Taifa kwanza: Viongozi watarajiwa wajitokeze sasa tujue misimamo yao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa kwanza: Viongozi watarajiwa wajitokeze sasa tujue misimamo yao!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 30, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Facebook @ NEW YORK CITY: Imekuwa ni tabia inayokubalika sana miongoni mwetu wananchi, na hasa wana CCM kwa Viongozi watarajiwa kunyamaza kimyaa, mpaka ikishafikia wakati wa uchaguzi ndio utaona wanaanza tokeza na kusema maneno machache sana kwenye public tena kwa ujanja sana ili kujaribu ku-minimize the damage ya where they stand on the ishus important to the people, waonekane wako kwenye mstari flani ambao unaaminkai sana kwamba unakubalika na Chama, regardless ya kukubalika na wananchi, matokeo yamekua viongozi na cham kukosa elimu ya kero za wananchi.


  - Tunasema hivi kwa wale wote Viongozi watarajiwa kwenye chama chetu CCM, ni vyema wakaanza kujitokeza sasa tukawajua wanasimamia wapi na ishus muhimu sana kwa taifa, zile tabia za kumchagua kiongozi tusiyejua anaposimama na ishus zimeanza kupitwa na wakati, wana-CCM tuwakatae kabisa viongozi wa namna hiyo, maana ni nothing but wanafiki, wanaotaka kujiweka sawa na upepo wa bendera kufuatana na siasa za wakati. Wanaotaka kutuongoza mbele ya safari tuanze kuwajua sasa wapo wapi na Mafisadi, Elimu, EPA, IPTL, KAGODA, DOWANS, Mgawo wa Umeme, Madini, Ulipaji wa kodi, Muungano, Udini, Ukabila, I mean na mengineyo tuwajue sasa wanasimamia wapi?

  - I mean matokeo ya hii tabia, hili taifa tumekua na viongozi ambao wanakuwa kama wanatokea Mars Planet, wananchi tunaongea lugha tofauti na wao, ndio maana mmoja wao alisema tutakula hata majani lakini ndege itanunuliwa, juzi tumesikia Mkurugenzi wa ATC aki-retire baada ya kuongoza shirika la ndege ambalo halina ndege hata moja anyways! Leo Tanzania tuna Radar ambayo hata walioitengeneza wamesema waliitengeza kwa sababu ya nchi kama Israel sio sisi, haya yote yamewezekana kwa sababu hili taifa tumejaza maviongozi wengi magoi goi, ambao hatukuwahi kuwasikia wakitoa maoni yao on anything kuhusu ishus muhimu kwa taifa kabla hawajawa viongozi, and then wakianza kutoa utumbo wao hadharani baada ya kuwa viongozi tunashangaa, walitokea wapi?

  Tunasema hivi wale wote mnaotaka kutuongoza mbele ya safari, tafadhalini sana jitokezeni sasa tuwajue misimamo yenu kuhusu ishus muhimu za taifa, na hasa kero za wananchi kwa sasa, sio kujificha ficha na baadaye kuja kutufikisha pabaya, we have enough tayari! Tunawakumbusheni tu kwamba wote tunawamulika sana kwenye hii mitandao na nje pia, kuona consistency ya misimamo yenu, kumbukeni kwamba huko tunakokwenda ni mitandao ndiyo itaaamua nani awe kiongozi wetu na nani asiwe!, sasa jitokezeni tuwajue misimamo yenu sasa!

  William Malecela @ New York City, USA.
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red kama kuna harufu ya uchokozi vile.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Viongozi watarajiwa ni akina nani?
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I was thinking on the same line kuna huu usemi umezoeleka sana hii awamu ya nne "WANAOMWANGUSHA KIKWETE". Everytime kuna scandal kubwa inatokea au uzembe uliokithiri utasikia ooh! wasaidizi wa Kikwete ndiyo wanaomwangusha. Gademu!!!!! Bei ya gas inavyozidi kuongezeka Marekani watu wanachojua ni Obama amesababisha, hutasikia hata siku moja wamarekani wakisema Biden, Eric Holder au mama Clinton. Sasa sisi siku zote ni kumwepusha mkulu hii sijui ni adabu ya wapi????????? Au Obama aanze kujitetea kwamba yeye hahusiki kwa sababu mafuta yanatoka middle east.

  Nakuunga kabisa mkono mkuu japo mimi si mwanaCCM, "WASIOMWANGUSHA KIKWETE WANYOSHE MIKONO JUU NA KUPITA MBELE"
   
 5. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  maoni mazuri
   
 6. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - I was moved na hotuba ya juzi ya Bashe kule Vijana ndio nikasema ni vyema tukawajua viongozi wetu watarajiwa wana misimamo gani na ishus muhimu za taifa, ingawa ukiisoma sana ile habari ya Bashe utaona kwamba hoja nyingi mle zimetokea hapa JF!

  William @ NYC, USA.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  May 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu haya maneno ni mujarabu sana. Inabidi tuwatambue wenye nia toka pande zote mapema kabisa kwa kuwa atakayechaguliwa atakuwa ni kiongozi wa watanzania na wala si kiongozi wa chama fulani kama atafanya maamuzi mabaya yatawaathiri watanzania wote na sio chama.

  hivi utaratibu wa kuonyesha nia CCM ukoje? Najua wengi huwa wanajitokeza baada ya kuombwa na wapiga kura ama wanachama wenzao kwa kutambua mchango wake. Labda ni wakati muafaka wa kupendekeza majina na kuwaomba wajitokeze ili tupate kauli zao.
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  May 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata mimi hukereka sana na hilo. Hivi nani anawachagua hao wasaidizi? Hivi nani ana uwezo wa kuwaondoa hao wasaidizi? Najua Rais ana uwezo wa kuwateua na kuwaondoa kwa hiyo kama wanamwangusha hakuna neno lingine zaidi ya kwamba Rais anajiangusha mwenyewe, kama hawafai si awaondoe atafute wengine wanaofaa kama anaendelea nao basi anaona wanafaa na kwa maana hiyo anajiangusha! Nimesikia hata Mkuu wa Maaskofu wa Menonite huko Mwanza, Mzee Mang'ana akimwambia Rais aachane na viongozi mizigo. Aachane nao tu.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yea unajua inachekesha eti watu walewale tunaoambiwa leo wanamwangusha JK hence kupelekea poor perfomace, 2015 utakuta ndiyo wanajitokeza eti kugombea uraisi. In short hawamwangushi JK ila wanawaangusha watanzania na hivyo hawaqualify kuchaguliwa kuwaangusha tena watanzania. Kama wanadhani sivyo basi they should stand out from the crowd and say something about the issues. Wanasimamia wapi na nini. Inanifurahisha sana uchaguzi wa Marekani pale wanapowafahamu wagombea wao na misimamo yao mapema kabisa kabla ya uchaguzi!!!!
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  May 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Unajua mkuu we are the future ya National Politics, meaning mitandao so ni muhimu sana tukaanza kuweka records zao na kuwalazimisha kusema wanaposimama na ishus muhimu kwa taifa, ili wakati ukifika tusiwe na wasi wasi kuwapima, I mean ninakaa chini na kujiuliza sana tumewezaje kua na Shirika la ndege lisilo na ndege hata moja? Halafu eti leo mkurugenzi wake ana-retire na atalipwa penshion mpaka mwisho wa maisha yake kwa kuongoza shirika la ndege lililokuwa halina ndege hata moja, viongozi wetu walikuwa wapi kuyaona haya?

  - I mean mitandao we are the future ya hili taifa, wapende wasipende that is a fact, sasa uamuzi ni wetu the mitandao kuwashupalia watarajiwa wote si tunawajua sana, sasa tuwamulike tuwajue wanaposimamia sasa!

  William @ NYC, USA.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Hapo kuna substance!

  Nadhani hii ndiyo sababu inayopelekea akina Nape kwenda kukagua majengo na mitaro ya maji-taka ya vyuo vikuu, na kutoa ushauri "technical" wa jinsi ya kufanya marekebisho(sielewi kama Nape ana taaluma ya uhandisi).

  Eneo kama UDOM lina wanataaluma wengi, lakini pia nadhani bado mafundi wa ujenzi wapo pale wakiendelea na ujenzi!...Lakini zaidi kuna Kuna Waziri wa Ujenzi na na watu wake wanaohusika na ukaguzi wa Majengo, hawa wote wanapoteza nafasi muhimu ya kujipandisha cv zao kwa kufanya ukaguzi kama aliofanya nape na kuonekana kwenye RUNINGA jioni yake!...matokeo yake tutakuja kuchagua watu wa dizaini ya NAPE maana ndio tunaowaona kwa frequency kubwa kwenye Media!.. ha ha haaa!
   
 12. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu, mimi nina maoni tofauti,

  Kama unamaanisha viongozi watarajiwa ni wagombea uraisi, kwa upande wangu hata wasipojitokeza mapema inabidi tuwahukumu kwa matendo yao yaliyopita. Bahati nzuri mara nyingi wagombea hawa huwa ni watu ambao wanakua tayari wana nafasi mbalimbali za uongozi kwenye jamii ... sasa si tuwahukumu kwa walichokifanya kabla ya kugombea?

  Unajua kwa nchi zetu za Africa, hasara ya kujitokeza kutangaza nia inaambatana na ahadi lukuki hewa. Sisi hatutaki tena ahadi, tuone ulifanya nini siku zilizopita. Mnasemaje wana JF?
   
 13. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  -Mkuu W.J.M tutawajua tu kwa matendo yao....imekua kawaida sana kwa tunaodhani ni makamanda wa ukweli kua vibaraka wa aliokua akiwalaani pindi apatapo nafasi...Hiyo mosi,mbili siasa zetu zimekua za chuki na kulipizana visasi ndiyo maana leo sishangai bwana mdogo (aliyeko kwenye uongozi leo) kumtukana mtu mzima aliyekua kwenye uongozi juzi simply kwa kua hakumpa nafasi enzi zake wakati bwana mdogo anaamini uwezo alikua nao by the time.

  -Wako wapi makamanda wapambanaji wenye uthubutu wa kusimama imara na kusema kwa haki "bwana mkubwa eee" nashukuru kwa kunipatia nafasi hii lakini ni dhambi kuisherehekea kwa kua sitakua nimewatendea haki wananchi ninaowawakilisha.Mbunge "mpinga ufisadi" leo ni Waziri asiye na dhamana ya kusema tena!

  -Kuokoa muda na wakati yafaa tu kusema kwamba mawazo yako ni mazuri ila ingefaa sana kama CCM ikafanyiwa reform ya ukweli na kukawepo kanuni za wazi za kushughulikia wale wote wanaokwamisha/haribu harakati za chama bila kujali nafasi zao kiserikali na chama kwa ujumla. Baada ya kufanikisha hili naamini wazalendo wenye nia njema na nchi hii watasimama kidete na bila kujitangaza tutajua wazi ni nani mwenye msimamo gani kwenye jambo gani.

  Wasalaaam
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  May 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Yote ni sawa mkuu, ni muhimu sana kujua wanasiama wapi kwa matendo yao na maneno yao pia kwa mfano kabla hii hotuba huko nyuma Bashe aliwahi kusema nini kuhusu haya aliyoyasema sasa?

  William @ NYC, USA.
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  May 30, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - CCM tunazo kanuni ila hazifuatwi tu!

  William @ NYC, USA.
   
 16. G

  Godwine JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  nadhani ni wakati wa mabadiliko
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu nadhani misimamo huwa inatoa mwanga kwa wananchi kuingia a bit deeper kufahamu hao watu ni wa namna gani. Kumbuka watu kama Mahanga na Serukamba walivyojitokeza hadharani kutetea Richmond, Dowans, kumtetea Lowassa. Hii ilisaidia kuconnect dots na hatimaye kuwafahamu ni watu wa namna gani. Personally nilikuwa namfahamu Mahanga kupitia kwa mtu wake wa karibu sana na siku zote alipokuwa akiniambia the inside out of the guy kisi fulani nilikuwa siamini amini.

  Sasa chukulia mfano Membe, bila kumjua msimamo wake kwenye issues utamhukumu kwa matendo yapi? Maana wizara anayoiongoza haina direct impact na maisha ya kila siku ya wananchi. Mtu kama Hawa Ghasia huwezi kumuhukumu kwa namna idara nzima ya utumishi wa serikali ilvyokuwa hovyo itakuwa ni kumuonea. Total reform ya hii kitu is such a huge project na inatakiwa ifanyike ndani ya serikali nzima including ikulu. Na mbaya zaidi total reforming that system will immediately make you so unpopular ndani ya serikali hivyo kujikuta hupewi ushirikiano.
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  hii dhamira imetoka wapi willy?.......
   
 19. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,963
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180


  Mkuu W Malecela . nakufagilia kwa analysis hii na proposition.
  Tunajua wapambe wa hawa "presidential canditates" wapo humu JF ila wawaambie kuwa akijitokeza FISADI tu (yale magamba yasiyotoka)siye tunaye.
   
 20. L

  LAT JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  W.J.M .... Muacheni mungu aitwe mungu

  hebu washa taa ya kijani kwa Livingstone Lusinde pale jimboni 2015 ..... naamini utajenga nchi
   
Loading...