Taifa kwanza: Viongozi watarajiwa wajitokeze sasa tujue misimamo yao!

kuna sehemu ndogo sana huenda najichanganya ama nachanganywa....haiingii akilini Nape M. N kusimama kidete na hata kufikia hatua ya kuwataja wakubwa wazi wazi kua walihusika/kuhusishwa moja kwa moja na ubadhirifu kwenye mradi wa Umoja wa vijana kipindi akiwa Youth,akasemwa sana kwamba ana gubu,hila na wakaenda mbali zaidi kwa kusema alitanguliza miguu badala ya kichwa...Naam Nape huyu huyu ni mwiba kwa wale waliomkandamiza juzi...kwa kukosa ufafanuzi huoni kwa mtu mwenye mawazo huru km mimi nitafikiria bwana Nape analipiza kisasi wakati sio sahihi na badala yake anasimamia kanuni?
 
Mkuu nadhani misimamo huwa inatoa mwanga kwa wananchi kuingia a bit deeper kufahamu hao watu ni wa namna gani. Kumbuka watu kama Mahanga na Serukamba walivyojitokeza hadharani kutetea Richmond, Dowans, kumtetea Lowassa. Hii ilisaidia kuconnect dots na hatimaye kuwafahamu ni watu wa namna gani. Personally nilikuwa namfahamu Mahanga kupitia kwa mtu wake wa karibu sana na siku zote alipokuwa akiniambia the inside out of the guy kisi fulani nilikuwa siamini amini.

Sasa chukulia mfano Membe, bila kumjua msimamo wake kwenye issues utamhukumu kwa matendo yapi? Maana wizara anayoiongoza haina direct impact na maisha ya kila siku ya wananchi. Mtu kama Hawa Ghasia huwezi kumuhukumu kwa namna idara nzima ya utumishi wa serikali ilvyokuwa hovyo itakuwa ni kumuonea. Total reform ya hii kitu is such a huge project na inatakiwa ifanyike ndani ya serikali nzima including ikulu. Na mbaya zaidi total reforming that system will immediately make you so unpopular ndani ya serikali hivyo kujikuta hupewi ushirikiano.

Haswaa!
Sio lazima wajitangaze, lakini wao wanajijua mioyoni mwao na ni vema wakaweka misimamo yao kuhusu masuala ya kitaifa.
Willy ana maana ya mifano ifuatayo: D.Cameron msimamo wake ni kuwa na serikali ndogo na kubana matumizi.
Obama: ku-regulate buisness na social welfare kama Health. Hu Jintao: Kukuza uchumi wa china kwa export, Momahan Singh: Kuiendeleza india kiteknolojia. Dr Slaa: Kusimamia matumizi ya fedha za umma, Zitto Kabwe: Madini yachangie pato la taifa, Maalimu Sefi: Kuvunja muungano, Mh Pinda: Kutochanganya siasa na sheria, Prof Shivji: Azimio la Arusha, Butiku: Nidhamu ya chama, Warioba: Nidhamu ya serikali, Dr Salimu: Muungano n.k

Sisi hatuna mahali kama kura za bunge kujua misimamo yao kitaifa ndiyo maana huwa wanazuka tu na kauli mbiu bila sisi kuwajua wanamanaanisha nini,kumbe wanafuata upepo wa kisiasa.
 
be blessed
leo umenifurahisha sana.
JK alifaidika na mfumo huu wa kupiga kimya kwani kwa mamiaka yote akiwa wizara tofauti hatukuwai kusikia msimamo wake kwenye ishu hata mmoja
mara gafla akawa rais .

mimi naona move ya akina Lowassa+Membe ilikuwa tamu manake with short time tungeanza kuwaweka kwenye viganja vyetu kuhusu misimamo yao.My take hawa jamaa mapema tu wangeliweza kutangaza nia.
 
William, nakubaliana na wewe. Lakini tatizo tulilonalo si kwamba viongozi hawasemi misimamo yao ila 'hawaishi" misimamo yao. They have to stand on those issues that they believe on. Kwa mfano, Mh Mwakyembe alifanya invistigation ya Richmond na mwishoe Bunge lilipitisha maazio ya mapendekezo yote 18 yalotolewa na timu yake. Pamoja na kwamba Pinda kama mkuu wa shughuli za Serikalia bungeni aliahidi kutoa report ya utekelezaji wa mapendekezo hayo (within a specified time) hakuna lolote limefanyika. Na sasa Mwakyembe ni Deputy Minister, wajumbe wake wengine wamerudi tena ndani ya bunge kama Stella Manyanya lakini hatusikii wana msimamo gani juu ya yale waliyosema. Personally, nimekuwa natamani sana kukutana na Stella Manyanya nimuulize what does she stand for? hilo tu.

Wapo wengine wamekuwa kama vinyonga, Mama Anne Kilango- she was spitting fire, Ole Sendeka na wengine, lakini sasa we don't know wamekaa kimya kwa sababu ufisadi umeisha? au they have given up.

Yote tisa, kumi ni hili, ni nani asiyekumbuka Kikwete wakati wa campaign za 2005, alikuwa anaongea vitu vizuri mno na kila mtu alimwamini, e.g mikataba ya madini, umeme, ajira kwa vijana, utawala wa sheria. Lakini sina shaka Kikwete will go down the history lane as the worst president this nation has ever had. Haijulikani ana msimamo gani kwenye anything. Hata issue ya Dowans na ICC alikuwa anafuata upepo!

Matekeo yake ni kwamba watu na hasa wapiga kura wanapoteza imani na wanasiasa (in case CCM ndio wameathirika zaidi) kwa sababu it is not what they say, it is what they DON'T say. au tuseme it is what they do.
 
Facebook @ NEW YORK CITY: Imekuwa ni tabia inayokubalika sana miongoni mwetu wananchi, na hasa wana CCM kwa Viongozi watarajiwa kunyamaza kimyaa, mpaka ikishafikia wakati wa uchaguzi ndio utaona wanaanza tokeza na kusema maneno machache sana kwenye public tena kwa ujanja sana ili kujaribu ku-minimize the damage ya where they stand on the ishus important to the people, waonekane wako kwenye mstari flani ambao unaaminkai sana kwamba unakubalika na Chama, regardless ya kukubalika na wananchi, matokeo yamekua viongozi na cham kukosa elimu ya kero za wananchi.

- Tunasema hivi kwa wale wote Viongozi watarajiwa kwenye chama chetu CCM, ni vyema wakaanza kujitokeza sasa tukawajua wanasimamia wapi na ishus muhimu sana kwa taifa, zile tabia za kumchagua kiongozi tusiyejua anaposimama na ishus zimeanza kupitwa na wakati, wana-CCM tuwakatae kabisa viongozi wa namna hiyo, maana ni nothing but wanafiki, wanaotaka kujiweka sawa na upepo wa bendera kufuatana na siasa za wakati. Wanaotaka kutuongoza mbele ya safari tuanze kuwajua sasa wapo wapi na Mafisadi, Elimu, EPA, IPTL, KAGODA, DOWANS, Mgawo wa Umeme, Madini, Ulipaji wa kodi, Muungano, Udini, Ukabila, I mean na mengineyo tuwajue sasa wanasimamia wapi?

- I mean matokeo ya hii tabia, hili taifa tumekua na viongozi ambao wanakuwa kama wanatokea Mars Planet, wananchi tunaongea lugha tofauti na wao, ndio maana mmoja wao alisema tutakula hata majani lakini ndege itanunuliwa, juzi tumesikia Mkurugenzi wa ATC aki-retire baada ya kuongoza shirika la ndege ambalo halina ndege hata moja anyways! Leo Tanzania tuna Radar ambayo hata walioitengeneza wamesema waliitengeza kwa sababu ya nchi kama Israel sio sisi, haya yote yamewezekana kwa sababu hili taifa tumejaza maviongozi wengi magoi goi, ambao hatukuwahi kuwasikia wakitoa maoni yao on anything kuhusu ishus muhimu kwa taifa kabla hawajawa viongozi, and then wakianza kutoa utumbo wao hadharani baada ya kuwa viongozi tunashangaa, walitokea wapi?

Tunasema hivi wale wote mnaotaka kutuongoza mbele ya safari, tafadhalini sana jitokezeni sasa tuwajue misimamo yenu kuhusu ishus muhimu za taifa, na hasa kero za wananchi kwa sasa, sio kujificha ficha na baadaye kuja kutufikisha pabaya, we have enough tayari! Tunawakumbusheni tu kwamba wote tunawamulika sana kwenye hii mitandao na nje pia, kuona consistency ya misimamo yenu, kumbukeni kwamba huko tunakokwenda ni mitandao ndiyo itaaamua nani awe kiongozi wetu na nani asiwe!, sasa jitokezeni tuwajue misimamo yenu sasa!

William Malecela @ New York City, USA.

Wananchi tumeishafanya uchaguzi siku nyingi sana, baada ya kupata shule ya maumivu makali
katika maisha yetu kwa kipindi cha zaidi ya miaka thelathini sasa, tumeishajua pumba na mchele.

William, naona bado uko nyuma sana ndugu, Watanzania tulio hapa nyumbani tumeishajua
kwamba, taifa hili haliwezi kupata uongozi acha viongozi, kutoka CCM, Tumewapitisha CCM
Kwenye joto kali sana wakati wa uchaguzi, tulitegemea kuona mabadiliko, lakini sasa ndio
wanaharibu zaidi.

Tumeisha amua kuachana nao, ndio maana tuko busy kuimalisha CHAMA CHA DEMOCRASIA
na MAENDELEO, Jana kimefanya Uchaguzi wa Balaza lake la Vijana, Ameshinda kijana anaitwa
JOHN HECHE, UMA wa watanzania unaimani hata kwa kijana mdogo sana kama huyu kuliko
hata mzee Mwenye.

Hao unaotaka kuwaamsha, wamerushiwa hata mawe lakini hawakustuka, wewe watakusikia
kweli, kwanza hizi hoja zako nzuri sana ulizoanza kuibuka nazo siku hizi, huko CCM zinachukuliwa
kama Mzee anakuandaa kijanja kuja kupambana na ama Ridhiwan au January.
 
William, nakubaliana na wewe. Lakini tatizo tulilonalo si kwamba viongozi hawasemi misimamo yao ila 'hawaishi" misimamo yao. They have to stand on those issues that they believe on. Kwa mfano, Mh Mwakyembe alifanya invistigation ya Richmond na mwishoe Bunge lilipitisha maazio ya mapendekezo yote 18 yalotolewa na timu yake. Pamoja na kwamba Pinda kama mkuu wa shughuli za Serikalia bungeni aliahidi kutoa report ya utekelezaji wa mapendekezo hayo (within a specified time) hakuna lolote limefanyika. Na sasa Mwakyembe ni Deputy Minister, wajumbe wake wengine wamerudi tena ndani ya bunge kama Stella Manyanya lakini hatusikii wana msimamo gani juu ya yale waliyosema. Personally, nimekuwa natamani sana kukutana na Stella Manyanya nimuulize what does she stand for? hilo tu.

Wapo wengine wamekuwa kama vinyonga, Mama Anne Kilango- she was spitting fire, Ole Sendeka na wengine, lakini sasa we don't know wamekaa kimya kwa sababu ufisadi umeisha? au they have given up.

Yote tisa, kumi ni hili, ni nani asiyekumbuka Kikwete wakati wa campaign za 2005, alikuwa anaongea vitu vizuri mno na kila mtu alimwamini, e.g mikataba ya madini, umeme, ajira kwa vijana, utawala wa sheria. Lakini sina shaka Kikwete will go down the history lane as the worst president this nation has ever had. Haijulikani ana msimamo gani kwenye anything. Hata issue ya Dowans na ICC alikuwa anafuata upepo!

Matekeo yake ni kwamba watu na hasa wapiga kura wanapoteza imani na wanasiasa (in case CCM ndio wameathirika zaidi) kwa sababu it is not what they say, it is what they DON'T say. au tuseme it is what they do.
Mkuu JK alikuwa prepared na mafisadi wakamuandalia kila kitu! Mkuu hawa watu wanaakili kuliko tunavyowafikilia au Nape anavyowachukulia, na wajanja sana. wanaweza kuingia popote na wanajua wananchi wanapenda kusikia nini! Kauli ya mtu si tatizo but ni kweli anachukia toka moyoni haya mambo?
 
Haswaa!
Sio lazima wajitangaze, lakini wao wanajijua mioyoni mwao na ni vema wakaweka misimamo yao kuhusu masuala ya kitaifa.
Willy ana maana ya mifano ifuatayo: D.Cameron msimamo wake ni kuwa na serikali ndogo na kubana matumizi.
Obama: ku-regulate buisness na social welfare kama Health. Hu Jintao: Kukuza uchumi wa china kwa export, Momahan Singh: Kuiendeleza india kiteknolojia. Dr Slaa: Kusimamia matumizi ya fedha za umma, Zitto Kabwe: Madini yachangie pato la taifa, Maalimu Sefi: Kuvunja muungano, Mh Pinda: Kutochanganya siasa na sheria, Prof Shivji: Azimio la Arusha, Butiku: Nidhamu ya chama, Warioba: Nidhamu ya serikali, Dr Salimu: Muungano n.k

Sisi hatuna mahali kama kura za bunge kujua misimamo yao kitaifa ndiyo maana huwa wanazuka tu na kauli mbiu bila sisi kuwajua wanamanaanisha nini,kumbe wanafuata upepo wa kisiasa.

Du umenichekesha sana msimamo wa seif! JK nadhani yeye itakuwa Maisha Bora kwa kila Mtanzania au Nguvu zaidi,kasi zaidi na hali zaidi huenda nadhani!
 
Wazo zuri lakini Tanzania wanasiasa hawaishi na misimamo yao wanabadilika kama kinyonga kutegemea na maslahi ya wakati.
 
Mfano mzuri ni Wassira, aka Tyson!
Siku akiona CCM wanambabaisha atahamia kunako maslahi!
 
Facebook @ NEW YORK CITY: Imekuwa ni tabia inayokubalika sana miongoni mwetu wananchi, na hasa wana CCM kwa Viongozi watarajiwa kunyamaza kimyaa, mpaka ikishafikia wakati wa uchaguzi ndio utaona wanaanza tokeza na kusema maneno machache sana kwenye public tena kwa ujanja sana ili kujaribu ku-minimize the damage ya where they stand on the ishus important to the people, waonekane wako kwenye mstari flani ambao unaaminkai sana kwamba unakubalika na Chama, regardless ya kukubalika na wananchi, matokeo yamekua viongozi na cham kukosa elimu ya kero za wananchi.

- Tunasema hivi kwa wale wote Viongozi watarajiwa kwenye chama chetu CCM, ni vyema wakaanza kujitokeza sasa tukawajua wanasimamia wapi na ishus muhimu sana kwa taifa, zile tabia za kumchagua kiongozi tusiyejua anaposimama na ishus zimeanza kupitwa na wakati, wana-CCM tuwakatae kabisa viongozi wa namna hiyo, maana ni nothing but wanafiki, wanaotaka kujiweka sawa na upepo wa bendera kufuatana na siasa za wakati. Wanaotaka kutuongoza mbele ya safari tuanze kuwajua sasa wapo wapi na Mafisadi, Elimu, EPA, IPTL, KAGODA, DOWANS, Mgawo wa Umeme, Madini, Ulipaji wa kodi, Muungano, Udini, Ukabila, I mean na mengineyo tuwajue sasa wanasimamia wapi?

- I mean matokeo ya hii tabia, hili taifa tumekua na viongozi ambao wanakuwa kama wanatokea Mars Planet, wananchi tunaongea lugha tofauti na wao, ndio maana mmoja wao alisema tutakula hata majani lakini ndege itanunuliwa, juzi tumesikia Mkurugenzi wa ATC aki-retire baada ya kuongoza shirika la ndege ambalo halina ndege hata moja anyways! Leo Tanzania tuna Radar ambayo hata walioitengeneza wamesema waliitengeza kwa sababu ya nchi kama Israel sio sisi, haya yote yamewezekana kwa sababu hili taifa tumejaza maviongozi wengi magoi goi, ambao hatukuwahi kuwasikia wakitoa maoni yao on anything kuhusu ishus muhimu kwa taifa kabla hawajawa viongozi, and then wakianza kutoa utumbo wao hadharani baada ya kuwa viongozi tunashangaa, walitokea wapi?

Tunasema hivi wale wote mnaotaka kutuongoza mbele ya safari, tafadhalini sana jitokezeni sasa tuwajue misimamo yenu kuhusu ishus muhimu za taifa, na hasa kero za wananchi kwa sasa, sio kujificha ficha na baadaye kuja kutufikisha pabaya, we have enough tayari! Tunawakumbusheni tu kwamba wote tunawamulika sana kwenye hii mitandao na nje pia, kuona consistency ya misimamo yenu, kumbukeni kwamba huko tunakokwenda ni mitandao ndiyo itaaamua nani awe kiongozi wetu na nani asiwe!, sasa jitokezeni tuwajue misimamo yenu sasa!

William Malecela @ New York City, USA.
:dance:Katika hili nakubaliana nawe kwamba ni muhimu kutambua mustakabali wa watarajiwa hasa misimamo yao ili mbele ya safari kieleweke! Kimsingi, ccm inazo kanuni zake ambazo kwa mtazamo wangu bado ni valid! Lkn zimekuwa zikivurugwa na wana ccm wenyewe,japokuwa when you read btn the lines wanao mtindo wa ku-groom viongozi kupitia vijana kwa kuwa-scout hata kusomesha ndani na nje pengine wewe William ni miongoni pamoja na kwamba si formal!!! Siyo vibaya???Mwl alikuwa na uwezo wa kuamua hili tumelishudia kwa Mkapa yasemekana ccm hawakupenda lkn peke yake alimpigia debe akawa rais na alijitahidi ku-contriol uchumi ukawa single-digity! Nani anabisha????? Sasa hivi hakuna wa kukemea imekuwa strugle for the fittest-law of the jungle!!! Makundi nayo yanachangia mitzizamo ya kihfidhina ndiyo balaa??????? KWA HALI KUJITOKEZA NI NADRA SANA !! Labda Sitta/Mwakyembe/Pinda/Malecela/Sumaye nk ndiyo wamethbutu kujitokeza nani mwiingine????? Tuachane na domocrasia isiyo muafaka!! Atakayejitokeza sasa hivi watakuwa na msimamo thabiti!!!!

DEMOCRACY IS A TOOL OF DEVIL USED TOCORRUPT MANKIND!!!!:A S 103:
 
William, nakubaliana na wewe. Lakini tatizo tulilonalo si kwamba viongozi hawasemi misimamo yao ila 'hawaishi" misimamo yao. They have to stand on those issues that they believe on. Kwa mfano, Mh Mwakyembe alifanya invistigation ya Richmond na mwishoe Bunge lilipitisha maazio ya mapendekezo yote 18 yalotolewa na timu yake. Pamoja na kwamba Pinda kama mkuu wa shughuli za Serikalia bungeni aliahidi kutoa report ya utekelezaji wa mapendekezo hayo (within a specified time) hakuna lolote limefanyika. Na sasa Mwakyembe ni Deputy Minister, wajumbe wake wengine wamerudi tena ndani ya bunge kama Stella Manyanya lakini hatusikii wana msimamo gani juu ya yale waliyosema. Personally, nimekuwa natamani sana kukutana na Stella Manyanya nimuulize what does she stand for? hilo tu.

Wapo wengine wamekuwa kama vinyonga, Mama Anne Kilango- she was spitting fire, Ole Sendeka na wengine, lakini sasa we don't know wamekaa kimya kwa sababu ufisadi umeisha? au they have given up.

Yote tisa, kumi ni hili, ni nani asiyekumbuka Kikwete wakati wa campaign za 2005, alikuwa anaongea vitu vizuri mno na kila mtu alimwamini, e.g mikataba ya madini, umeme, ajira kwa vijana, utawala wa sheria. Lakini sina shaka Kikwete will go down the history lane as the worst president this nation has ever had. Haijulikani ana msimamo gani kwenye anything. Hata issue ya Dowans na ICC alikuwa anafuata upepo!

Matekeo yake ni kwamba watu na hasa wapiga kura wanapoteza imani na wanasiasa (in case CCM ndio wameathirika zaidi) kwa sababu it is not what they say, it is what they DON'T say. au tuseme it is what they do.

- Hawasemi kwa sababu hatuwaulizi na hata wakisema hatuweki records, naomba mwananchi mmoja anisaidie hivi kabla ya hii hotuba ya juzi ya Bashe, huko nyuma aliwahi kusema nini on the same ishus?

- Kwa mfano Mzee Msekwa, alipowekwa pembeni na uongozi, alisema maneno mengi mazuri sana, lakini walipomrudisha sijasikia akisema tena na wala mwandishi yoyote akimuuliza kuhusu yale maneno ya kishujaa aliyoyasema akiwa nje ya uongozi, WHY? Sasa mambo madogo kama haya ambayo ni muhimu sana kwa taifa kwa nini tunategmea kufanyiwa na wengine?

William @ NYC, USA
 
Yes tatizo sio msimamo tatizo ni wakishaingia "jikoni" sisi waliotuacha "sebuleni" tunabaki tunashangaa Maana wakiwa sebuleni wanayoongea yote tunaona wanafaa kuwa jikoni. Sasa wakipewa nafasi ya kwenda jikoni kimyaaa tena baadae ndo wantumiwa na wapishi wabovu kuja kutueleza sisi wa sebuleni kwanini mapishi hayaivi ..

Mimi nimetolea mfano Kuna viongozi wanasema kisiasa tuende bishaa zetu na tukuze ajira. How?? wakati wabuge wote wanavaa suti za china na Italy/ Hawashoneshi japo suti viwili kwa maufundi wa wa humu ndani. Majukwaani wanawaambia watanzania tununue bidhaa za Tanzania. Hivi ni Kosa kwa mbunge kuvaa Moka japp pai moja ya kuchongesha ya ndani.

Kuna wizara ya mazingra pamoja na wataaam wa mazingira pale wana magari yanayotoa carobon emmsion na ma VX mengi tu . Si waziri si katibu wana akili ya kusema ebu tununue gari ya umeme moja kwa matumizi ya wizara au japo satandard yao iwe Vitara tu. So kama viongozi wa wiziara ya mazingira hawaoni umuhimu wa mazingira. Lakini hawa viongozi wakiwa kwenye TV utasikia wakiongela mazingira kama maprof..........

kuna mifano mingi ni kwamba tumejikita kwenye siasa sana na tunasahu matendo na mifano. Na siasa ni simple sababu ni maneno tu
 
Ni wazo zuri kwa hawa watu kujitokeza wakafahamika misimamo yao na wala hawa sababu ya kuogopa. Yule aliyekuwa anawatishia kufa hatunaye tena.
 
Facebook @ NEW YORK CITY: Imekuwa ni tabia inayokubalika sana miongoni mwetu wananchi, na hasa wana CCM kwa Viongozi watarajiwa kunyamaza kimyaa, mpaka ikishafikia wakati wa uchaguzi ndio utaona wanaanza tokeza na kusema maneno machache sana kwenye public tena kwa ujanja sana ili kujaribu ku-minimize the damage ya where they stand on the ishus important to the people, waonekane wako kwenye mstari flani ambao unaaminkai sana kwamba unakubalika na Chama, regardless ya kukubalika na wananchi, matokeo yamekua viongozi na cham kukosa elimu ya kero za wananchi.

- Tunasema hivi kwa wale wote Viongozi watarajiwa kwenye chama chetu CCM, ni vyema wakaanza kujitokeza sasa tukawajua wanasimamia wapi na ishus muhimu sana kwa taifa, zile tabia za kumchagua kiongozi tusiyejua anaposimama na ishus zimeanza kupitwa na wakati, wana-CCM tuwakatae kabisa viongozi wa namna hiyo, maana ni nothing but wanafiki, wanaotaka kujiweka sawa na upepo wa bendera kufuatana na siasa za wakati. Wanaotaka kutuongoza mbele ya safari tuanze kuwajua sasa wapo wapi na Mafisadi, Elimu, EPA, IPTL, KAGODA, DOWANS, Mgawo wa Umeme, Madini, Ulipaji wa kodi, Muungano, Udini, Ukabila, I mean na mengineyo tuwajue sasa wanasimamia wapi?

- I mean matokeo ya hii tabia, hili taifa tumekua na viongozi ambao wanakuwa kama wanatokea Mars Planet, wananchi tunaongea lugha tofauti na wao, ndio maana mmoja wao alisema tutakula hata majani lakini ndege itanunuliwa, juzi tumesikia Mkurugenzi wa ATC aki-retire baada ya kuongoza shirika la ndege ambalo halina ndege hata moja anyways! Leo Tanzania tuna Radar ambayo hata walioitengeneza wamesema waliitengeza kwa sababu ya nchi kama Israel sio sisi, haya yote yamewezekana kwa sababu hili taifa tumejaza maviongozi wengi magoi goi, ambao hatukuwahi kuwasikia wakitoa maoni yao on anything kuhusu ishus muhimu kwa taifa kabla hawajawa viongozi, and then wakianza kutoa utumbo wao hadharani baada ya kuwa viongozi tunashangaa, walitokea wapi?

Tunasema hivi wale wote mnaotaka kutuongoza mbele ya safari, tafadhalini sana jitokezeni sasa tuwajue misimamo yenu kuhusu ishus muhimu za taifa, na hasa kero za wananchi kwa sasa, sio kujificha ficha na baadaye kuja kutufikisha pabaya, we have enough tayari! Tunawakumbusheni tu kwamba wote tunawamulika sana kwenye hii mitandao na nje pia, kuona consistency ya misimamo yenu, kumbukeni kwamba huko tunakokwenda ni mitandao ndiyo itaaamua nani awe kiongozi wetu na nani asiwe!, sasa jitokezeni tuwajue misimamo yenu sasa!

William Malecela @ New York City, USA.
Ndugu Malecela unaandika mawazo mazuri lakini viongozi wote wanaotokana na CCM hivi sasa ni wachumia tumbo, hawana huruma na watanzania, huyo Kikwete ambaye mnamtetea kwamba watendaji wake wanamuangusha ni nani asiye jua kuwa kabla ya kuukwaa urais alikuwa na kashfa luluki sema kwa sababu ya falsafa yenu ya wakati wa uchaguzi ya mafiga matatu, mnatuchagulia majambazi, wezi, wazinzi, wasanii, wauza unga.
Na kiongozi mzuri ndani ya CCM ni yule mwenye pesa ya kuwapa wajumbe wakati wa vikao vya chama, ndio maana mapacha watatu wanawatesa sana na hamuwezi kuwatosa.
EPA uliohitaja hapo juu ndio ilimuingiza rais wako madarakani, na pia mikataba mibovu ya madini naye anahusika,
Bwana Malecela nimekuwekea na maelezo kutoka tovuti ya Chadema kuhusu rais wako halafu niambie nani amewaangusha watanzania.
Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.
 
Ingawa topic yako imebase kwa wanaccm, ila mimi nikiileta kitaifa zaidi, hakuna kiongozi ambaye anajulikana msimamo wake kwa sasa zaidi ya Dr Slaa, huu ndio ukweli ambao simlazimishi mtu aukubali.
Samuel Sitta kama angekuwa ni kiongozi mwenye msimamo alitakiwa ajiuzuru kuonesha kwamba anasimamia anachoamini, na kabla hajawa mbunge/spika alikuwa ni mkurugenzi wa TIC, na TIC ndio gateway ya wawekezaji fake ambao wanakuja kuwekeza hadi kuuza biashara ya maua ya shillingi 100/= je alilisidia vipi Taifa kipindi hicho kulinda ajira za wazawa? Huyu hafai kuwa Rais.
Nitarudi.
 
W.J.M .... Muacheni mungu aitwe mungu

hebu washa taa ya kijani kwa Livingstone Lusinde pale jimboni 2015 ..... naamini utajenga nchi

- Ha! ha! ha! ha! Mkuu wangu wa kazi! ha! ha! ha!, well we will see! Mh. Lusinde ni mbunge wangu na hands down na ushindi wake, muhimu ni deliverance kwa wananchi as opposed na crying for a status quo, kama Lusinde can deliver hakuna sababu ya kupingana naye next elections maana ni wananchi kwanza!

- HOWEVER: kama ameshindwa ku-deliver then somebody has to step up to the plate, I am a Revolutionary and my life speaks for itself, ujumbe wangu kwa Lusinde deliverance or be prepared to face the music! ha! ha! ha! ha!

William @ NYC, USA.
 
Mkuu Willy,
Walio wengi miongoni mwao hao wanaotarajiwa kukipokea kijiti mbona wako kweney list chafu sasa wajitokeze mapema si mtawachambua mpaka wakose la kusema. Utaratibu wa chama chako ndio mbovu maana hakitaki weney nia wajitokeze au wasafi wajitokeze ambao hawana harufu ya ufisadi maana wataundiwa zengwe na wale ambao wamekwishaharibika
 
- Ha! ha! ha! ha! Mkuu wangu wa kazi! ha! ha! ha!, well we will see! Mh. Lusinde ni mbunge wangu na hands down na ushindi wake, muhimu ni deliverance kwa wananchi as opposed na crying for a status quo, kama Lusinde can deliver hakuna sababu ya kupingana naye next elections maana ni wananchi kwanza!

- HOWEVER: kama ameshindwa ku-deliver then somebody has to step up to the plate, I am a Revolutionary and my life speaks for itself, ujumbe wangu kwa Lusinde deliverance or be prepared to face the music! ha! ha! ha! ha!

William @ NYC, USA.

hapo kwenye red ..... ndiyo maana nilisema kwamba ninaamini unaweza kujenga nchi na si kuitetea ccm peke yake

deliverance is not just a word ... it has magnitude and direction same as velocity.... expect this from devoted people like Dr. Slaa , Hon Mbowev and Hon Zitto ....

Nape is a first class puppet of the twenty first century ..... he can not deliver anything as clock closes down to 2015 ... mkuu think twice

otherwise .... take my words .... the likes of Lusinde are the same dissidents .... never expect patriotism and change... expect immoral leadership and imperative mindset that leads to economic standstill and underdevelopment
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom