Taifa la Tanzania mikononi mwako Mungu

Watanzania macho yao yapo mbele yako Mungu. Usipo shuka nakututetea basi tumeangamia. Wewe unaona toka mbali sana na Wewe ndie Baba wa Taifa la Tanzania.
Shetani amekunjuwa makucha kuturaruwa nakutugawa mithili ya vazi lililo kuukuu.

Je utafunga macho yatokee yale wanadam wamepanga yatokee siku zijazo au utashuka na kuusikiliza mkutano wao nakuwagawanya ndimi kuliokoa Taifa?

Wakati Hayati baba wa Taifa anaondoka hapa duniani alisema neno ambalo kwa sasa huu niwakati wako kulitekeleza... Alisema anatuombea Watanzania na yakwamba alitupenda na aliona yatakayo tokea kwa watanzania na akaomba Utusaidie na kutuokoa.

Mungu najuwa yapo mambo yamekukera na yamekukwaza na umeshuka kwa operation maalumu ktk Taifa la Tanzania najuwa watanzania wengi wakiwa wamelala wasijuwe chochote wewe utapita ktk anga ya Tanzania nakuacha watu midomo wazi wakati watakapo amka wasiamini kile umefanya.

Baba najuwa huu mwaka mpaka 2025 matendo yako yatakuwa dhahiri kwa taifa swala la haki utu na usawa utalisamia like never before. Wengi hawato amini ila je jina lako lidharaulike ? Lahasha kwa ajili ya watanzania umeshuka kwa ajili ya hili taifa umeshuka.

Hukushindwa kumpa miaka mingi Hayati Magufuli ila Wewe kwakuwa ni Mzee wa Siku Baba wa Siri za dunia ukaufupisha mwisho wake baada yakuona Kesho ambayo hakuna mtanzania aliijuwa na hata milele hatutojuwa maana jambo hili halikuwa lakawaida na kamwe pasipo kuachia wewe lisingetokea. Ila umetuacha na maswal magumu kwanini ulimuondoa katikati ya watu milion arobain na kitu? Mbona Ezekia ulimuongezea miaka yakuishi why not Magufuli?


Ulishuka ukawasikiliza ukaona mipango yao na malengo yao ktk siri ukausitisha mpango wao na hii nikujidhihirisha Wewe ni Mungu wa Taifa hili tumelia tumeombeza ila Wewe unabaki kuwa Mungu. Mapenzi yako yatimizwe duniani kama mbinguni na kazi yako haina makosa.

Wakati huu umeshuka na wengi wapo ktk usingizi wakiwa wamesahau kile kimetokea...
Wengine wakiabudu miungu nakupunga pepo kwa ajili ya Taifa je malango ya Taifa utaruhusu haya yatoke? Moyo wangu unalia na unaomboleza maana najuwa hutokubali na mbaya kuliko yote Utajibu wakati wakiza kinene sana.

Weka maarifa na hekima kwa wakuu wa ulinzi na usalama wa Taifa hili waonyeshe ktk maono na ndoto yale yatatokea wape mbinu za kimbingu kulinda amani ya Taifa Tz.



Taifa hili ni Taifa lako Taifa hili ni mali yako Mungu ulio wapa watanzania wote pasipo kujali dini,kabila au tamaduni. Sisi ni watoto wako. Amen

Niliwahi kusema, hiki kipindi muhimu kufunga nakuombea taifa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom