula.
  2. Wenye nchi- ni wale ambao hijisikia nchi ni mali yao.
  3. Wananchi ambao hawa ni walala hoi, na ni masikini wa kutupwa. Kundi hili huishi kama wapangaji kwa wenye nchi kuzidi kuwaneemesha wala nchi!.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Umesahau Manyapala, wale wanaochunga na kulinda kati ya wenye mali, walaji na wapangaji..
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,817
  Likes Received: 36,921
  Trophy Points: 280

  mbona kama kuna minajiri ya jazba hapa??
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 9. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nchi hiyo ambayo mtoto wa wale ambao si walaji akijaribu kutia mkono kwenye bakuli la walaji anashikwa mkono unalambwa na kusuguliwa kwenye mchanga asirudie tena kujaribu kuingiza mkono wake kwenye bakuli la walaji. La halaula. laana tupu. Lakini watakula watavimbiwa wataishia kujamba (ashakum si matusi) tu.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kama hakuna umaskini na utajiri utapimaje maendeleo?
  Kama hakuna wanokula yanini kuwa na midomo?
  Kama hakuna wasokula ya nini kuwa na nderemo?
  Kama hutaki kuliwa kwanini wewe wala?
  Asie kula kalala seuse anaeliwa?
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  UDADISI: Rethinking in Action: chakula
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kuwa wanaokula kwa kweli hawana wasiwasi kabisa wa kuwa na njaa!
   
 13. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Great thinker at work.......:A S 465:
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Mkandara, manyapala ni sehemu ya wenye nchi, wengi wao wakishatumika vya kutosha hugeuka walanchi na wengine huishia kuwa makapi tuu na kugeuka wananchi wa kawaida, kama ilivyo kwa baadhi ya wenye nchi ndio hao wala nchi kwa mtindo wa kikulacho!.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  I am reading Cry Havoc book by Simon Mann and this is what Simon Mann says in one of his many statements which undermine our African leadership.......
  "Setting up the right businesses in Africa takes you to the right people. It is what we called Bongonomics, in dubious honor of the late and unlamented leader of Gabon, President Omar Bongo. African politicians love foreign investors. Get to the politicians and you quickly get the top humbre. Once you are with the number one, then the treasure box flies open".

  Hakuna la ziada la kuongeza, sisi tuendeleee kuliwa tu maana wathungu wanaijua winning formula ya kuila Africa na wanaitumia ipasavyo.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Unalitambuaje Taifa la aina hiyo? Waliwao na wanaowala wanatofautiana vipi?
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  angalia meno yao (yana mabaki kiasi gani) na jinsi wanavyocheua au kupiga mihayo!
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na wanaoliwa wana wasiwasi wanini? kuliwa?
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna formula yake niliiona humu JF inakuwa hivi, 83 + 17 = 100

  17 wanaokula, 83 wanaoliwa.
   
 20. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  aaaagh! Mi nilifikiri ni Richard Mabala(kumbe mwanakijiji), unaaaaandiiiika mpaka basiiii ! Tunga vitabu basi ! Sometime una bore.
   
Loading...