Taifa imara hujengwa katika misingi ya HAKI, HESHIMA, UHURU na UMOJA!

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kila binadamu anastahili kuwa na Taifa lake. Anastahili kuwa na nyumba yake na familia yake. Taifa kama nyumba ni lazima vijengwe juu ya matumaini na upendo.

Familia ina haki ya ukuaji kama Taifa lilivyokuwa na haki ya ukuaji.

Familia imara inategemea sana mahusiano baina ya baba na mama na majukumu ya pamoja katika malezi na makuzi lakini pia katika kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kujenga uchumi wa familia. Umoja katika familia ni muhimu kama ulivyo umoja katika Taifa. Pale wanafamilia wanapounganishwa na emotion au feelings za upendo baina yao na sense of duty for each other. Bond yao it determine their future.

Familia lazima iwe na maono kama ilivyo kwa Taifa. For any great man kumpenda mke wake ni responsibility, '' A DUTY OF HONOR'' This Courage within, to protect and to care for the familly, is the responsibility of each man on the earth. Mwanaume anaposhindwa kuunganisha familia yake ni udhaifu mkubwa sana.

Hii ni sawasawa na kwa Taifa any great leader, matumaini yake na dhamira yake ni lazima iwe kuunganisha watu wake, kuwafanya watu wake wapendane, wawe wamoja.

Kwahiyo hii bond katika familia inapokuwa strong enough na itakapo panuka na kama kila mtu akiwajibika ipasavyo Taifa lazima litanyanyuka.

Kwahiyo makuzi ya watoto wetu ni muhimu sana katika ujenzi wa Taifa imara. Mtu yeyote anayeangamiza familia au kuhiharibu ana haribu kiini cha Taifa. Kuna uhusiano mkubwa kati ya familia imara na Taifa imara.

Uongozi unaanzia katika familia. Watoto lazima wakushimu kama baba katika familia kwa matendo yako ni lazima uwa tiishe watoto wako na uwafundishe maana ya maisha na jinsi ya kuishi lakini pia ni lazima tuwafundishe utanzania. Tutafsiri upya utanzania. Hawa watoto ndio viongozi wa kesho tusipowafundisha katika maadili nchi yetu itapotea. Ni lazima tuwakuze katika wajibu, wao ndio watakao linda Taifa hili. Ni lazima tuwakuze katika wajibu na umoja.

Taifa hili lina kiu. Linahitaji watu wake bora kuliokoa.

Ni lazima tuwe na dira kama Taifa na ni lazima tujue tunapoelekea. Na katika safari hii ni muhimu kutomuacha mtu yeyote kwakuwa sisi ni Taifa moja.

Kwahiyo jukumu letu kubwa ni kujenga familia imara na kuunganisha hizo familia na kuunda jamii ambazo ziko imara na zinazoshirikiana kujiletea maendeleo yao wenyewe. Ni muhimu bila kupendana wenyewe kwa wenyewe hatuwezi kujenga Taifa hili.

Kama tusivyojali familia zetu hatujali jamii zetu katika upendo uliokamilika. Hatuwezi kuiikimbia hii ni nchi yetu ni lazima tupambane na changamoto hizi. Tupendane na tujue tuna jukumu moja la kujenga Taifa hili.

Haya mambo ya kujenga mahusiano yetu ni muhimu kabla hata hatujazungumzia masuala ya kiuchumi. Tunahitaji nguvu ya pamoja na tunahitaji watu wenyewe kujitolea kulijenga Taifa lao kwa mapenzi yao na uaminifu. Hatutafanikisha hili pasipokujenga mahusiano yetu na kuaminiana.

Lazima tutambue sisi ni wamoja hatuwezi kuendesha Taifa hili kwa propaganda kitu tunachoitaji ni maendeleo yetu. Tusiligawe Taifa hili kwaajili ya maslahi ya muda mfupi na kuweka rehani baadae yetu. Ni lazima tulipende Taifa letu na tuwe na mtazamo wa kuona mbali. Ni lazima tuwajengea baadae bora watoto wetu kusiwe na uadui miongoni mwetu bali urafiki.

Kwahiyo baadae yetu itategemea sana ubora wa elimu tutayotoa kwa watoto wetu na makuzi yao. Bila maadili hatutaweza kulilinda na kulikuza Taifa hili. Ni lazima tufikiri sasa kuhusu uzalendo na ujenzi wa jamii zetu. Ni lazima tufikiri sasa kuhusu Utaifa. Enzi za ubinafsi lazima iishe haisaidii kitu na wala hailetei furaha Taifa bali manung'uniko na chuki. Tunahitaji mabadiliko ya akili na moyo. Njia tunayopitia sasa hivi sio salama haitotupeleka mbali ni njia ya vita na mapigano hatutaweza kujenga na kulilinda Taifa hili katika mwelekeo wa ubinafsi.

Ni wajibu wetu kujenga shule bora. Kujenga hospitali bora. Kutumia fedha vizuri kwa maufaa ya Taifa na sio anasa. Nahitaji viongozi wetu wabadilike tumewapa dhamana walete maendeleo yetu sio kujinufaisha wao. Tujenge Taifa hili kwa pamoja tuna watu maskini sana wanahitaji msaada.

Kwa wananchi wanawajibu wa ujenzi wa Taifa hili ni lao. Sio tu kuisubiri serikali bali kufanya kazi kwa bidii. Kutafuta maarifa na kuwa raia wema. Ni juhudi zetu pekee zitakazo tufanya tutoke hapa tulipo. Kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kufikiri tukiongozwa na uzalendo wetu na ndoto yetu ya kuwa Taifa linalo heshimika na lenye nguvu. Tuna uwezo wa kulibadili Taifa hili. Ni jitihada zetu na umoja wetu utakao tukomboa.

Serikali inawajibu wa kuwasaidia watu wanaoonyesha jitihada za kulinyanyua Taifa hili na wenye mawazo chanya. Wana jukumu la kutengeneza mazingira mazuri kwa vipaji kukua.

Ni ukweli usio pingika ili Taifa hili likue tunahitaji mabadiliko ya fikra. Mabadiliko ya mawazo yetu. Tukibadilisha mawazo yetu tutabadilisha mwelekeo wa maisha yetu na wa Taifa kwa ujumla. Tumaini litarudi tena miongoni mwetu. Ni lazima kama Taifa tufanye yaliyo sahihi na kila mtu atengenezewe mazingira ya kukua na kuwa na maisha mazuri yasiyokuwa na wasiwasi wa baadae ataishije au atakula nini. Ni lazima tujenge Taifa kuwa sehemu ambayo haki inalindwa na kuendelezwa na vizazi vyote. Katika matumaini haya ni lazima tuishi na tulijenge Taifa hili katika misingi imara ambayo Tumaini litadumishwa. Bila matumaini hatutawza kukua kama Taifa. Sisi ni watu wamoja na baadae yetu ni moja.

Ni lazima tujenge Taifa linalo heshimu utawala wa sheria sio tu kwa kuogopa adhabu bali kwa mapenzi kwa Taifa. Kwa mapenzi kwa raia wenzako. Taifa imara hujengwa katika misingi ya Haki, heshima, uhuru na umoja sehemu ambayo tumaini litaendelezwa na litamea daima mioyoni mwa watu.
 
Karibu mkuu.

Hapa bongo watu wanafanya kazi sana mkuu, tena wanchapa kazi kwelikweli. Lakini kama uko nje jaribu kwanza kufikiri yaliyomkuta Tido Mhando, au Daudi Balali.

Siku hizi ukisema haki Tanzania kama huna hela unajisumbua

Heshima, heshima kama huna hela huheshimiwi.

Uhuru.....9 Dec

Umoja...Muungano unaelekea kubaya, udini unaiva, etc etc

Kwa hiyo ujue kabisa kwa kazi ni kubwa.
 
Hapa bongo watu wanafanya kazi sana mkuu, tena wanchapa kazi kwelikweli. Lakini kama uko nje jaribu kwanza kufikiri yaliyomkuta Tido Mhando, au Daudi Balali.



Siku hizi ukisema haki Tanzania kama huna hela unajisumbua

Heshima, heshima kama huna hela huheshimiwi.

Uhuru.....9 Dec

Umoja...Muungano unaelekea kubaya, udini unaiva, etc etc

Kwa hiyo ujue kabisa kwa kazi ni kubwa.

Nchi hii itabadilishwa na mimi na wewe.
 
wapo baadhi ya watu wanajitolea kujenga nchi ila kuna wajinga baadhi wanakwamisha jitihada za hao waleta maendeleo mfano unataka kufungua kampuni ukienda BRELA unaambiwa utoe kidogo mshiko ili mambo yako yafanikiwe sasa mtu unashindwa kujua nini kazi ya hao maofisa hapo ofisini kwao..

bado tunahitaji mabadiliko ya hali ya juu sana..


#ChangeNiMimiNiWeweNiSisi
 
wapo baadhi ya watu wanajitolea kujenga nchi ila kuna wajinga baadhi wanakwamisha jitihada za hao waleta maendeleo mfano unataka kufungua kampuni ukienda BRELA unaambiwa utoe kidogo mshiko ili mambo yako yafanikiwe sasa mtu unashindwa kujua nini kazi ya hao maofisa hapo ofisini kwao..

bado tunahitaji mabadiliko ya hali ya juu sana..


Ni kweli kabisa mkubwa tuna hitaji mabadiliko makubwa katika nchi yetu ili tuweze kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom