Taifa hili linahitaji kusameheana, kujenga umoja wa kitaifa pamoja na kusahau yote ya nyuma

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,208
Nimemuona Zito ametwiti kuwa iundwe tume ya kijaji kuhoji watu wote walioteswa, kuumiza na kuharibiwa mali zao wakati wa awamu ya tano.

Mimi naona nchi yetu inahitaji jambo kubwa kabisa kwa sasa nalo ni MSAMAHA KWA WOTE waliotenda maovu wakiwa katika utumishi wao.

Neno la Mungu linasema "Hakuna amri iliyo kuu zaidi ya upendo" tuwapende na kuwaombea wale wanaotuudhi maana kama tukiwachukia tunafanya kipi cha maana? ama kama tukiwapenda wale tu wanaotupenda tutakuwa tumetenda ziada gani?

Kwa maana hata waovu huwapenda wale wawapendao. Basi kama taifa tujiepushe na visasi kwa maana hiyo siyo kazi ya mwanadamu bali ya Mungu.

Ole Sabaya, Paul Makonda na wengine walifanya kazi ya utumishi wao kwa uwezo wao, mapungufu yao yameonekana kuwa makubwa basi wasamehe na taifa lipate baraka kwa toba hiyo.

Tukiweka visasi mbele basi taifa letu litaangamia maana hakuna aliye salama kuanzia kwa Spika, naibu spika, Jaji mkuu, Mwanasheria mkuu wa Serikali, Mwenyekiti tume ya uchaguzi, Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi. etc
 
Bila kujifunza kupita Tume ya ki-Jaji aliyopendekeza Mh. Zitto Kabwe basi kunauwezekano wa maovu kujirudia kupitia viongozi watakaolewa madaraka.

Tume hii ya Ki-Jaji itatufahamisha maovu yote na kuweka kumbukumbu rejea viongozi wakiapishwa na kula kiapo pamoja na semina-elekezi watakuwa wanaeleweshwa kwa mifano halisi.

Viongozi wanaapa kulinda katiba inayojumuisha mambo mengi ikiwemo kuhakikisha wanatetea haki ya kuishi, wananchi kutobaguliwa, kulinda mali za raia na kuhakikisha usalama na amani inakuwepo lakini viongozi hao wakisha chaguliwa au kuteuliwa wanasahau kiapo chao na kutufanya 'mateka' wao.

Mifano hai ya ukiukwaji wa viapo, katiba, kutesa watu, kufanyia ukatili raia itakuwepo na inayohusu Tanzania moja kwa moja katika mazingira wanayoyaishi hivyo wala hatutahitaji mifano ya Libya, Iraq, Hitler ili kuelewa ulevi wa madaraka madhara yake ni yapi na kuwa funzo la kihistoria kazi iendelee kujenga Tanzania inayojali Utu, Haki, Uhuru na Maendeleo ya watu.
 
Ukizuia watu kufahamu ukweli walivyoumizwa ipo siku watavamia hata makao ya wafu kuwaadhibu.
Kule kwa dikteta Francisco Franco walifikia kwenda kulivamia makao ya milele ya 'shujaa' wafukue kaburi la mwendazake Francisco Franco .

N.B
Habari zaidi za historia za tawala za mkono wa chuma kandamizi :
24 Apr 2018
Madrid, Spain

Mihimili ya Bunge na Mahakama za afiki kuweka historia sahihi ya dikteta Jenerali Franco wa Uhispania

Diktekta Jenerali Francisco Franco alitawala taifa hilo la Hispania kwa staili ya utawala wa 'mkono wa chuma' kwa muda wa miaka 39 hadi alipofariki dunia kwa afya dhoofu mwaka 1975.

Katika kipindi chake cha utawala wa Jenerali Franco, watu wengi walipotea ktk mazingira ya utatanishi na wengineo maelfu kufungwa jela kutokana na kuwa na itikadi tofauti za kisiasa zilizokwaza utawala wake.

Diktekta Franco alikuwa na mahusiano ya karibu viongozi wa juu wa kanisa, maana kanisa lilikuwa na ushawishi ktk maisha ya raia na pia kuunga mkono utawala wa kifalme ktk Hispania.

Jenerali Franco katika vita (1936-1939) vya wenyewe kwa wenyewe Hispania iliyoisha mwaka 1939 hakutaka kuona nchi hiyo ikiishia kumeguka ktk majimbo ya Catalonia n.k Hivyo alitumia majeshi kuhakikisha nchi inabakia bila mgawanyiko. Ushindi wa majeshi ya Franco, ulishangiliwa na kubatizwa kuwa ni ushindi dhidi ya wapiganaji wasio na imani ktk uwepo wa Mungu, Ufalme , uzalendo na umoja wa taifa.

Vita hivyo vilisababisha maelfu ya vifo na Diktekta Franco kuja na wazo la Kujenga basilica / makumbusho maalum ktk mfano wa kanisa kuwaenzi waliopoteza maisha ktk vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.

Katika wosia wake Dikteta Franco, aliomba kuzikwa ktk basilica hilo na wahanga wengine wa vita ili kujibainisha na wafu wengine waliopigania au kufa kutetea taifa hilo la Hispania lisigawanyike.

Hata hivyo miaka 43 baadaye toka kifo cha diktekta huyo, wananchi, mwanaharakati wa haki za binadamu na wanasiasa wameona kuwa ukatili uliofanyika na utawala wake haustahili kusahauliwa.

Hivyo kupitia Bunge na Mahakama wameona kuweka historia sahihi kuwa ktk utawala wa Franco kuna unyama na ukatili mwingi ulitendeka ktk utawala wake uliodumu miaka 39.

Kuhitimisha hilo, hoja ya kufukuliwa mwili wake imepitishwa Bungeni na kutiliwa uzito mahakamani kisheria kuwa Diktekta huyo hastahili kulala ktk makumbusho hayo kutokana na vitendo viovu vilivyofanyika ktk utawala wake wa kiimla.



Spanish court has for the first time authorised the exhumation of bodies from the Valley of the Fallen. It is a vast mausoleum where the fascist dictator General Franco is buried with thousands of victims of Spain’s 1936 civil war.
 
Kule nchini Iraq, dikteta Saddam Hussein sanamu yake iliadhibiwa na wananchi wenye hasira kali.
Tanzania tunaweza kuepuka hilo kwa kujifunza kupitia Tume ya ki-Jaji ya Maridhiano kwa kujifunza kuwa uongozi wa kikatili ktk ngazi zote za serikali hautakiwi.
 
Nimemuona Zito ametwiti kuwa iundwe tume ya kijaji kuhoji watu wote walioteswa, kuumiza na kuharibiwa mali zao wakati wa awamu ya tano. Mimi naona nchi yetu inahitaji jambo kubwa kabisa kwa sasa nalo ni MSAMAHA KWA WOTE waliotenda maovu wakiwa katika utumishi wao. Neno la Mungu linasema "Hakuna amri iliyo kuu zaidi ya upendo" tuwapende na kuwaombea wale wanaotuudhi maana kama tukiwachukia tunafanya kipi cha maana? ama kama tukiwapenda wale tu wanaotupenda tutakuwa tumetenda ziada gani? kwa maana hata waovu huwapenda wale wawapendao. Basi kama taifa tujiepushe na visasi kwa maana hiyo siyo kazi ya mwanadamu bali ya Mungu. Ole Sabaya, Paul Makonda na wengine walifanya kazi ya utumishi wao kwa uwezo wao, mapungufu yao yameonekana kuwa makubwa basi wasamehe na taifa lipate baraka kwa toba hiyo. Tukiweka visasi mbele basi taifa letu litaangamia maana hakuna aliye salama kuanzia kwa Spika, naibu spika, Jaji mkuu, Mwanasheria mkuu wa Serikali, Mwenyekiti tume ya uchaguzi, Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi. etc
Kwani mliwahi gombana? CCM uwajua au unawasikia?
 
Nimemuona Zito ametwiti kuwa iundwe tume ya kijaji kuhoji watu wote walioteswa, kuumiza na kuharibiwa mali zao wakati wa awamu ya tano. Mimi naona nchi yetu inahitaji jambo kubwa kabisa kwa sasa nalo ni MSAMAHA KWA WOTE waliotenda maovu wakiwa katika utumishi wao. Neno la Mungu linasema "Hakuna amri iliyo kuu zaidi ya upendo" tuwapende na kuwaombea wale wanaotuudhi maana kama tukiwachukia tunafanya kipi cha maana? ama kama tukiwapenda wale tu wanaotupenda tutakuwa tumetenda ziada gani? kwa maana hata waovu huwapenda wale wawapendao. Basi kama taifa tujiepushe na visasi kwa maana hiyo siyo kazi ya mwanadamu bali ya Mungu. Ole Sabaya, Paul Makonda na wengine walifanya kazi ya utumishi wao kwa uwezo wao, mapungufu yao yameonekana kuwa makubwa basi wasamehe na taifa lipate baraka kwa toba hiyo. Tukiweka visasi mbele basi taifa letu litaangamia maana hakuna aliye salama kuanzia kwa Spika, naibu spika, Jaji mkuu, Mwanasheria mkuu wa Serikali, Mwenyekiti tume ya uchaguzi, Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi. etc
Watu wamezushiwa kesi za uongo, akaunti zimefungwa, mabilioni yao yameibiwa, walioiba hawajakubali makosa.

Unataka wasamehe nini sasa wakati walioiba hawajakubali makosa?
 
Hapana ngojeni kwanza, sisi tulivumilia miaka mitano yote, Yani nyie miezi mitatu tu mshaanza kuomba maridhiano???

Tulishakubaliana matajiri wataishi kama mashetani na masikini kama malaika sasa upande umegeuka, mkiona mjini pagumu Kuna basi ametoa RC wa Dar la kubeba ombaomba mnaweza kuunga mkarudi mtuachie mji sasa.
 
CCM Asilia ikitaka kurejesha utengamano nchini, inabidi itambue CCM Mpya ilivyokengeuka na ijisahihishe. Ili kurejesha imani kwa waTanzania inapata kuelewa haya yafuatayo :



Katika vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania kwa muda huu 2021, CCM ni chama dhaifu kupita vyote hata cha CHAUMA chini ya mwenyekiti mzee Hashim Rungwe ni chama thabiti kuliko CCM.



Sababu ni kuwa mwendazake baada ya kuua mihimili ya dola, mahakama na bunge akamalizia kukimaliza chama kilichomweka madarakani. Muda huu CCM haina Mwenyekiti wa Taifa wala Katibu Mkuu wa chama.



Hali hii imefikiwa kwa vile CCM ilishindwa kumdhibiti mwendazake kufanya mambo yake ya kuwaondoa vigogo tishio ndani ya CCM na kuleta "wageni" na kuwazawadia vyeo kwa sharti wamuimbie mapambio anayopenda kusikia.



Kina Bashiru Ally Kakurwa, Humphrey Polepole ni aina ya viongozi ambao viongozi walikuwa hawawezi kumuambia chochote Mwenyekiti ambacho wao wanaamini kinyume na kama kina Nape Nnauye , January Makamba na hata wazee kama Yusuf Makamba, Abdulrahman Kinana.



Tukija katika dola, mwendazake aliiyumbisha na kuivuruga kabisa mfumo wa utumishi serikalini yaani civil service. Aliwachukua watu wasio na ujuzi wa utumishi serikalini na kuwapachika vyeo vya u DED, Makatibu Wakuu na kujaribu kuhitimisha pigo kuu la kuua utumishi serikalini kwa kumuapisha Dr. Bashiru Ally Kakurwa kama Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ktk historia ndiye Katibu Mkuu aliyekuwa hana uzoefu kabisa ktk utumishi wa serikali kuu.



Tukija katika mhimili wa Mahakama tuliona alivyouburuza na kuwapa vyeo vya ujaji kwa vigezo dhaifu mfano kuandika hukumu kwa kiSwahili huku kesi hiyo ikiwa ni nyepesi mno.



Bunge pia lilipelekeshwa kwa Spika kuelekezwa kuwashughulikia wabunge wake kwa kuwatoa nje ili waje kushughulikiwa na mwendazake nje ya Bunge. Wabunge wa CCM pia hawakuepuka kipigo cha kisiasa toka kwa mwendazake, ktk kuelekea uchaguzi wa 2020 walishughulikiwa na 'wajumbe' na kama waliweza kupenya walikutana na rungu la Mwenyekiti wa CCM.



Vyeo katika ngazi za uwaziri tumeona waliojiunga mwishoni ktk CCM toka vyama mbadala walitunikiwa vyeo huku wale waliokulia ktk UVCCM na Jumuiya za CCM toka utotoni wakiambulia kuwa backbenchers. Yote hii ilikuwa kuonesha CCM imekufa na sasa mtu mmoja ndiyo kila kitu hivyo wasifurukute au kuwashwa kuhoji au kutoa mawazo mbadala.



Tanzania ilikuwa inaelekea kubaya, lakini kama uzi huu ulivyotabiri wa mwana JF Mvuv, inaonekana ndani ya CCM ndiyo kulikuwa na fukuto kubwa la kutokubaliana na kinachoendelea na sasa tunasikia baada ya mwendazake kuondoka, wabunge wa CCM na SPIKA mwanaCCM wanaanza kutoa maoni ambayo yanaonekana na waimba pambio wa mwendazake kuwa ni unafiki.



Ili kuirejesha Tanzania katika mstari wa haki ikiwemo na CCM yenyewe Asilia kuweza kuaminika kusimamia haki na katiba ya nchi, Tume ya Kijaji lazima iundwe.



Tume ya KiJaji ipewe hadidu rejea Kuchunguza ukiukwaji mkubwa wa katiba, haki za binadamu na ukatili uliotendeka ktk utawala wa CCM iliyojiita CCM Mpya.
 

When Dictators Fall: Preventing Violent Conflict During Transitions from Authoritarian Rule​

Entrenched authoritarian systems are those where a leader or group has centralized power and resources in a manner that limits meaningful political and economic inclusion, instrumentalizes key State institutions, reduces democratic space and often allows a specific individual to remain in power well beyond typical constitutional limits.

This paper concerns the transitions out of entrenched authoritarian rule, the often volatile moments when new leadership comes into power. Some transitions take place peacefully, largely within constitutional order, but others may descend into civil unrest or even escalate into all-out civil war. In support the UN’s prevention mandate, this project is driven by the question, why does one country peacefully transition out of authoritarian rule while another falls into violent conflict, and what can the UN do to influence pathways away from violence?

This project draws on scholarship around authoritarianism and neo-patrimonial States as well as original research by United Nations University Centre for Policy Research into entrenched political systems. It identifies four key factors that may influence whether a transition tends to result in violent conflict:

  1. past forms of rule (democratic or authoritarian);
  2. the way in which a political system transitions (e.g. through a coup, election, death, transfer of power or popular uprising);
  3. the fate of the individual leader, including questions of personal property and accountability for human rights abuses; and
  4. economic performance and the degree of inequality within a given society
Source: When Dictators Fall: Preventing Violent Conflict During Transitions from Authoritarian Rule - United Nations University Centre for Policy Research
 
Ni kweli kabisa iundwe timu ya kijaji ya kijaji itakayo hoji watu wote na kutoa report. Hii itasaidia watu wote wenye mamlaka kutokurudia makosa. Nitakuja mfano Wangu Mdogo.

Machi 11.2020 nilikamatwa kwa maelekezo ya mkuu wa wilaya Fulani nikawekwa ndani kwa siku saba bila kosa lolote kwa sababu tu nilikuwa nagombea nafasi ya moja wapo katika moja ya chama cha wafanyakazi Tanzania.

Mkuu wa wilaya alihisi Mimi si mwanachama wa chama chake na alipo nitoa alitaka nioneshe kadi ya chama chake nami sikuwa nayo.

Nilikuja kugundua alitumia chama kama mwavuli kumbe ugomvi ulikuwa ni juu ya Binti ambaye tumegongana naye hakuishia hapo.

Julai 23. 2020 siku ya uchaguzi huo, niliitwa kwa mkuu wa wilaya, kwa SAA 1.30 asubuhi, Sikujua sababu ya kuitwa, kumbe lengo lake ilikuwa ni kunizuia nisiingie kwenye ukumbi ili nichaguliwe, nilipofika alimuita Katibu tawala, DSO, walinifungia katika moja ya chumba na kunitaka nieleze historia ya maisha yangu kwa maandishi.

Waliniacha kwenye chumba hicho siku nzima, kumbe waliandika barua kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi kuwa nimejitoa kwenye uchaguzi huo na wakaipeleka wakamsimamia akaisoma na baada ya uchaguzi walirudi na kunifungulia kisha kunitaka kuondoka hapo.

Ki ukweli awamu iliyopita ilikuwa ni ya mateso, shida na dhiki. Hivyo ninaungana na Zito kabwe iundwe tume ya kijaji kuchunguza mambo haya.
 
Hamna kusamehe mtu hapa, wakati wao wanawaingiza watu vyupa matackleni unadhani hao watu hawakuomba msamaha? Waliwasamehe? Akina Mdude wapo mahabusu mwaka mzima sasa kwa makosa ya kubumba ili kumridhisha dikteta uchwara, why hamjawasamehe? Anzeni kwanza nyie kwa kuwaachilia wote mliowabambikia kesi na kutoka in public kusema maovu yenu yote!
 
Hakuna kusamehe mtu
Kwa sheria zilitungwa kwa ajili ya wananchi wa kawaida tuu na sio viongoz pia???

Huu ni uonevu,watu wamekatwa mikono,wamipigwa misumari miguuni wameingiziwa chupa sehem za siri

Halafu unasema wasamehewe HAPANA KWA KWELI

SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimemuona Zito ametwiti kuwa iundwe tume ya kijaji kuhoji watu wote walioteswa, kuumiza na kuharibiwa mali zao wakati wa awamu ya tano. Mimi naona nchi yetu inahitaji jambo kubwa kabisa kwa sasa nalo ni MSAMAHA KWA WOTE waliotenda maovu wakiwa katika utumishi wao. Neno la Mungu linasema "Hakuna amri iliyo kuu zaidi ya upendo" tuwapende na kuwaombea wale wanaotuudhi maana kama tukiwachukia tunafanya kipi cha maana? ama kama tukiwapenda wale tu wanaotupenda tutakuwa tumetenda ziada gani? kwa maana hata waovu huwapenda wale wawapendao. Basi kama taifa tujiepushe na visasi kwa maana hiyo siyo kazi ya mwanadamu bali ya Mungu. Ole Sabaya, Paul Makonda na wengine walifanya kazi ya utumishi wao kwa uwezo wao, mapungufu yao yameonekana kuwa makubwa basi wasamehe na taifa lipate baraka kwa toba hiyo. Tukiweka visasi mbele basi taifa letu litaangamia maana hakuna aliye salama kuanzia kwa Spika, naibu spika, Jaji mkuu, Mwanasheria mkuu wa Serikali, Mwenyekiti tume ya uchaguzi, Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi. etc
Malipo ya maovu hasa mauaji ya awamu ya tano ni katiba mpya. Msamaha ni ujinga, msamaha huu hauwezi kukomesha yaliyotokea yasijirudie

Kwa maana walitenda haya kwa kibali cha katiba mbovu inayowapa mamlaka makubwa na kujiona miungu.

They must pay katiba mpya in return!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom