Taifa la wadokozi, wezi, wasaliti, wazushi, waongo kamwe haliwezi kusonga mbele kwa kauli za big res

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
TAIFA LA WADOKOZI, WEZI, WASALITI, WAZUSHI, WAONGO KAMWE HALIWEZI KUSONGA MBELE KWA KAULI ZA BIG RESULT NOW!

Taifa letu sasa linatimiza miaka 52, ni miaka mingi na michache kulingana na mitazamo na maoni ya watu. Wapo watu wanaofikiri nchi kuendelea inahitajii miaka zaidi ya hamsini nayo kwao ni kigezo cha taifa kuendelea au Kwa maana ya kuwa na wataalamu wa kutosha waliozalishwa kipindi hicho chote cha miaka takribani 50, sasa mimi najiuliza kuwa inachukua miaka mingapi kuzalisha wataalamu hao? Kwani miaka 50 kama unazalisha wataalamu sasa WATAALAMU hao watakuwa wameeanza kukidhi vigezo vya kustaafu kwa hiari, na wengine wakijiandaa kustaafu kwa kisheria.

Taifa hili ni moja kati ya mataifa yanayoendelea ambayo yamesomesha watu wake ndani na nje ya nchi vya kutosha! Lakini wataalamu hao baadhi wapo ndani ya nchi , WAMEHATAMIA, WAMEHODHI madaraka ya kisiasa ndani ya serikali na chama, wameacha kabisa taaluma zao sasaivi wanakazi moja tu kubuni kauli mbiu za serikali zinazo pumbaza wananchi kwa misamiati, kutoa propaganda za enzi ya UGININGI, mara utasikia wakisema SERIKALI YETU SIKIVU, TUPO KWENYE MCHAKATO, SERIKALI IMELIONA HILO, TUMEFANYA UPEMBUZI YAKINIFU, UCHUMI WA TAIFA LETU UNAKUWA KWA KASI 7%, TAIFA LITAENDELEA KUJENGEA UWEZO WANANCHI ILI WAWEZE KUMILIKI UCHUMI WA KISASA KWA AJILI YA SOKO LA USHINDANI, MKUKUTA, MKURABITA, BIG RESULT NOW n.k.
Wamekuwa wakibuni kila uchwao maneno mazuri yenye kuvutia umma wa Watanzania na yenye lengo la kupumbaza fikra angavu yenye kujenga taifa lenye uchumi shirikishi zidi ya maneno YASIYOTEKELEZEKA. Mfano katika project ya KILIMO KWANZA inatumia mabilioni ya fedha ya walipa kodi, lakini wanaonufaika zaidi na mpango huu ni watu wachache na nitaeleza, mikoa inayopata ruzuku ya pembe jeo za kilimo asilimia kubwa ni WABUNGE, WENYEVITI WA HALMASHAURI za vijiji. MADIWANI, MAAFISA WATENDAJI WA NGAZI ZA VIJIJI jamaa zao na ndugu zao. Malalamiko haya si yangu ni ya wananchi na baadhi ya wabunge wamekuwa wakisikika! Lakini matarajio ya KILIMO KWANZA kitakwimu hazieleweki kwani pamoja na nchi hii kulishwa na wakulima wa jembe la mkono kwa miaka yote lakini Maisha ya wakulima hayabadiliki Kama yanavyoripotiwa na serikali.
Kwani hata tani hizo chache za KILIMO cha mkono bado wakulima wanalilia soko hakuna!! Hakuna kitu ambacho kimekuwa kikifanywa kwa utaratibu unaoeleweka vikaleta tija mipango yetu imekuwa ni ya KIMASLAHI ya watunga sera na watekelezaji.
Zahanati inawezwa kujengwa kwa milioni 15, Waziri akakodi ndege ya kumpeleka na kumrudisha bado na gari likatoka dar mpaka mkoani likachoma mafuta na posho ya dereva ika-gharimu milioni 25! Kuzindua zahanati ya milioni 15!! Achia mbali posho za kwaya, ngoma, ngonjera na msafara unaozidi magari 20.

Nchi Kama Rwanda imepiga hatua kubwa licha ya kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, wameweza kujisahihisha wakajifunga mkanda na leo ni taifa la tofauti kabisa wao hawakuchukua miaka 50, japo wapo watu watasema Rwanda wanachota, wanaiba madini uko Kivu ya Kongo, sawa na sisi wenye madini yetu wenyewe, gesi, uranium, chuma, makaa ya mawe, misitu, hifadhi ya wanyama, mlima K'njaro, bandari, maziwa na bahari?
Au tunahitaji KIONGOZI ambaye ataiongoza nchi kwa mkono wa chuma? Kama Hitler, MOBUTU, LENIN? Tumekuwa na mipango madhubuti, mizuri, vipaumbele vya taifa lakini tunakwama kwenye kutengea bajeti, na hata ikitengewa bajeti pesa haifiki Kama ilivyokusudiwa. Pesa zinatafunwa na watu hawachukuliwi hatua za kinidhamu stahiki. Wakati mwingine asilimia kumi tu au chini ya asilimia 20 ndo zinakwenda kwenye mradi na bado ichakachuliwe!. Tumekuwa na ugonjwa wa WIZI NA UDOKOZI kuanzia kwa viongozi mpka kwa Watendaji.


MWISHO, Taifa hili linahitaji mabadiliko makubwa katika mifumo ya kitaasisi Ili
1. iweze kuwajibika kwa UMMA
2. Kuwepo kwa uwazi na ukweli
3. Utawala wa sheria
 
wewe sio msomi? kama ni msomi utuambie unafanyia sekta ipi tuje kuiga kwako hayo uliyoyaandika. Tatizo kubwa wasomi wengi WATAIFA hili ni matapeli wakubwa. Hawa wanasiasa wanafundishwa kuiba na ninyi mnaojiita WASOMI, mnajilipa mishahara mikubwa ili kujiweka tofauti, mnajilipa posho kubwa ili kuwahonga vimada vyenu. HALAFU UNAKUJA NA POROJO ZA ETI SERIKALI. SERIKALI NI WATU KAMA WEWE UMEPEWA MADARAKA BAADA YA KUSHIBA UNAKUJA NA HOJA ZA UPUMBAVU HAPA.YAANI NINYI WASOMI MANAKERA SANA.
 
wewe sio msomi? kama ni msomi utuambie unafanyia sekta ipi tuje kuiga kwako hayo uliyoyaandika. Tatizo kubwa wasomi wengi WATAIFA hili ni matapeli wakubwa. Hawa wanasiasa wanafundishwa kuiba na ninyi mnaojiita WASOMI, mnajilipa mishahara mikubwa ili kujiweka tofauti, mnajilipa posho kubwa ili kuwahonga vimada vyenu. HALAFU UNAKUJA NA POROJO ZA ETI SERIKALI. SERIKALI NI WATU KAMA WEWE UMEPEWA MADARAKA BAADA YA KUSHIBA UNAKUJA NA HOJA ZA UPUMBAVU HAPA.YAANI NINYI WASOMI MANAKERA SANA.

Mkuu komenti yako ni nzuri sana, lakini tanzania ya leo iko kitofauti. Ingekuwa ni taaswira tungeiita "Virtual image", Tanzania ya leo ukikuta mfanyakazi anasifiwa na viongozi wa juu ujue anawapigia dili, na ukikuta kiongozi anasifiwa na watu wa chini yake ujue anawatumikia wananchi. Huyu wa pili amekuw adui mkubwa wa madili ya wakubwa na anasakwa kila kona, Tafadhali fikiria yaliyowatokea hawa na sababu zake halisi, Sokoine, kigoma, juwan, barlow, kolimba, n.k. pia pitia kurasa za kina Ulimboka, mwakyembe, mwandosya, kibanda, n.k.
Kuna jamaa niliyemfahamu vizuri akiwa chuoni na baadae akaajiriwa idara ya ng'ombe tena akawekwa ktk sehemu nzuri kama farm manager. kila bosi wake alivyomtembelea alihitaji ng'ombe wauwawe ktk taarifa yeye aswage akauze. Hayo yakamtesa mshikaji mara ya kwanza akauwa kadhaa, mara ya pili ikafata baada ya miezi michache tu, na ya tatu ikafuata kwa karibu ndipo mshikaji alipogoma kusikiliza amri na kumwambia bosi, leo siuwi. Njooo uandike mwenyewe, alichojibiwa ni kuwa kesho yake alisimamishwa kibarua na kauli ya kutoajiriwa popote kwa muda usiojulikana ila mshahara akaendelea kupewa. yuko mshikaji anaendelea kulea wajukuu kwa kosa hilo.
Hata hivyo tembea uone, Tz ina maajabu zaidi yale 7 yaliyojitangaza. yapo mengi yamefichwa ktk karatasi sizilizofichwa kwabani.
 
Back
Top Bottom