Taifa Kukosa Muelekeo & Sera: Is CCM Too Big For Itself?

KANU ya kenya ilikuwa kubwa vilevile, USSR likuwa kubwa vilevile..sioni sababu yoyte ya kuogopa ukubwa wa CCM tatizo wapambanaji (wanaojiita) hawapambani ila wanafanya maigizo kwa sababu (interest) zao na za kikundi chao so hawana mshiko kwenye jamii iliyo pana na kubwa.

Itafika siku na iko karibu Wanamchi watashindwa kuvumilia na kwenda barabara kwa nguvu wakiongozwa na watu wenye kulnda kwa dhati maslahi yao kuliko hawa wanaojiita wapiganaji (wasanii)
 
- Hapana mkuu ninasimama mabadiliko siku zote ila huwa sikurupuki, nisingeweza kusema haya huko nyuma kwa sababu sikuwa na sababu, ni sasa kwa maoni yangu ndio CCM wameanza kutoa sababu za msingi za sisi wananchi kudai kugawanyika kwao, ingawa kwako huenda walishazitoa zamani,

- Waliyoyafanya in the last four months ni simply kwamba chama ni kikubwa mno kwa hata Mwenyekiti wake kukisimamia, I understand weekend hii kuna kikao cha siri cha CC tutasubiri kuwasikia wanasema nini lakini ninasema kwamba wakati umefika wa sisi wananchi kudai kuvunjika kwa CCM ikibidi hata kwa ku-suggest kuundwa mswaada kama wa anti-trust kule US, uliovunja shirika kubwa la mafuta la Standard Oil la Rockefeller ambalo nalo lilikuwa kubwa mno kama CCM ya sasa, it took a new law kulivunja, wananchi tunahiatji sasa kudai haya ya sheria mpya ya kuivunja CCM, sababu za msingi zipo tena wazi!

- Mkulu Pasco, ni sasa ndio zipo sababu za msingi za kuanzisha sheria ya kuivunja CCM na hasa kitendo cha juzi cha kulitumia bunge kumsafisha Lowassa na wenzake, ahsante kwa kunielewa mkuu!

Mungu aibariki Tanzania.

Respect.

FMEs!
Sasa kama Lowassa hana makosa mnalazimishaje awe nayo? Tatizo lako Field Marshals unataka kile unachokiona wewe ni sahihi basi wengine wooooote tuamini.

Kumsema Lowassa sasa hivi ni sawa na Kelele za Mbu nje ya neti.
Ameshaambiwa kuwa huko mbeleni atakuja kuwa kiongozi wa umma. Mnaoumia mkajinyonge
 
Well mkuu naona kila mwenye macho ameona nini alichokifanya EL, hatuna haja ya kuambiwa na mtanzania mmoja. Lakini tusijaribu kuwaangalia individuals tuzungumzie chama chote kwa ujumla na utaratibu wa chama wa kuwashughulikia wanachama ambao inaonekana wazi kuwa si wanachama waaminifu kwa chama na kwam nchi, hasa wale ambao ni waroho wa fedha na madaraka. Inawezekana kweli sisi ni mbu tulio nje ya net, lakini aliyemo ndani ya hiyo net asiyedhani kuwa atakaa humo siku zote. Na usishangae kuona netu inachanwa
 
JF ina vichwa vikali, natamani mngetumia majina yenu halisi mgombee uongozi labda hii nchi ingebadilika, sasa mnaongeaa tuu na hoja za nguvu then mnajificha mafichoni.
 
Safari yetu kama Taifa ni ndefu sana , ila kuna njia ya mkato watakaokubali kuipita hiyo wataweza kufika mapema na salama , ila tukiamua kuendelea na njia tunayoitumia tutaumia sana njiani na sio wote wataweza kufika kwani wanaweza hata kufa njiani kwa sababu ya njaa, kiu, magonjwa n.k.

Suala ni sisi kuamua sasa...now.....

Watanganyika ni waoga mno
Hawana uthubutu wa kudai haki zao
Hawana uthubutu wa kuwawajibisha viongozi wazembe wasiotimiza wajibu wao
Hawana uthubutu wa kusimamia mawazo yao
Hawana uthubutu wa kufanya maamuzi yenye manufaa kwa ajili yao(umma)
Hawana uthubutu wa kuwahoji viongozi wao hata kama wanawafanyia yasiyostahili
Hawana uthubutu wa kupiga kura kwa manufaa ya umma

Watanganyika hawajui wanachokifanya au wanachotakiwa kufanya ndio maana ni wepesi kudanganyika, na ndiyo sababu ya ccm kuendelea kutuburuza kila kukicha kwa kuwa kama wanavyosema ccm wenyewe na kwa sababu wana uhakika kwamba 70% wapo wapo tu. Wanajua wakiwapelekea khanga, vitenge, kofia, t-shirts, pilau, pombe za kienyeji na chumvi wanawapigia kura za kuwapa ushindi wa tsunami.

Tutake tusitake, ili kujinasua toka kwenye makucha ya ccm lazima watanganyika tubadilike, tuwe kama wenzetu wazanzibari au wakenya!!

Kazi kubwa tuliyonayo ni kuhakikisha kwamba wana JF wote hatuko miongoni mwa hiyo 70% na tuhakikishe tunawasaidia kwa kuwaelimisha wenzetu wajitambue, kila mmoja atambue thamani ya kura yake.
 
Are you among them?

Nyie ndio mnaharibu dhana nzima ya fikra..kitu cha kipuuzi kinarudia rudia eti watanzani ni waoga blah blah..

Unakumbuka watanzania walivyoamka wakati wa mrema! mimi naamini watanzania wanaweza na wanaosema hayo wana ajenda zao kutulemeza kifikra na kutukatisha tamaa tena kwa makusudi

Hatuna viongozi wanaoaminika ambao tutakuwa tayari kufa kwa ajili yao..tunasumsubir mandela wetu soon atakuja!
 
Acha porojo, Mandela ni mmoja tu yuko Sauzi.

Kwa taarifa yako mimi nilishaacha kuwapigia kura wagombea wa chama cha mafisadi long time ago na ninaendelea hivyo hivyo kila uchaguzi pasipo kukosa!
Na mwaka huu panapo majaliwa nitapiga kura ya mabadiliko ya kweli.

Nyie mlikuwa na Nyerere(JK1), na sasa mnae Kikwete (JK2) na mtaendelea na JK zenu miaka nenda rudi.

Watanzania hamjaamka, tena sasahivi ndio CCM imewafunika Blanketi nzito ( Unaifahamu blanketi ya Raymond toka kenya miaka ileeee).

Kama unabisha kwamba watanganyika sio waoga, tukumbushane hapa hapa ikifika Nov.2010 nani kashinda uchaguzi kwa Tsunami kama sio hao hao mafisadi.
 
Chama kimepitia misukosuko mingi toka 1977. Hali ya hewa ilichafuka. Ikasafishwa. Kiberiti kilitingishwa. Kikapumzishwa. Kelele zimepigwa. Zimetulizwa. Kigumu Chama! Kidumu!

"Chama hiki Mapinduzi
Kimeleta mageuzi:
Si Chama pekee tena,
Viko aina aina.

Na Chama cha Mapinduzi,
Watambue Viongozi,
Ni Chama cha Muungano,
Si Chama cha Utengano.

Kama mwanachama wake
Hazipendi sera zake,
Atoke, asichelewe,
Aanze chake mwenyewe.

Kama Viongozi wetu
Hawapendi sera zetu,
Watoke waende zao,
Waanzishe vyama vyao.

Viko vyama bozibozi
Vyatafuta viongozi,
Waende waviongoze,
Na hiki tukipongeze!

WASITEKE CHAMA NYARA
WAKILAZIMISHE SERA
AMBAZO KATU SI ZAKE
NI ZA WAPINZANI WAKE."

- JK Nyerere, Tanzania! Tanzania!
 
.

Kwanza heshima mbele Mzee FMES, pili asante kumbe na wewe sasa ndio umeliona hili tangia jana! na sasa unasimama uhesabiwe kwa kusema enough! .

Mzee Mwanakijiji alishayaona hayo kitambo na ameshaandika sana. Mimi ni miongoni mwa waumini kuwa really changes must come from within otherwise ni superficially.

Kesema ukweli, post kama hii, toka kwa mtu kama wewe, huu sasa ndio uthibitisho wa true and genuine patriotism kwa nchi yako kwa kuweka maslahi ya taifa mbele beyond party politics.

Niko hapa Dodoma, wale tuliokuwa na mategemeo nao, ndio hao tena wamekuwa wamoja, wapiganaji ndio washafisha mafisadi, and now they sail the same boat united as one.

My opinion, kusubiri CCM imeguke its just a wishful thinking na tutangoja milele!. Something has to be done now more than ever, sasa ni nini cha kufanyika, lini na namna gani, is subject to more discussion to follow ila
Mzee umesikika sasa ni bado tuu kusimama nawe uhesabiwe!

"Together we can, bring the changes we can believe in"... Yes we can!

Asante

Pasco.
Field Marshal kasema kweli, CCM ni tatizo kubwa. umasikini wetu ni chama hiki kuwepo madarakani kwa muda mrefu. Chama kisichotaka democrasia ya kweli.
Kimeteka wasomi, wafanyabiashara, walimu hasa wa primari, watumishi wa umma.

Kusubiri CCM kumeguka, itachukua muda mrefu sana. Napendekeza tusaidie kukimega au kukiua kwa ajili ya maslahi ya Tanzania. Njia zifautazo zitumike kukiangusha:-
1. Tuwaambie ukweli wanaCCM kwamba ni vigumu sana sera zao kuleta maendeleo.
2. tuwanyime kura na wakiiba tuwaumbue kwa mbinu za kikachero
3. Tuwaelimishe watanzania kukataa rushwa za kanga, pilau, na yafananayo na hayo
4. Tuviunge vyama vya upinzani vyenye mwelekeo
5. Tuwe na ujasiri kutetea taifa letu hata ikihatarisha maisha yetu.
6. Tuwe badiliko kwanza badala ya kusubiri badiliko.
7. Tuihabarishe jamii ya Watanzania kwa njia mbalimbali
8. Tuwazomee mafisadi ambao wamekumbatiwa na ccm
9. Tushirikishane njia zinazosaidia CCM kufa siyo kumeguka.
10. Tuone miaka 33 ya ccm madarakani yanatosha

Tushirikiane kukiua ccm maana chimbuko la umaskini wetu.
 
Njia pekee ya kuiadhibu CCM ni kutafsiri hasira zetu kwa vitendo.Na kwa bahati nzuri,nafasi ya kufanya hivyo inakarabia: OKTOBA 2010.
 
Nchi ilikofika sasa inahitajika MAPINDUZI ya aina yoyote hata ikibidi ya silaha kuiondoa serikali ya CCM madarakani. Vinginevyo kama tunasubiri kura ndo zituokoe basi tusubiri miaka 10 au 20 ijayo ambapo itakuwa "too late"...tutakuwa tumeishasagika saaana tu!
 
Sasa kama Lowassa hana makosa mnalazimishaje awe nayo? Tatizo lako Field Marshals unataka kile unachokiona wewe ni sahihi basi wengine wooooote tuamini.

Kumsema Lowassa sasa hivi ni sawa na Kelele za Mbu nje ya neti.
Ameshaambiwa kuwa huko mbeleni atakuja kuwa kiongozi wa umma. Mnaoumia mkajinyonge

- Kwa maneno yako inaonekana tatizo lako ni kujisikia kila ninachosema ni sahihi, siwezi kukusaidia kwa hilo,

- Lowassa hawezi kusafishika ni mchafu sana, anahangaika tu ndio maana Rostam analilia majaji maana anajua kwamba sheria iko pale pale! na kumbuka taifa la Tanzania ni kubwa sana kuliko one person Lowassa! we are past him tena longtime ago!

Respect.

FMEs!
 
Field Marshal kasema kweli, CCM ni tatizo kubwa. umasikini wetu ni chama hiki kuwepo madarakani kwa muda mrefu. Chama kisichotaka democrasia ya kweli.
Kimeteka wasomi, wafanyabiashara, walimu hasa wa primari, watumishi wa umma.

Kusubiri CCM kumeguka, itachukua muda mrefu sana. Napendekeza tusaidie kukimega au kukiua kwa ajili ya maslahi ya Tanzania. Njia zifautazo zitumike kukiangusha:-
1. Tuwaambie ukweli wanaCCM kwamba ni vigumu sana sera zao kuleta maendeleo.
2. tuwanyime kura na wakiiba tuwaumbue kwa mbinu za kikachero
3. Tuwaelimishe watanzania kukataa rushwa za kanga, pilau, na yafananayo na hayo
4. Tuviunge vyama vya upinzani vyenye mwelekeo
5. Tuwe na ujasiri kutetea taifa letu hata ikihatarisha maisha yetu.
6. Tuwe badiliko kwanza badala ya kusubiri badiliko.
7. Tuihabarishe jamii ya Watanzania kwa njia mbalimbali
8. Tuwazomee mafisadi ambao wamekumbatiwa na ccm
9. Tushirikishane njia zinazosaidia CCM kufa siyo kumeguka.
10. Tuone miaka 33 ya ccm madarakani yanatosha

Tushirikiane kukiua ccm maana chimbuko la umaskini wetu.

Good ideas...........yet the bucks still stops with us........HOW?
 
Lazima tufanye maamuzi magumu ya kujitoa mhanga kama tunataka kuiokoa nchini yetu. mkuu ogah ninachokiongelea kwa hali tuliyofikia hapa watanzania ni kwamba kwanza lazima tutenge muda wetu kwa ajili ya kulitetea taifa letu na pili tutenge kiasi kadhaa cha pato letu katika kulitetea taifa letu. maneno matupu hayavunji mfupa. tukiendelea kupiga jarambi jf, kwenye stuli ndefu na vijiweni bila kuchukua hatua yoyote madhubuti tutalalama mpaka povu litutoke na hamna mabadiliko yoyote ya maana yatakayotokea isipokuwa mafisadi wataendelea kutanua na kuiangmiza nchi. lazima tuwe tayari kujitolea pesa na muda, hamna njia ya mkato. hivyo ni vitu nyeti na muhimu sana kwetu lakini ndivyo vinavyohitajika katika vita hii.

tuache mazoeya la kulaumu na kukubali kwamba tatizo ni sisi. tatizo cio ccm, ccm imekuwa hivyo kwa kuwa tumeilea na kuijengea mazingira ambayo yameruhusu iwe hivyo. tatizo sio wapiga kura wanaonunuliwa kwa khanga na chumvi, wao uwezo wao wa kufikiri hauwaruhusu kuona kwamba wanayofanya ni makosa. tatizo ni sisi wenyekujua kwamba kuna maovu yanatendeka tanzania lakini hatuchukui hatua yoyote zaidi ya kulalamika. tunaweka maslahi yetu mbele sana kabla ya maslahi ya taifa. Kuchangia harusi ya mtoto wa shangazi ni muhimu sana kwetu kuliko kumchangia dk slaa aweze kushinda uchaguzi arudi bungeni kututetea. Kuhudhuria mechi ya simba na yanga ni bora kwetu kuliko kupoteza muda kwenda kuwaelemisha watanzania wenzetu wasiokuwa na uelewa waweze kufanya maamuzi ya busara siku ya uchaguzi. hatutaki kupoteza muda kuingia kwenye vyama vya upinzani tuvipe changamoto vikomae vipambane na ccm tunasubiri kwanza vikomae vyenyewe vipendeze au wefukuzwe wengine waunde ccj ijijenge ndipo nasi tujihusishe. hatutaki kuhudhuria maandamano ya kukemea uovu unafanywa na watawala wetu tukihofia tukionekana ajira zetu zitakuwa matatani. sisi wenye uwezo wa kufikiri au tulioenda shule tunajua tatizo ni nini na tunauelewa wa kujua ni njia gani ya kulitatua. tayari tumeshatoa fikra, hisia, mawazo na maneno sasa ni wakati wa kutoa muda wetu na pesa yetu. Tumia akili yako fikiria ni wapi unaweza kuekeza muda wako na pesa yako katika kulikomboa taifa letu na ufanye hivyo.

Hatua ya kwanza ni fikra na maneno, ya pili ni pesa na muda, ya tatu kama vyote vitashindikana ni kujitolea maisha yako ili uweze kujikomboa. Wapo watanzania sasa hivi ambao wameishiwa fikra, hakuna mahali malalamiko yao yanasikilizwa, hawana pesa na muda wao wote unatumika kuwatumikia wengine, wao kujitolea maisha yao si uamuzi mgumu. Tusipoingia kwenye vita hii wakati huu basi wao watatuingiza kwenye vita yao penda tusipende pindi ustahimili wao utakapoisha.
 
Sisi wenyewe humu JF hatuna tofauti kabisa na viongozi wa CCM. Hatuna tunalolisimamia. Tunadhani kwamba mle ndani ya CCM iliyooza kwa kiwango kile bado wamo viongozi safi kabisa. Tunawafagilia na kuwasifu sana. Hivi kweli kiongozi safi, mwadilifu anaweza kuwa CCM? Anafanya nini kwenye uozo huo?
Mmewaona mashujaa wenu wanakoishia sasa?
 
Lazima tufanye maamuzi magumu ya kujitoa mhanga kama tunataka kuiokoa nchini yetu. mkuu ogah ninachokiongelea kwa hali tuliyofikia hapa watanzania ni kwamba kwanza lazima tutenge muda wetu kwa ajili ya kulitetea taifa letu na pili tutenge kiasi kadhaa cha pato letu katika kulitetea taifa letu. maneno matupu hayavunji mfupa. tukiendelea kupiga jarambi jf, kwenye stuli ndefu na vijiweni bila kuchukua hatua yoyote madhubuti tutalalama mpaka povu litutoke na hamna mabadiliko yoyote ya maana yatakayotokea isipokuwa mafisadi wataendelea kutanua na kuiangmiza nchi. lazima tuwe tayari kujitolea pesa na muda, hamna njia ya mkato. hivyo ni vitu nyeti na muhimu sana kwetu lakini ndivyo vinavyohitajika katika vita hii.

tuache mazoeya la kulaumu na kukubali kwamba tatizo ni sisi. tatizo cio ccm, ccm imekuwa hivyo kwa kuwa tumeilea na kuijengea mazingira ambayo yameruhusu iwe hivyo. tatizo sio wapiga kura wanaonunuliwa kwa khanga na chumvi, wao uwezo wao wa kufikiri hauwaruhusu kuona kwamba wanayofanya ni makosa. tatizo ni sisi wenyekujua kwamba kuna maovu yanatendeka tanzania lakini hatuchukui hatua yoyote zaidi ya kulalamika. tunaweka maslahi yetu mbele sana kabla ya maslahi ya taifa. Kuchangia harusi ya mtoto wa shangazi ni muhimu sana kwetu kuliko kumchangia dk slaa aweze kushinda uchaguzi arudi bungeni kututetea. Kuhudhuria mechi ya simba na yanga ni bora kwetu kuliko kupoteza muda kwenda kuwaelemisha watanzania wenzetu wasiokuwa na uelewa waweze kufanya maamuzi ya busara siku ya uchaguzi. hatutaki kupoteza muda kuingia kwenye vyama vya upinzani tuvipe changamoto vikomae vipambane na ccm tunasubiri kwanza vikomae vyenyewe vipendeze au wefukuzwe wengine waunde ccj ijijenge ndipo nasi tujihusishe. hatutaki kuhudhuria maandamano ya kukemea uovu unafanywa na watawala wetu tukihofia tukionekana ajira zetu zitakuwa matatani. sisi wenye uwezo wa kufikiri au tulioenda shule tunajua tatizo ni nini na tunauelewa wa kujua ni njia gani ya kulitatua. tayari tumeshatoa fikra, hisia, mawazo na maneno sasa ni wakati wa kutoa muda wetu na pesa yetu. Tumia akili yako fikiria ni wapi unaweza kuekeza muda wako na pesa yako katika kulikomboa taifa letu na ufanye hivyo.

Hatua ya kwanza ni fikra na maneno, ya pili ni pesa na muda, ya tatu kama vyote vitashindikana ni kujitolea maisha yako ili uweze kujikomboa. Wapo watanzania sasa hivi ambao wameishiwa fikra, hakuna mahali malalamiko yao yanasikilizwa, hawana pesa na muda wao wote unatumika kuwatumikia wengine, wao kujitolea maisha yao si uamuzi mgumu. Tusipoingia kwenye vita hii wakati huu basi wao watatuingiza kwenye vita yao penda tusipende pindi ustahimili wao utakapoisha.

Jembe............tatizo letu (kwa mtizamo wangu) si ideas ya nini tufanye...........ideas ziko nyingi sana sana.....nzuri kwa ajili ya Taifa letu..........lakini tuna watu mediocre wamepanda through the system to the top positions ndio wanotuamulia UJINGA na UJAMBAZI unaoendelea...............

.......nimefurahi though kuona mapendekezo yako kuhusu swali langu "How?".....Pesa na Muda.......thats Ok with me.........but ........wazo la kujitolea maisha.......can you please fafanua/dadavua..........
 
KANU ya kenya ilikuwa kubwa vilevile, USSR likuwa kubwa vilevile..sioni sababu yoyte ya kuogopa ukubwa wa CCM tatizo wapambanaji (wanaojiita) hawapambani ila wanafanya maigizo kwa sababu (interest) zao na za kikundi chao so hawana mshiko kwenye jamii iliyo pana na kubwa.

Itafika siku na iko karibu Wanamchi watashindwa kuvumilia na kwenda barabara kwa nguvu wakiongozwa na watu wenye kulnda kwa dhati maslahi yao kuliko hawa wanaojiita wapiganaji (wasanii)

Mkuu, kwa upande wa KANU (Kenya), waliokuja kuwa wapinzani wake ni wale wale waliokuwa viongozi wakuu wa chama hicho. Walichokifanya wakati ule ni kuanzisha vyama vingine (upinzani) na kushindana na KANU. Vile vile, kushindwa kwa KANU kulifanyika kwa mbinu ya viongozi wa KANU wa juu kabisa. Kwa mfano,

1. Rais aliekuwa akimaliza muda wake alipendekeza na kushinikiza Uhuru Kenyatta kuwa mgombea uRais akijua kuwa hakuwa na uzoefu mkubwa wala ukubalikaji wa kutosha kwa wananchi.

2. Muda mfupi kabla ya uchaguzi 2002, Rais aliekuwa akiondoka madarakani alifanya kikao cha siri na Rais wa sasa alipokuwa hospitali akitibiwa kutokana na ajali ya gari. Walichokubaliana ni siri hadi leo.

3. Sheria za uchaguzi ziliruhusu vyama kuanzishwa na kushiriki uchaguzi hata kama kina siku chache tangu kusajiliwa.

Mambo kama hayo na mengine, ndio yaliyochangia kuangushwa kwa KANU na hadi sasa kiko hoi.

Kwa upande wa Tanzania, sheria za uchaguzi na muundo wa vyama vyetu hauko sawa na ule wa Kenya (japokuwa Kenya nao wanafanya mabadiliko ya Katiba kuweka hali kuwa ngumu kuanzisha vyama siku chache kabla ya uchaguzi, ama kuhama vyama na kubaki kuwa Mbunge, n.k).

Ni vigumu sana kwa viongozi wa juu kabisa wa CCM kuamua kuanzisha
chama na kipya na chenye uwezo wa kushiriki uchaguzi na kushinda kwa kishindo.

Vile vile, profiles za viongozi wa upinzani, uwezo wao kushawishi na kiuchumi, hautoi changamoto inayotegemewa kwa CCM.

Safari ni ndefu, ila nadhani tutafika. Matumaini yapo kwa kuwa, kwanza vyama vya upinzani vinaendelea kupata uungwaji mkono (japo kidogo). Wananchi wanaanza kuviamini na vikiamua, vinaweza kujiunda kutoa upinzani wa kweli.

Ila vikubali kuendelea kupambana katika hali ngumu iliyopo sasa bila kuchoka. Vile vile viamue kutoa fursa sawa kwa wanachama wake ili kushiriki kugombea nafasi za juu kabisa za nchi.
 
Back
Top Bottom