Taifa hujengwa kwanza katika mahusiano ya watu. Na mahusiano hayo yanapobomoka ndio mwanzo wa vita, vurugu na fujo

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Wakati mwingine tunafikiri hasi kuhusu sisi wenyewe. Hii ni hatari sana kwetu. Tukifikiri hasi kuhusu sisi wenyewe tunazuia ukuaji wetu na tunajidumaza. Pengine tunapaswa kukaa na kujitafakari kwa kina tunajichukuliaje na ni kweli hivyo tunavyojichukulia ndivyo tulivyo? au mawazo yetu yanatufanya jinsi tulivyo kwa kufikiri hasi kuhusu sisi wenyewe? Na tunajua kwamba mawazo yana nguvu kubwa ya uumbaji. Mawazo yanatengeneza tabia na matendo yetu. Jinsi tunavyojichukulia ndivyo jinsi tutakavyotenda.

Matendo yetu ni taswira ya utu wetu wa ndani eg mawazo yetu na hisia zetu pengine na matamanio yetu. Lakini binadamu hapaswi kuongozwa na matamanio yake bali fikra zake. Tukiendekeza matamanio yetu hatutaweza kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Maamuzi yetu hayapaswi kuongozwa na tamaa, hasira au matamanio bali fikra.

Kwahiyo ni wajibu wetu kufikiri kabla ya kutenda kwasababu mwelekeo wetu na majaliwa yetu hutegemea hilo. Kwa matendo yetu tunavuna tunachopanda. so our conduct is something we must look closely. so watu wanatuhukumu kulingana na matendo yetu. Upumbavu wetu au hekima zetu huonekana katika jinsi tunavyotumia akili zetu kwenye kufanya maamuzi. Upumbavu na hekima uko katika vitu viwili utumiaji wa akili kwenye kufanya maamuzi.

Na maamuzi yetu ni kama mimba huzaa matunda. Na maamuzi mengine yana gharama kubwa mno kwenye maisha. Lakini tunajua kwamba maamuzi mazuri huleta amani na utulivu. Kwahiyo usiwe na haraka unapotaka kufanya maamuzi muhimu chukua muda wako kutafakari. kwahiyo mwelekeo wako na hatma yako inategemea uwezo wako wa kuamua mambo.

Maisha uliyonayo ni creation of your own mind. so we must ask ourselves if we use our mind correctly? je our mind is good servant to us or not? Je tunatumiaje akili zetu for good or for evil? inategemea jinsi gani tuna direct akili zetu na matokeo hutokea katika mwelekeo huo. Kama tunaongoza akili zetu katika kutafuta amani tutaipata amani kama fujo tutaipata fujo. Inategemea jinsi tunavyoongoza akili zetu na mavuno yetu hufuata kulingana na akili zetu. mithali hii ni ya kweli tutavuna tunachopanda. Ukipanda amani utavuna amani.

Vitu vyote tunavyoviona vizuri na vibaya ni matokeo ya fikra zetu. So fikra mbaya huzalisha mambo mabaya. Kwahiyo ni wajibu wetu kufikiri mawazo mazuri na kuwaza chanya na kupeleka mawazo yetu mwelekeo huo. Kuna vitu vingi vizuri ambavyo akili za binadamu zimefanya. kwanfano sasa hivi natumia kompyuta, nina simu , tumeweza kuunda ndege na kujenga nyumba nzuri.

Tumeitwa kutenda mema na yenye tija katika dunia hii na kuifanya dunia hii mahali pazuri pa kuishi. Lakini matumizi mabaya ya akili zetu uharibu dunia tuliyo nayo . so fujo vita, vurugu na kutoelewana huletwa na matumizi mabaya ya akili. so ubinafsi umekuwa sehemu ya binadamu na shida kubwa kwetu. kwasababu hiyo harmony imekuwa shida kwetu. so love and care for other human beings inaanza kuyayuka taratibu and materialism kushika kasi ambayo ni pacha na ubinafsi.

Na hakutakuwa na amani kama watu wakiwa na fikra zenye mwelekeo huo. I believe we are born to serve each other and to cooperate among ourselves. We can not win anything if we are not one. So the spirit of friendship is important to us. I believe we must look each other as brothers and respect each other. Kama tutakuwa na aina hii ya mawazo tutaunda taifa bora. We can not win any war iwe vita ya kiuchumi kupambana na umaskini au vita na adui yeyote mwingine kama sio wamoja, kama hatuheshimiani na kama hatuonani kama brothers, Lazima tufikie kwenye kuelewana kwetu. Hatutakuwa na dira kama hatuelewani.

Na kuelewana kunakuja kwa kuheshimiana kwetu na kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko maslahi yetu binafsi na maslahi yetu ya makundi. Ni muhimu kuwa na mtizamo huu tunajenga taifa, Na msingi wa kwanza wa taifa ni mahusiano ya watu wake. Na kunapokuwa hakuna haki katika taifa mahusiano ya watu hutetereka na amani huwa mashakani. so we need viongozi wenye busara ili taifa hili liendelee kuwa stable. We can not have order kama hatuna viongozi wenye vision na hekima.

I hope watu mnaonisoma mnanielewa ninachozungumza haya mambo ni very sensitive. So sisi tupo leo hapa kwenye nchi hii kesho watakuja wengine lakini itategemea sana misingi tuliowajengea ni imara kiasi gani. Our stability depend on how we despense justice with no partiality. As leader if you do that people will trust you. I believe we gain strength by doing justice.

Lazima tuanze kuwa na uhusiano mzuri sisi wenyewe kwanza kabla ya kuwa na uhusiano mzuri na wengine na taifa kwa ujumla. Kama tunajichukia ni vigumu sana kupenda wengine na hata kulipenda taifa lako. Utatamani liharibike tu. Ni vigumu kuwa na uhusiano mzuri na wengine kama huna uhusiano mzuri na wewe mwenyewe. Kwahiyo ni muhimu kujenga uhusiano mzuri na wewe mwenyewe ambao utakusaidia kuwa na uhusiano mzuri na jamii inayokuzunguka.

Na taifa hujengwa kwanza katika mahusiano ya watu. Na mahusiano hayo yanapobomoka ndio mwanzo wa vita, vurugu na fujo. Na hii ni sawa tu na mahusiano ya taifa moja na jingine. Taifa lazima lijenge mahusiano yake ya ndani kuwa bora kwanza ndipo watakapokuwa na mahusiano mazuri yasiyo na unafiki na mataifa mengine. Skill ile ile ndio inayo apply. You can not love other if you do not love yourself.
 
You know very well that our nation is the product of brutal colonization. So sometimes you need some sorts of fujofujo to keep things going.
 
You know very well that our nation is the product of brutal colonization. So sometimes you need some sorts of fujofujo to keep things going.
Hahaha. So why Tuliopigania uhuru?
 
Sio kwamba walitosheka?

I think at some point our colonial masters realized that colonizing a group of people is a mammoth undertaking. So they came up with a brilliant idea. They give us independency, but they retained the economic means.
 
I think at some point our colonial masters realized that colonizing a group of people is a mammoth undertaking. So they came up with a brilliant idea. They give us independency, but they retained the economic means.
So tunatokaje hapo tuje na plan?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom