Taharuki baada ya fununu za wapima tezi dume kupita nyumba baada ya nyumba

kanali mstaafu

JF-Expert Member
May 17, 2015
4,319
4,089
Jana nikiwa natoka job nilipita kwenye mchezo wa bao ili kama ilivyo kawaida yangu. Nilikuta story zimezagaa eti jopo la wapima tezi dume linapita nyumba kwa nyumba. Wanaume walikuwa wamehaha huku wakikwepa kurudi nyumbani mapema na kuahidi kudamka kukwepa hii kadhia. Ww Makonda naomba tuheshimiane. Na baridi yotee hii kidole tena kije huko ama watutakia nini??. Anzia wewe na jiwe mpimwe mjitangaze hadharani na kisha sisi tutafata.
 
tezi dume haipimwi kwa vidole siku hizi!!
lakini pamoja na yote Muache kuyakuza mambo !
KITAALUMA HAKUNA MTU ANAEWEZA KUPIMWA KWA NGUVU!
Huo utaratibu wa nyumba kwa nyumba HAUPO by UMMY MWALIMU
 
Ila wanaume wa Dar mna matatizo sana. Yan mnaogopa kurudi nyumbani kisa hao wapimaji.? Anapata ujasiri wapi wa kunipima bila ridhaa yangu.? Anaanzia wapi kunigusa kabla sijamruhusu mimi.? Hata wakija kumi sidhani kama kuna sheria inasema watu wapimwe kwa lazima.

Siwezi kuongozwa na akili za kisukuma. Kuweni na amani hakuna kitu kama hicho.
 
Back
Top Bottom