aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 792
- 1,144
HAWANA makosa wametutoka, hawakutaraji walipotoka, yakawakuta ya kuwakuta. Hawa watoto si wa fulani. Ni watoto wapendwa kweli, wa letu taifa. Wamepotea pwa hatwewaona tena.
Aah innalillah Wainnaillayh Rajuun, ndio. Twapaswa kujua tena na tena kwamba; yule alowaleta ardhini, ndo huyo alowarudisha wapotoka. KweTu ni kumshukuru yeye Rabbana kaamua. Tuseme ewe Mwenyeezi Mungu wabariki kwa wema kule waliko. Amiin.
Tunaomboleza. Tatizo tunaomboleza huku wengine wakisahau majukumu yao ya kufariji. Wakaa pembeni, labda katikati ya majumba yao makubwa na kutoa salamu lakini hawajisogezi msibani.
Ila tuache lipite; kwanza hilo si muhimu. Haya mambo ya kijamii haya, yategemea mtu ulikotokana huko. Mtu hawezi kupenda ngoma leo kwa sababu kawaona kinamama wa Kizaramo wamepita mtaani kwake wakinengua midundo ya singeli. Lazima awe na mapenzi ya ngoma tangu enzi.
Rafiki yangu mmoja Zanzibar analaumiwa sana na wenzetu kwa kutoonekana misibani au katika hafla nyingine za kijamii. Hataki au hapendi kujumuika na wenzake.
Nikauliza nyie mwamlaumu huyu mwenzetu kwani huu utamaduni wa kujumuika na wenzake katika mambo ya kijamii kama tunavyojumuika sisi alikuwa nao zamani?
Jibu lilikuaje unajua? Haa huyo tangu huko nyuma mgumu sana. Nikawauliza tena “hamumsingizii.” Ndio ukweli, hajishughulishi na mambo haya. Basi tambueni udongo upate ulimaji. Msihangaike.
Lakini wacha bwana wapo wanaume hawajifichi. Jamaa mmoja kavua ujinga akapiga yake kwamba mzee umetoa salamu kwa mbali hujafika msibani una uchungu sana kweli. Ila wafiwa wamefika na kuaga na kisha kuchukua wafu wao. Nani bora?
Nakwambia watu wengine usipime. Ukiwapa nafasi ndogo wanaitumia mpaka unashangaa. Lakini matumizi mengine ya nafasi au fursa yanakirihisha. Umepewa kipaza sauti useme machache unasema meeeeeeeengi. Tena ya ovyo ohooo. Poo Simo.
Kawaida yangu naitumia ipasavyo nafasi. Natoa mawili matatu ya kuelekeza jamii kupendana, kushirikiana na kusaidiana. Wengine wanathibitisha walivyopungukiwa hekima na busara mbele za wananchi.
Viongozi bora na bora viongozi wapi bora? Wewe unaweza kujua si unazo akili za kupambanua mchele na pumba. Tatizo watu wanajidharau wakidhani kazi ya kuelimishana ni ya waandishi wa habari peke yetu. Kila mtu na kila mwananchi anao mchango.
Unaona kwa sababu hatuna taasisi za kufundisha viongozi ndio taifa linajikuta linaendelea kuendekeza mila za zamani. Mila zipi?
Si hizi za kuamini kwamba mpaka zama hizi ni sahihi viongozi wetu tuwape dhamana ya kutuongoza kwa kigezo cha kujua KK tu. Eti ukishajua kusoma na kuandika unatpsha wewe. Nakuteua diisii au arasii au mwakilishi wa mjengoni. Basi. Just like that.
Haki ya Mungu hili taifa linaumwa. Kusoma na kuandika unakuwa mkuu wa wilaya au mkoa? Unaowaongoza wamesheheni digrii mabegani na viunoni. Usishangae mjengoni ukasikia wabonge wanasema tu ndioooooooooo.
Imepita hapo sheria bomu. Kandamizi kuliko zile za enzi za Hitler Ujarumani au Kaburu Bondeni. Au hiyo imepita sera pungufu. Imepita hapo protokali ya Afrika Mashariki isiyoshiba maslahi yetu kama taifa.
Weee nanihii njoo tena sikia. Ukae hapo ule ulwa pasina kumuangalia mtu yeyote usoni. Usiogope wala kumhofia mtu yeyote awaye. Tunakulinda katika kula ulwa wetu tulopewa na Bwana wa hili taifa. Mtizame vile; utadhani taifa la ujima.
Hili taifa linaumwa nshaamini. Wakadhani wamepata daktari. Wanashangaza na wao wanashangaa leo. Nawauliza hamkujua mzee kingungi ana akili kubwa japo kachoka? Hamkujua wale wazee wawili watatu wale nao waliyaona?
Hee unajua wewe, nimesahau mvua zimekuwa nyingi hadi watu wanasaidiwa kwa vidau kuvuka mitaa. Mvua imeshiba ardhini. Tuombe Subhana tupe mepesi mepesi mazito hatuyawezi mafukara sie. Tuhoi kila upande.
Shikamoo marahaba. Nimeubwaga kwako.