Taharuki Mbagala, wafanyakazi wa mwendokasi wakigoma

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,333
2,000
Taharuki imetawala maeneo ya Mbagala-Zakhem, baada ya Polisi kupiga mabomu ya machozi kuwatuliza wafanyakazi zaidi ya 1,000 wanaotengeneza barabara ya mwendokasi kugoma wakishinikiza kulipwa stahiki zao.

Tukio hilo lilitokea leo, Septemba 6,2021 baada ya Polisi kupiga mabomu hayo mara mbili asubuhi na mchana, lakini hali hiyo haikusaidia chochote zaidi ya wafanyakazi hao wa kampuni ya Sinohydro wanaotengeneza barabara ya mwendokasi kutoka Kariakoo hadi Mbagala kuendelea na msimamo wao wa kutaka walipwe chao.

Wafanyakazi hao licha ya kulipwa mishahara, wanaulalamikia uongozi wa kampuni ya Sinohydro kkushindwa kuwalipa malimbikizo ya malipo ya chakula, usafiri na makazi kwa miaka miwili sasa kama mkataba wao unavyoeleza.

Baada ya polisi kuona mbinu hiyo imeshindwa kufanikiwa, wamewakamata watu sita waliokuwa vinara akiwemo kiongozi wa wafanyakazi hao na kwenda kuwafungia rumande kwenye kituo cha Maturubahi Zakhem.

Mwananchi iliwasil eneo la tukio saa 6:30 mchana na kushuhudiwa umati wa wafanyakazi hao wakiwa wamekaa vikundi wakiwa na madumu ya maji waliyokuwa wananawa usoni kila Polisi walipokuwa wakipigwa mabomu.

Wakizungumza kwenye tukio hilo, baadhi ya wafanyakazi hao akiwemo Juma salum amesema wamefikia hatua hiyo baada ya uvumilivu kuwashinda kwa kuwa madai hayo ni ya muda mrefu.

“Kwa siku tunalipwa Sh12,500 kama mshahara wa kazi lakini kwenye mkataba unasema gharama za chakula, usafiri na makazi ambazo ni Sh7,500 na kuwa Sh 20,000 kwa siku zitajumuishwa kwenye mshahara. Kwa miaka miwili sasa hatuoni ukijumuishwa,”amesema
Amesema imefikia kipindi wamechoka licha ya madai yao kupelekwa serikalini ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo na kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla lakini hayafanyiwi kazi.

Viongozi wa kampuni hiyo hawajapatikana kuzungumzia tukio hilo, kwani walikuwa wamejifungia kwenye ofisi zao, huku mara kwa mara wakichungulia dirishani.

Hata hivyo Mwananchi limemtafuta Kamanda mkoa wa kipolisi Temeke, Richard Ngole aliyekiri kufahamu tukio hilo na kwamba baadhi ya watu wanashikiliwa.

"Ni kweli tunawashikilia baadhi ya watu kwa kuwa wamegoma kufanya kazi, sisi kama jeshi la polisi shughuli yetu ni kulinda usalama wa raia pamoja na mali zao,"ameeleza Kamanda Ngole kwa njia ya simu.

Baadaye Mwananchi lilimtafuta Mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kwa nyakati tofauti kujua kama wanafahamu kinachoendelea kwenye eneo hilo,lakini simu zao zilikuwa zinaita muda mwingi bila kupokelewa

MCL

1.jpg
 

Ngwakwiii

Senior Member
Dec 6, 2019
129
250
Sino hydro ya babati, singida ndo hii hii tuu bado yatesa watu,
Yaani mpaka leo any way sitokaa hata kama nina shida ya namna gani kufanya kazi kwenye hii kampuni
 

Mr Spider

Member
Feb 28, 2020
67
125
Polisi haikuwa na ssbabu ya kupiga mabomu kama suala la mgomo wa kudai stahiki ni suala la haki ya mfanyakazi
Jeshi la Polisi kwa nyakati hizi ni kama lina ugomvi na wananchi, na ndiyo maana Hamza aliyetenda lile tukio wananchi baadhi walifurahi na jeshi la polisi nalo limekuja na ripoti ya uchunguzi ambayo haihawaingia akilini walio wengi. Nchi yetu inahitaji Kupata Rais kiunganishi wa taifa... Haijalishi atatokea chama gani lakini kwa hali hii ni picha mbaya sana kwenye taifa letu.
 

Mr Spider

Member
Feb 28, 2020
67
125
Mwananchi iliwasil eneo la tukio saa 6:30 mchana na kushuhudiwa umati wa wafanyakazi hao wakiwa wamekaa vikundi wakiwa na madumu ya maji waliyokuwa wananawa usoni kila Polisi walipokuwa wakipigwa mabomu.

Ndugu Mwandishi mchana wa tarehe 6 September 2021, bado haujafika naomba urekebishe hapo tujue muda sahihi wa tukio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom